The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Mahakama moja nchini Israel imekataa ombi la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kuahirisha kusikilizwa kwa kesi yake dhidi ya rushwa, baada ya rais wa Marekani Donald Trump kutaka kesi hiyo ifutiliwe mbali.
Wakili wa Netanyahu alimuomba jaji katika mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo kwa wiki mbili, akisema kiongozi huyo anahitaji kushughulikia masuala ya usalama baada ya siku 12 za vita kati ya Israel na Iran.
Mahakama imesema ombi lililotolewa halina msingi au uhalali wa kuahirisha kusikilizwa kesi hiyo. Siku ya Jumatano wiki hii Trump aliielezea kesi dhidi ya Netanyahu kuwa ya kisiasa na kutaka ifutiliwe mbali mara moja au msamaha utolewe kwa kiongozi huyo aliyomuita shujaa.
Netanyahu amemshukuru Trump kumuunga mkono katika vita vyake na Iran vilivyositishwa Juni 24 kwa makubaliano ya kusitisha vita, yaliyotangazwa na Donald Trump. Waziri Mkuu huyo wa Israel amekanusha kuhusika na rushwa huku wafuasi wake wakisema kesi yake inaendeshwa kisiasa.