Mahakama Kuu Nigeria Yatoa Amri ya Zuio Kwa Muigizaji Lizzy Kutom-post Mtoto wa Jux na Priscilla

Mahakama Kuu Nigeria Yatoa Amri ya Zuio Kwa Muigizaji Lizzy Kutom-post Mtoto wa Jux na Priscilla

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mahakama Kuu ya Jimbo la Lagos nchini Nigeria imetoa amri ya muda inayomzuia muigizaji wa Nollywood, Liz Anjorin, kuchapisha au kusambaza picha na maudhui yoyote yanayomhusu mtoto wa Priscilla Ojo na msanii Juma Jux, aitwaye Rakim, kwenye mitandao ya kijamii .

Amri hiyo iliyotolewa kufuatia ombi la dharura lililowasilishwa na familia ya Priscilla na Jux, inamzuia muigizaji huyo kutumia akaunti zake za Instagram, Facebook, WhatsApp, na TikTok kutangaza au kupakia taarifa zozote zinazomhusu mtoto huyo au wazazi wake hadi pale mahakama itakapomaliza kusikiliza shauri hilo.

Chanzo cha mgogoro huu kinatokana na ugomvi wa muda mrefu uliopo kati ya Liz Anjorin na muigizaji mwenzake Iyabo Ojo, ambaye ni mama mzazi wa Priscilla Ojo.

Baada ya Jux na Priscilla kupata mtoto wao, Liz Anjorin anadaiwa kuanza kuchapisha video zilizoibua maswali kuhusu kuzaliwa kwa mtoto Rakim na hata kutaka wakutane mahakamani kuthibitisha madai yake.

Hali hiyo iliwalazimu Jux na Priscilla kuchukua hatua za kisheria wakieleza kuwa uchapishaji wa picha za mtoto wao bila idhini unakiuka faragha ya mtoto na kuharibu heshima ya familia yao.
1788760607190.png
 
Back
Top Bottom