Hata Yesu anayeaminiwa na Mwingira aliwakandia viongozi lakini sio kwa style ya Mwingira ambaye nyuma ya pazia ni mnyang'annyi na mfanya biashara mashuhuri kama kina Barabas. Mtume hajifagilii mwenyewe. Kila ajikwezaye atadhiliwa na kila ajidhiliye atakwezwa.
Historia ya uendeshaji wa kiroho wa Mwingira umejaa shaka tupu, lakini ajuaye kuhukumu vizuri ni Mungu mwenyewe. Mwenzake Kakobe alijifagilia sanaaa lakini somo limeanza kupanda kichwani kidogo siku hizi japo baaaaado kabisa. Watenda kazi wa Mungu wa kweli kwa kawaida ni vigumu kuwaona ila kwa kazi zao, nao wapo wengi tu. Kila debe lililo tupu hutika mno!
Paulo alionya sana, lakini maonyo ya Paulo si rahisi watu kama Mwingira wakafurahia kuyafanyia kazi, achilia mbali kuyatafakari kwa ajili yao wenyewe. Kawaida watu wa style ya Mwingira kila asomapo Maandiko anatafakari kwa namna ya kumhusu anayekwenda kumhubiri, yeye mwenyewe anadhani hayamhusu maana tayari anadhani amekubaliwa na Mungu. Hilo nalo, ni tatizo kubwa.