Mahakama itoe hati ya kumkamata kiongozi wa dini aliyesema Rais amfutie kesi Mbowe

Mahakama itoe hati ya kumkamata kiongozi wa dini aliyesema Rais amfutie kesi Mbowe

Shule za kata
kwa sasa limeisha hilo.
kesi imeondolewa lkn kama ingekuwa inaendelea basi utaratibu ungebaki plepale.
Ni hatari kwa afya ya ubongo wako. Wizi wa mitihani ni hatar zaidi kwa akili yako.
Haya sema tena. Endelea kujichokonoa na kunusa
 
Naunga mkono hoja ,haiwezekani Kama taifa kuhamishiwa kwenye mijadara ya ajabu utadhani Tanzania hii Kuna Mbowe pekee,tuna watanzania wengi Sana wenye kuhitaji huruma ya rais lakini leo hii the talk in town imekuwa juu ya huyu gaidi Mbowe ,huu Ni upuuzi.

Hao viongozi wa dini waende kuhubiri habari za uzinzi na ulevi, mambo ya sheria wawaachie Wanasheria.

Mbona sijawahi hata siku moja kuona mwanasheria akiwasemea au kuwaingilia watumishi wa mungu?
viongozi wa dini pigeni kelele na sabaya apewe msamaha wa rais au kesi ifutwe tu
 
Ndo ashafutiwa kesi unateseka kutokea wapi?
 
Kiongozi wa dini aliye muomba Mh. Rais amfutie kesi Mbowe na wenzake ni kosa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ameingilia mchakato wa mahakama ktk kutoa haki.

Tamko la kiongozi huyo wa dini limeonyesha wazi kuidharau mahakama na kuingilia taratibu za mahakama.

Kiongozi huyo wa dini anafahamu wazi kuwa kesi hiyo ipo Mahakamani na inaendelea kusikilizwa na ni kosa kuizungumzia kesi iliyoko Mahakamanii lkn kwa maksudi kabisa Kiongozi huyo wa dini akaamua kutamka neno hilo la kuvuruga na kuingilia utaratibu wa mahakama.

kitendo hicho sio tu kaidharau Mahakama bali ameidhihaki na kuiona mahakama si chochote sio lolote, hivyo endapo mahakama haitochukua hatua ktk vitendo/kitendo kama hiki basi Mahakama itakuwa sio chombo cha kutoa haki.

Kama leo Vingozi wa dini wanadiriki kuto kuheshimu Muhimili wa Mahakama kwa kuomba eti Rais mfutie kesi Mbowe basi tutegemee siku nyingine pia wataomba Pia Sabaya afutiwe kesi. Tutavuruga nchi yetu kama hatuto heshimu utawla wa sheria.

Viongozi wetu wa dini tunawaonba wawe makini na matamko yao ambayo yanaweza kuleta utata na kuvuruga taratibu za nchi, wajiepushe kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa wazi wazi kwani watatugawa sisi waumini wao, lengo la viongozi wa dini ni kutuunganisha sio kutugawa kwa misingi ya kisiasa, kama tunavyo muona baba askofu wamkula na wengine ambao mara zote wanatugwa kwa misingi ya kisiasa.

Hivyo ili kulinda uhuru na hadhi ya mahakama ni vyema Kiongozi huyo wa dini akamatwe na afikishwe mbele ya mahakama ili aweze kujibu tuhuma za kuingilia na kudhihaki taratibu za Kimahakama.

Utawala wa Sheria lazima uheshimiwe kwa kuviheshimu vyombo vyetu vilivyo pewa mamlka kwa mujibu wa Katiba.
Hata hivyo rais hajamfutia kesi Mbowe
 
Kwanza hapo huyo Kiongozi wa Dini ameingiliaje Mahakama wakati ameongea na Mhimili mwingine tofauti.Kama angemwambia Jaji amuone mshtakiwa hana hatia hapo kweli angekuwa ameingilia Mahakama
 
Sijui iitwe pumba....au ni mtu tu kuwa mweupe....au ni makosa tu ya kumiliki simu hivyo mtu anaamua tu kupost pumba
 
ni jambo la busara kwa Mbowe kuwaomba radhi watanzania kama alivyo washukuru walio muombea.

Jeuri, kiburi na majivuno hayasaidii,
naamini Mbowe akiwaomba radhi watanzania atakuwa amejijengea heshima mara dufu uamuzi ni wake.
 
kesi ya uamsho ilifunguliwa na watuhumiwa walisota mahabusu zaidi ya mika 8 bila kesi kusikilizwa.....kesi yao haijawahi kusikilizwa ktk kipindi cha miaka 8, tofauti na kesi ya Mbowe imesikilizwa na sasa inaelekea kwenye Hukumu, sasa ktk mazingira hayo unaanzaje tena kumuomba Rais eti afute kesi?!

tukianza haka kamchezo, tutaanza na kesi ya Mbowe siku nyingine itakuwa kesi ya askofu, shek, waziri, Mfanyabiashara mkubwa n.k n.k.
huo ndio utakuwa mwisho wa utawala wa Sheria.............
Unajisikiaje na hii comment yako?
 
ni jambo la busara kwa Mbowe kuwaomba radhi watanzania kama alivyo washukuru walio muombea.

Jeuri, kiburi na majivuno hayasaidii,
naamini Mbowe akiwaomba radhi watanzania atakuwa amejijengea heshima mara dufu uamuzi ni wake.
Aombe radhi kwa lipi?
 
Back
Top Bottom