Mahakama Kuu yaamuru Polisi kumfikisha Mahakamani Neema Mwakipesile wa BAWACHA Agosti 12, 2021

Mahakama Kuu yaamuru Polisi kumfikisha Mahakamani Neema Mwakipesile wa BAWACHA Agosti 12, 2021

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Polisi wenu wamemuachia HURU Bi. Neema Mwakipesile Sakalile baada ya mawakili wetu kupeleka Habeas Corpus mahakamani na kesi kupangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM... Muda huu wamemuachia baada siku 15.. Huu ni UONEVU!

Mawakili wetu muda huu wamepata 'summons' (wito) ya kesi ya Neema Sakalile Mwakipesile. Ni case Number 156 ya mwaka 2021 imepangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Mhe. Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM.

Hatua hii imekuja baada ya Mawakili wake kuripoti Mahakamani unlawful detention ya mteja wao na wakaiomba mahakama kutoa amri ya kuletwa mbele ya Mahakama. Kisheria inaitwa "Habeas corpus"
 
Narudia tena, tuna Jeshi la ajabu mno na linatia aibu sana sana, wamemshikilia kwa siku kibao, Mawakili wa Chadema wameenda mahakamani, Polisi wameona mambo yanakua magumu wamemuachia.

Polisi wenu wamemuachia HURU Bi. Neema Mwakipesile Sakalile baada ya mawakili wetu kupeleka Habeas Corpus mahakamani na kesi kupangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM... Muda huu wamemuachia baada siku 15.. Huu ni UONEVU!
 
Jana kwenye Space hili jambo lilijadiliwa kwa kirefu jinsi walivyonyanyasa Dada wa Watu bila kosa.

Walivyoulizwa wakasema eti "TISS" ndio waliomkamata kwa makosa ya mtandao! Tangu lini TISS wakakamata na kuweka watu mahabusu?

Leo wameona moto wa Jana kwenye Space wameamua kumuachia faster, kuna siku watajichanganya wataingia cha kike
 
Mbona nasikia wamemuachia arudi Nyumbani. Sasa huko Mahakamani sijui wataenda kujielezaje.
 
kamwe Demokrasia ya Vurugu haikubaliki ktk nchi hii ya Tanzania.

Vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama kamwe havito mvumilia mtu yeyote yule atakaye jifanya yeye anaijua sheria zaidi ya Jeshi la polisi.
lazima tujifunze adabu ya kuheshimu sheria zetu.

hakuna aliye juu ya sheria uwe ccm, uwe chadema au huna chama lazima uwe na adabu.

kama ange fanya mambo yake angepata usumbufu huu wa kulala mahabusu?

wakati mwengine ni kujitakia matatizo tu.
 
Hivi Sirro hajui kuwa kuna siku kibao kinaweza mgeukia?!
OMARI MAHITA , IGP ambaye rekodi yake ya ukatili bado haijavunjwa , baada ,ya kustaafu aliburuzwa mahakamani kwa kesi ya fedheha ya ubakaji wa House girl wake mwenyewe na kumjaza mimba , halafu kukataa matunzo ya mtoto , baada ya mtoto kuletwa mahakamani kama kielelezo hata vipofu waliona , yaani mtoto ni mahita copyright !

Si ccm aliyoipigania wala jeshi la polisi alilolitumikia lililoweza kumuokoa na aibu ile , hili jambo liwe funzo kwa IGP wa sasa
 
kamwe Demokrasia ya Vurugu haikubaliki ktk nchi hii ya Tanzania.
Vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama kamwe havito mvumilia mtu yeyote yule atakaye jifanya yeye anaijua sheria zaidi ya Jeshi la polisi...
Umesoma? Na kama umesoma umeelewa? Kwahio wao Polisi ndio wana mamlaka ya kumshikilia MTU bila kumpeleka mahakamani kwa 15days plus? Ndio Kanuni zao zinavyosema?? Msiropoke mnakera
 
kamwe Demokrasia ya Vurugu haikubaliki ktk nchi hii ya Tanzania.
Vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama kamwe havito mvumilia mtu yeyote yule atakaye jifanya yeye anaijua sheria zaidi ya Jeshi la polisi...
Yaani we jamaa kwaiyo kujua sheria zaidi ya polisi ni kosa, hata hao polisi hawako juu ya sheria mahabusu mtumiwa hatakiwi kukaa zaidi ya masaa 48 Sasa huoni hapo polisi wanavunja sheria makusudi inatakiwa ifikie kipindi polisi waanze kujitambua
 
Back
Top Bottom