Mahakama Kuu ya Kenya imeamuru kukamatwa kwa raia wa Uingereza anayetuhumiwa kumuua Agnes Wanjiru karibu na kambi ya mafunzo ya jeshi la Uingereza huko Nanyuki miaka 13 iliyopita. Mwili wa Agnes Wanjiru, mwenye umri wa miaka 21, ulikutwa ndani ya shimo la choo mnamo Aprili 2012, wiki chache baada ya kushuhudiwa akiondoka na wanajeshi wa Uingereza kutoka baa moja. Ingawa mahakama imeamuru kukamatwa kwa mtuhumiwa aliye nchini Uingereza, haikutaja jina lake
Familia ya Wanjiru imesema kuwa wamekuwa wakingoja haki kwa muda mrefu sana na sasa wanatumai itatimizwa. Esther Muchiri, msemaji wa familia, amesema kuwa uamuzi huu ni hatua ya mbele, lakini si haki kamili bado. Amehoji kwa nini baada ya miaka 13 bado jina la mtuhumiwa linafichwa, akisisitiza kwamba familia inahitaji majibu ya kweli na uwazi
Uingereza kupitia Waziri wa Ulinzi John Healey, tayari ilikuwa imeahidi kusaidia familia ya Wanjiru kupata haki, huku ubalozi wa Uingereza ukirejelea kujitolea kwake kwa suala hilo lakini ukikwepa kusema iwapo ombi la kumrejesha mtuhumiwa Kenya limeshaanzishwa. Wakati huo huo, wasiwasi umeendelea kuibuliwa na wakazi kuhusu jinsi vikosi vya Uingereza vinavyowatendea wananchi na mazingira karibu na maeneo yao ya mafunzo nchini Kenya
Source: Africana news