Uzuri ni kwamba updates za kesho kila mwananchi anazo. Ili kujua kua huyu Jaji hajatenda haki kabisa kwa watuhumiwa na huenda angeendelea na hii kesi angewafunga. Hatuhitaji degree kuelewa kua Jaji Mustapha Siyani alitumika kuibeba Jamhuri kwa ukweli ulio wazi. Mimi pia kwa taaluma yangu ya sheria ingawa sifanyi uwakili nimeona haya;
1. Kuhusu kuchukuliwa maelezo nje ya muda. Polisi wanatoa sababu ya kuchukua maelezo nje ya muda kwa sababu waliondoka na Mtuhumiwa Adamoo kwenda Moshi na Arusha kumtafuta Moses Lijenje aliyetoroka, Lakini Adamoo anasema kuwa hajawahi kwenda Moshi wala Arusha zaidi ya kupelekwa Dar es Salaam. Polisi hawaonyeshi popote ikiwa waliandika kwenye Registar book kua walitoka kituoni kwenda Arusha na Moshi, Polisi hawatoi ushahidi wowote kua walienda Arusha au Moshi nani aliwaona na waliongea labda na polisi wa Moshi na Arusha, Wala hawakuonesha kua huko Moshi na Arusha waliongea na ndugu gani wa Moses Lijenje.
2. Kuhusu Adamoo kuchukuliwa Maelezo kwa kuteswa. Afande Kingai anasema walimchukua Maelezo Central Dar es salaam. Hapa Adamoo anasema wakati anateswa akitundikwa juu kama Popo na Mishikaki alikua akipigwa huku akichukuliwa maelezo ambayo alikuja kuyasaini akiwa Mbweni na wala hakupewa muda wa kuyasoma.
Wake wa watuhumiwa walisema Mahakamani kua walienda Central Polisi baada ya kuambiwa kua walishasafirishwa wakiwatafuta waume zao lakini wakaambiwa hawapo, walipewa mpaka Registar book hawakuwaona, hivi unachukuaje maelezo ya mtuhumiwa hayupo kwenye Registar book? Jaji Siyani haya yote hakuyaona? Hivi hizi dhambi anazobeba Jaji,anadhani ataishi milele kwa mateso ya hawa watu?