Mahakama Kuu Dar, imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Spika Ndugai kwa kumtambua Mwambe kama Mbunge baada ya Kujiuzulu

Mahakama Kuu Dar, imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Spika Ndugai kwa kumtambua Mwambe kama Mbunge baada ya Kujiuzulu

Tatizo lako husomi....na hiyo ni sifa moja mbaya sana ya Watz walio wengi ukiwemo.Uvivu wa kusoma!!!
Kwa mtu anayesoma au aliyesoma Katiba ya JMT hii kesi iko wazi kabisa. Tatizo ni Mahakama kupindisha na kucheza na longolongo ya kusingizia"Technicalities" ili kujaribu kuzima hoja....Non-sense!!!
Ujielewi
 
View attachment 1467675
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa uamuzi na kutupilia mbali shauri la Kikatiba Na. 10 la mwaka 2020 lililofulinguliwa na Wakili wa Kujitegemea Revocatus Paul Kaunda kupinga Kauli ya Mhe. Spika aliyoitoa Bungeni kumtambua Mhe. Cecil Mwambe kuendelea kuwa Mbunge.

Mahakama Kuu kupitia Jopo la Majaji watatu ambao ni Mhe. Jaji Issa Maige, Stephen ,Mrimi Magoiga na Seif Mwinshehe Kulita, wametupilia mbali shauri hilo kwa uamuzi kuwa "SHAURI HILO HALINA MSINGI KISHERIA NA LENYE LENGO LA KUSABABISHA USUMBUFU KWA MAHAKAMA ". Mahakama imeona kuwa hoja zilizoletwa Mahakamani hapo zinahusu kuitaka Mahakama kutoa tafsiri iwapo Mhe. Mwambe ni Mbunge au sio mbunge. Hoja hiyo ingepaswa kuletwa kupitia shauri la Uchaguzi chini ya Ibara ya 83 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio suala la Maombi ya Haki ya Kikatiba kama Mleta maombi hayo alivyofanya kupitia Ibara ya 26(2) ya Katiba. Mahakama imeona kuwa suala ambalo limejitokeza Bungeni kuhusu kukoma au kutokoma kwa Ubunge wa Mhe. Mwambe linahusu pia uamuzi wa Spika chini ya Kifungu cha 37 Cha Sheria ya

Katika shauri hilo Mleta Maombi waliwakilishwa na Wakili Daimu Halgfani, Steven Mwakibolwa, Fulgence Massawe. Mwambe aliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea Raphael na Upande wa Mhe Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamewakilishwa na Bw. Vicent Tangoh (Wakili wa Serikali) Mkuu) , Bw. George Mandepo (Wakili wa Serikali Mkuu), Bibi Alesia Mbuta (Wakili wa Serikali Mkuu), Bw. Erigh Mrisha (Wakili wa Serikali) na NBibi Narindwa Sekimanga.

Mahakamani hapo leo pia, Mahakama ilitaja kesi inayofafana iliyofunguliwa na Arusha na kuhamishiwa Masijala ya Dar es Salaam. Kesi hiyo Na. 12 ya 2020 imefunguliwa na Asasi iliyo ya Kiserikali ya Civic and Legal Organisation ikipinga pia ubunge wa Mhe. Mwambe. Wadawa katika kesi hiyo ya kikatiba ni Mhe. Spika , Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Cecil Mwambe.

Kesi hiyo itakuja kwa kutajwa tena Mahakamani hapo tarehe 11 Juni, 2020.

=====

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai akiomba mahakama hiyo kutengua amri ya Spika kumtambua Cecil Mwambe kama mbunge halali wa Ndada ikisema amekosea kufungua shauri hilo.

Mbali na Ndugai, walalamikiwa wengine katika shauri hilo ni aliyekuwa mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mfumo wa mawakili wa Tanzania unaonesha kwamba aliefungua kesi hii bwana Revocatus Paul Kaunda ni marehemu, kwa hyo ina maana hii kesi ilifunguliwa na Marehemu????
 
Acha Usanii na ubabaishaji wewe.
Watz Wana Haki ya kuhoji na kuona Sheria na Katiba inazingatiwa pale WATAWALA WA CCM. wanapoingia Sheria na taratibu za nji kwa interests zao.
Cecil Mwambe hakupaswa na hapashwi kuwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba ya JMT. Yeye alishajiuzulu Uanachama wa Chama kilichomtokea Bungeni kwa kura za Wananchi...!

Tatizo ni kwamba JIWE na Serikali yake ya majambazi ya CCM wamaiteka mihimili ya Mahakama na Bunge kiasi kwamba inacheza ngoma inayosikika na JIWE....!!

Hii ilikuwa ni kesi ya Kikatiba na kulikuwa na hoja ya msingi kabisa hata kama Kuna dosari za kiufundi katika kufungua shauri hili!! lakini kwa vile waloguswa ni Vigogo wa Chama Twawala lazima kesi itupuliwe mbali ili kulinda maslahi ya majambawazi ya CCM!
Namiomba sana Mungu hawa Majaji wanao amua kesi kwa maslahi ya amri za kutoka juu wewe hai hadi utakapo patikana uongozi wa nchi unao fuata sheria na kutii viapo vyao. Maana hivi sasa siamini kama kuna majaji/mahakimu wanao tafsri sheria.
Ati jaji anasema mahakama ina sumbukiwa?? Kweli?? Hivi wana thubutu kujiita majaji kweli?? Mungu yupo
 
