Mahafali ya Chuo kikuu Dodoma; Rais Magufuli atunukiwa shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa

BEN SAANANE upo wapi ndugu???? Huku kutunukiwa sio bure ni kuhalalisha.

Kumbuka alivyokigawa kivuko kwa jeshi ili kuhalalisha.
 
UDOM si walikuwa na ziada ya majengo ata wakazipa taasisi za serikali zifanye ofisi. Mbona inanishangaza wanaitaji billion izo kwa ajili ya majengo tena
 
Pesa watu wanazo za kutosha ila linapokuja swala la mahafali ukumbi umejaa wasomi yani ukiangalia hadi unahisi kusisimkwa,kuna ka raha flani ukiwa na mashahada ya namna hii mjue nyie chukulieni poa.
 
We jamaa acha uongo mimi nimeenda pale na CBB alafu una sema nini. Acha kugeneralize mambo. Na nimegraduate poa tuu ila mziki wa pale Natural Science sitakaa niusahau
Siyo kweli mkuu kuna dogo namfahamu alidahiliwa pale 2012 Bsc.Maths alikuwa na dv 1.5 PCM
 
We jamaa acha uongo mimi nimeenda pale na CBB alafu una sema nini. Acha kugeneralize mambo. Na nimegraduate poa tuu ila mziki wa pale Natural Science sitakaa niusahau

Kitu kinachoshangaza ni aina ya mtaalamu UDOM wamemtumia kupata estimates za ujenzi na ukarabati wa hizo Ndaki na Ukumbi. Juzi Waziri Mkuu wamewaondoa katika nafasi zao watendaji wa TBA kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa jengo la NEC, pia gharama zimepaa toka 10 bilioni, 13 bilioni hadi 32 bilioni hadi Waziri Mkuu akashangaa! Kumbukeni pia waliondolewa kule Ukonga, wakapewa JKT na wanalalamikiwa na Halmashauri za Wilaya nyingi tu kwa kutomaliza kazi mapema na ubora wake.
 
Sasa hiyo ni habari nyingine hapo kuna upigaji.
Kitu kinachoshangaza ni aina ya mtaalamu UDOM wamemtumia kupata estimates za ujenzi na ukarabati wa hizo Ndaki na Ukumbi. Juzi Waziri Mkuu wamewaondoa katika nafasi zao watendaji wa TBA kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa jengo la NEC, pia gharama zimepaa toka 10 bilioni, 13 bilioni hadi 32 bilioni hadi Waziri Mkuu akashangaa! Kumbukeni pia waliondolewa kule Ukonga, wakapewa JKT na wanalalamikiwa na Halmashauri za Wilaya nyingi tu kwa kutomaliza kazi mapema na ubora wake.
 
UDOM si walikuwa na ziada ya majengo ata wakazipa taasisi za serikali zifanye ofisi. Mbona inanishangaza wanaitaji billion izo kwa ajili ya majengo tena
Majengo yaliyokuwa yanatumiwa na serikali ni majengo ya ndaki ya elimu ya biashara na sheria (CBSL), pesa zilizotajwa ni kujenga ndaki sayansi asilia na hisabati (CNMS) pamoja na ndaki ya sayansi ya dunia na uhandisi (CoESE)
 
We jamaa acha uongo mimi nimeenda pale na CBB alafu una sema nini. Acha kugeneralize mambo. Na nimegraduate poa tuu ila mziki wa pale Natural Science sitakaa niusahau
Umeelewa post yangu vizuri?nilikuwa namjibu mdau juu kuwa siyo kweli wanaodahiliwa pale ni wale wenye DD tu nikatoa huo mfano wa dogo aliyeenda pale akiwa na one yake kali tu
 
We jamaa acha uongo mimi nimeenda pale na CBB alafu una sema nini. Acha kugeneralize mambo. Na nimegraduate poa tuu ila mziki wa pale Natural Science sitakaa niusahau
Uongo wangu ni upi?
 
1574343116456.png

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, amevitaka vyuo hapa nchini kujikita kufanya utafiti mbalimbali ambazo zitakuja na suluhisho la kutatua Changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zetu.

Pia amevitaka vyuo hivyo vitafute mbinu ya kuhakikisha vinazalisha watimu wanaoweza kujiajiri na sio kutegemea kuajiliwa na umma.

Dkt. John Magufuli ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika maafali ya kumi(10) ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, UDOM, ambapo pia ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa, katika chuo hicho, ambapo wahitimu takribani elfu sita(6000) watatunukiwa Shahada mbalimbali.

Dkt. Magufuli amesema vyuo vinawajibu wa kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitasaidia kuja na suruhisho la kutatua changamoto mbalimbali katika jamii .

