My point is, umekosa huo "msaada" sehem uliyotaka, kwahiyo unafanya nini, unakufa? Unakaa chini unalia kama mtoto mdogo? Unaacha wazo lako life? Mtu anayetakiwa kulifanya wazo lako lifanikiwe ni wewe, siyo ndugu yako. Man up and move on. Acha kukaa ukiwaza wengine wanamiteremko kwa sababu aaabeechee, unaonekana wa ajabu kukaa ukilialia mitandaoni kumlaum "blaza" wako. Sina mafanikio ya kihivyo ndugu mi naganga tu kama mwananchi wa kawaida, lakini sijawahi kumtegemea mzazi wala ndugu zaidi ya kulipiwa ada mwisho A-Level, chuo nilijilipia, nimiaka ishirini iliyopita lakini sijawahi kuwasilisha shahada yangu popote kuomba kazi wala sijaomba mtaji kwa jamaa yeyote kwa sababu siamini katika ujamaa! Acha kushinda nyuma ya keyboard, toka nje ya huo mji ujifunze maisha.