Wakuu m;eta taarifa anasema kwamba aliefungua kesi ni wakili wa mahakama kuu kwa maana hyo anatambulika na mfumo wa mawakili tanzania kwa maana ya wakili anaeitwa ''PAUL REVOCATUS KAUNDA'' Lakini mfumo wa mawakili Tanzania(tams) unamtambua mtu anaeitwa
Wakili wa Kujitegemea Revocatus Paul Kaunda
Wakuu katika mfumo wa Mawakili Tanzania hakuna wakili anaetambulika kwa jina la "REVOCATUS PAUL KAUNDA" na hata kwenye Petition husika petitioner ni "PAUL REVOCATUS KAUNDA" na kwenye mfumo wa Mawakili Tanzania Wakili anaetambulika ambae mfumo unaonesha ni Marehemu ni "REVOCATUS KULWA PAUL KAUNDA" Je huyu aliefungua kesi anasemekana ni wakili kujitegemea wa Mahakama kuu mbona kwenye mfumo wa Mawakili Huko TANZANIA Hayumo???
 
Ndyo mjue hii nchi inawenyewe. Nyie endeleeni kuwa wasindikizaji tu.
 
Hahaha nilijua tu, mahakama zenyewe zimejazwa makada wa CCM ulitegemea nini
Nchi hi kamwe haitakuwa huru Kama Sheria za nchibzinafinyangwa namna hiyo.Mm naona itungwe Sheria ili mgombea binafsi aruhusiwe kugombea.Kama mtu anajivua uanachama mwenyewe lkn Bado anatambulika kuwa mbunge ni vioja vya Karne.
 
Ok noted and thanks

Wanasiasa wanapotezea watu muda wa kufanya kazi

Kila mtu apambane na hali yake

Liwe Bunge au Mwambe kila mtu anaangalia familia yake

Kwa ufupi wananchi angalieni maisha yenu
VIONGOZI WASIPOFUATA UTARATIBU LAZIMA TUWAAMBIE KUKAA KIMYA HAKUSAIDII
 
View attachment 1467675
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa uamuzi na kutupilia mbali shauri la Kikatiba Na. 10 la mwaka 2020 lililofulinguliwa na Wakili wa Kujitegemea Revocatus Paul Kaunda kupinga Kauli ya Mhe. Spika aliyoitoa Bungeni kumtambua Mhe. Cecil Mwambe kuendelea kuwa Mbunge.

Mahakama Kuu kupitia Jopo la Majaji watatu ambao ni Mhe. Jaji Issa Maige, Stephen ,Mrimi Magoiga na Seif Mwinshehe Kulita, wametupilia mbali shauri hilo kwa uamuzi kuwa "SHAURI HILO HALINA MSINGI KISHERIA NA LENYE LENGO LA KUSABABISHA USUMBUFU KWA MAHAKAMA ". Mahakama imeona kuwa hoja zilizoletwa Mahakamani hapo zinahusu kuitaka Mahakama kutoa tafsiri iwapo Mhe. Mwambe ni Mbunge au sio mbunge. Hoja hiyo ingepaswa kuletwa kupitia shauri la Uchaguzi chini ya Ibara ya 83 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio suala la Maombi ya Haki ya Kikatiba kama Mleta maombi hayo alivyofanya kupitia Ibara ya 26(2) ya Katiba. Mahakama imeona kuwa suala ambalo limejitokeza Bungeni kuhusu kukoma au kutokoma kwa Ubunge wa Mhe. Mwambe linahusu pia uamuzi wa Spika chini ya Kifungu cha 37 Cha Sheria ya

Katika shauri hilo Mleta Maombi waliwakilishwa na Wakili Daimu Halgfani, Steven Mwakibolwa, Fulgence Massawe. Mwambe aliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea Raphael na Upande wa Mhe Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamewakilishwa na Bw. Vicent Tangoh (Wakili wa Serikali) Mkuu) , Bw. George Mandepo (Wakili wa Serikali Mkuu), Bibi Alesia Mbuta (Wakili wa Serikali Mkuu), Bw. Erigh Mrisha (Wakili wa Serikali) na NBibi Narindwa Sekimanga.

Mahakamani hapo leo pia, Mahakama ilitaja kesi inayofafana iliyofunguliwa na Arusha na kuhamishiwa Masijala ya Dar es Salaam. Kesi hiyo Na. 12 ya 2020 imefunguliwa na Asasi iliyo ya Kiserikali ya Civic and Legal Organisation ikipinga pia ubunge wa Mhe. Mwambe. Wadawa katika kesi hiyo ya kikatiba ni Mhe. Spika , Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Cecil Mwambe.

Kesi hiyo itakuja kwa kutajwa tena Mahakamani hapo tarehe 11 Juni, 2020.

=====

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai akiomba mahakama hiyo kutengua amri ya Spika kumtambua Cecil Mwambe kama mbunge halali wa Ndada ikisema amekosea kufungua shauri hilo.

Mbali na Ndugai, walalamikiwa wengine katika shauri hilo ni aliyekuwa mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
HAYA YANAMWISHO
 
ndo uone sasa wewe ambaye kila siku unapga kelele mbowe kuwa hafai uenyekiti , huyo mwambe wako kwa taarifa ndo alipitishwa na kamati kuu ya CCM aje kuwa mwenyekiti wa chadema, wajanja wakamchinjia baharini.
MWANZONI NILIKUWA UPANDE WA MWAMBE ILA MAMBO YANAVYOENDA NIKATAMBUA LILIKUWA PANDIKIZI BORA WALIVYOMFUKUZA
 
Mchezo wa kuhalalisha matumizi ya ruzuku

Chuki dhidi ya viongozi wanaopingana na mwenye chama

Kuwakomoa viongozi wanaohama CHADEMA
 
Back
Top Bottom