Mahakama kutoa uamuzi wa uhalali wa hati ya kesi ya uhaini ya Jenifer Jovin( Niffer) na wenzake 21, Novemba 25

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa uhalali wa hati ya kesi ya uhaini inayomkabili mfanyabiashara Jenifer Jovin (26), maarufu Niffer na wenzake 21, Novemba 25, 2025.

Mahakama hiyo imepanga tarehe hiyo kutoa uamuzi huo, leo Jumanne, Novemba 11, 2025, baada ya kukamilisha usikilizwaji wa pingamizi dhidi ya hati hiyo lililotolewa na jopo la mawakili wao linaloongozwa na Peter Kibatala.

Leo Mahakama hiyo imesikiliza majibu ya Jamhuri pamoja na majibu ya utetezi dhidi ya majibu ya Jamhuri.

Niffer ambaye alikamatwa mapema kabla ya siku ya kupiga kura na wenzake hao waliokamatwa siku ya kupiga kura, Oktoba 29, 2025 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, wakihusishwa na maandamano ya kupinga uchaguzi huo. Walipandishwa kizimbani mahakamani hapo Ijumaa, Oktoba 7, 2025.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Wakili Kibatala aliieleza Mahakama wateja wao walipokuwa Polisi waliteswa kwa kupigwa kwa lengo la kuwashinikiza kukubali kuandika na au kusaini maelezo yao ya onyo, na licha ya wengine kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao lakini hawakuwahi kupatiwa matibabu.

Hivyo aliomba Mahakama ielekeze msimamizi wa gereza ambako watapelekwa mahabusu iwapatie matibabu na taarifa za matibabu yao ziwasilishwe mahakamani kuwa sehemu ya kumbukumbu za kesi hiyo.

Soma Pia: Niffer na wengine 97 wafunguliwa mashtaka, yakiwemo ya UHAINI kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025

Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya anayesikiliza kesi hiyo katika hatua hiyo ya uchunguzi wa awali kabla ya kuhamishiwa Mahakama Kuu yenye mamlaka ya kuisikiliza, alikubaliana nayo na akatoa maelekezo hayo.

Pia, Kibatala alipinga hati ya mashtaka akidai ina kasoro kwa kujumuisha makosa mawili yaani kula njama na kosa mama la uhaini, ambayo hayapaswi kuwekwa katika hati moja.
 
Uhuni tu wa kutaka kuwakomoa na kuwatesa watu bila huruma.

Hapo atakuwa amepata maelekezo toka juu au anasubiri maelekezo toka juu.
 
Uonevu unaongeza chuki
 
Kuna aina za kesi kuendelea ni kudhalilisha mahakama
 
Back
Top Bottom