"Vyuo vyetu hivi vijitahidi kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitasaidia Jamii hasa katika kilimo, ufugaji na viwanda na pia uchimbaji wa madini, tafiti hizo ziwasaidie wakulima, namna ya kufaidika na shughuri zao"

"Pia vyuo hivi vijikite katika kuzalisha wahitimu ambao wataweza kujiajiri na sio kuzalisha wahitimu wa kuja kuajiriwa na Umma, na ninyi wahitimu mkawe Chachu katika kuziondoa changamoto zilizopo katika jamii na sio ninyi kwenda kuwa changamoto katika jamii" amesema Dkt Magufuli.

Aidha amesisitiza kwa serikali na taasisi mbalimbali mbali kujenga Utamaduni wa kutumia wataalamu wanaozalishwa ndani ya nchi, ili kupunguza gharama kubwa na kupunguza wasomi ambao wamehitimu na hawana kazi ya kufanya.

Pia ameelezea mafanikio ambayo yamepatikana katika awamu ya tano, kuwa serikali imefanya Mambo mengi ikiwamo, ununuzi wa ndege, upanuzi wa viwanja vya Ndege, na ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege msalato ambao itawezesha ndege yoyote duniani kutua.

Ameongeza kuwa mengine,ni "Kubana matumizi kwa serikali, kuondoa watumishi hewa, kuzuia safari za nje ya nchi, kukarabati shule kongwe na vyuo vya ufundi, pamoja na kuongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu, na kutoa elimu bure" amesema.

Mbali na mafanikio hayo amesema zipo changamoto ambazo zinajaribu kukwamisha juhudi hizo kuwa ni mabeberu, vibaraka wa ndani na nje ya nchi ambao wanajaribu kukwamisha juhudi hazo na kusema hawata kata tamaa na wataendelea kuwatumikia wananchi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ametunukiwa shahada ya heshima ya Udaktari wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Dodoma kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya kwanza ya uongozi wake. Hakika amestahili.

Sisi wananchi tutamtunuku ya kwetu mwakani ambayo ni: #T2020JPM

IMG_20191121_162959_109.jpeg
 
View attachment 1268303

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, amevitaka vyuo hapa nchini kujikita kufanya utafiti mbalimbali ambazo zitakuja na suluhisho la kutatua Changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii zetu.

Pia amevitaka vyuo hivyo vitafute mbinu ya kuhakikisha vinazalisha watimu wanaoweza kujiajiri na sio kutegemea kuajiliwa na umma.

Dkt. John Magufuli ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika maafali ya kumi(10) ya Chuo Kikuu Cha Dodoma, UDOM, ambapo pia ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa, katika chuo hicho, ambapo wahitimu takribani elfu sita(6000) watatunukiwa Shahada mbalimbali.

Dkt. Magufuli amesema vyuo vinawajibu wa kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitasaidia kuja na suruhisho la kutatua changamoto mbalimbali katika jamii .

"Vyuo vyetu hivi vijitahidi kufanya tafiti mbalimbali ambazo zitasaidia Jamii hasa katika kilimo, ufugaji na viwanda na pia uchimbaji wa madini, tafiti hizo ziwasaidie wakulima, namna ya kufaidika na shughuri zao"

"Pia vyuo hivi vijikite katika kuzalisha wahitimu ambao wataweza kujiajiri na sio kuzalisha wahitimu wa kuja kuajiriwa na Umma, na ninyi wahitimu mkawe Chachu katika kuziondoa changamoto zilizopo katika jamii na sio ninyi kwenda kuwa changamoto katika jamii" amesema Dkt Magufuli.

Aidha amesisitiza kwa serikali na taasisi mbalimbali mbali kujenga Utamaduni wa kutumia wataalamu wanaozalishwa ndani ya nchi, ili kupunguza gharama kubwa na kupunguza wasomi ambao wamehitimu na hawana kazi ya kufanya.

Pia ameelezea mafanikio ambayo yamepatikana katika awamu ya tano, kuwa serikali imefanya Mambo mengi ikiwamo, ununuzi wa ndege, upanuzi wa viwanja vya Ndege, na ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege msalato ambao itawezesha ndege yoyote duniani kutua.

Ameongeza kuwa mengine,ni "Kubana matumizi kwa serikali, kuondoa watumishi hewa, kuzuia safari za nje ya nchi, kukarabati shule kongwe na vyuo vya ufundi, pamoja na kuongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu, na kutoa elimu bure" amesema.

Mbali na mafanikio hayo amesema zipo changamoto ambazo zinajaribu kukwamisha juhudi hizo kuwa ni mabeberu, vibaraka wa ndani na nje ya nchi ambao wanajaribu kukwamisha juhudi hazo na kusema hawata kata tamaa na wataendelea kuwatumikia wananchi.
Thesis yake ya Phd ilisaidiaje umma ya Tz ?
 
Back
Top Bottom