TLS kupitia baraza la uongozi la chama kuwaomba wananchama wote wafike ukumbi wa Pius Msekwa shule ya sheria ambapo wangezungumzia uhuru wa vyama vya taaluma ambavyo vinabana wanachama wa TLS kupitia miswada na sheria zilizotungwa kubana tasnia ya Mawakili
BUNGE LARIDHIA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA
Imewekwa: 01 Nov, 2023
Na William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesoma kwa mara ya tatu Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria wa mwaka 2023 (The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2023) na kuridhiwa na Bunge na sasa utapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo naye akiridhia Muswada huo utakuwa sheria.
Muswada huo unaolenga kufanyia marekebisho sheria Ishirini na Tatu ili kuondoa upungufu uliobainika wakati wa utekelezaji wa Sheria hizo umesomwa tarehe 31 Oktoba, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.
Source :
MoCLA | Bunge laridhia Muswada wa Marekebisho ya Sheria
The Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2023 is a Tanzanian law that amends various laws relating to the legal sector. The Act was enacted on August 16, 2023 and has not yet been commenced.
The Act amends a number of laws, including the Advocates Act, the Legal Aid Services Act, and the Business Registration Act. The amendments are intended to improve the efficiency and effectiveness of the legal sector in Tanzania.
Some of the key amendments made by the Act include:
- Amending the Advocates Act to make it easier for foreign lawyers to practice law in Tanzania
- Amending the Legal Aid Services Act to expand the scope of legal aid services available to Tanzanians
- Amending the Business Registration Act to make it easier for businesses to register and operate in Tanzania
The Act is expected to have a significant impact on the legal sector in Tanzania. It is hoped that the amendments will make the legal system more accessible and affordable for Tanzanians.
Here are some of the potential benefits of the Act:
- Increased access to justice for Tanzanians
- Improved efficiency of the legal system
- Reduced costs of legal services
- Enhanced investor confidence in Tanzania
The Act is also expected to have some potential challenges. These include:
- The need to train lawyers and legal aid providers on the new amendments
- The need to increase funding for legal aid services
- The need to ensure that the amendments are implemented effectively
Overall, the Legal Sector Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2023 is a positive development for the legal sector in Tanzania. The Act is expected to improve the efficiency and effectiveness of the legal system, and make it more accessible and affordable for Tanzanians. However, there are some potential challenges that will need to be addressed in order to ensure that the Act is implemented effectively.
MORE INFO :
BUNGENI 31 OKTOBA 2023
Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (Mb.),
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
31 Oktoba, 2023
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, naafiki.
(Hoja ilitolewa iamuliwe)
SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ahsante sana. Hoja
imeungwa mkono. Tunaendelea na utaratibu wetu. Namwita sasa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria. Wasomaji inabidi mkae upande wangu wa huku kulia, ikiwa
mmechaguliwa kusoma na wale wengine upande wa kushoto ili
tuwe tunakomboa wakati. (Makofi)
Kwa niaba ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa
Florent Laurent Kyombo.
MHE. FLORENT L. KYOMBO – MAKAMU MWENYEKITI KAMATI YA
KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa
Spika, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria, naomba kuwasilisha maoni na
ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria, kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali (Na. 4) ya mwaka 2023 (The Written Laws Miscellaneous
Amendments (No. 4) Bill, 2023).
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(5) ya Kanuni
ya Kudumu ya Bunge, Toleo la Februari, 2023, naomba kuwasilisha
maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali (Na. 4) ya mwaka 2023. Kwa kuzingatia masharti ya
Kanuni ya 93(2) ya Kanuni ya Kudumu ya Bunge, Muswada huu
ulisomwa Bungeni kwa Mara ya Kwanza katika Mkutano wa Kumi
Page 166
Eliezer Mbuki Feleshi (Mb) Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu
maudhui ya Muswada huu. Baada ya Kamati kupatiwa maelezo
ya Serikali, Wajumbe walipata fursa ya kuuliza maswali, na kupata
maelezo ya ufafanuzi katika ibara mbalimbali za Muswada.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge Kamati ilifanya Mkutano wa Kusikiliza Maoni ya
Wadau (Public Hearing) tarehe 19 Oktoba, 2023 ili kupokea maoni
yao kuhusu Muswada huu. Aidha, Kamati ilipokea maoni kwa njia
ya mtandao kutoka kwa watu na makundi mbalimbali ya wadau
ambao hawakuweza kufika mbele ya Kamati kuwasilisha maoni
yao.
Mheshimiwa Spika, nawashukuru wadau wote waliotoa maoni yao
ili kuuboresha Muswada huu na nichukue fursa hii kuwatambua
kama ifuatavyo: -
1. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS);
2. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC); pamoja na
3. Wadau binafsi kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mheshimiwa Spika, baada ya hatua hiyo, Wajumbe wa Kamati
walipata fursa tena ya kujadili maudhui ya Muswada kwa
kuzingatia maelezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa
kuzingatia maoni ya wadau. Mnamo tarehe 23 Oktoba, 2023
Kamati ilikutana tena na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye
alijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati kuhusu
ibara mbalimbali za Muswada.
Mheshimiwa Spika, baada ya hatua hiyo, nilizingatia masharti ya
Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge na kukujulisha rasmi
kwamba Kamati imekamilisha uchambuzi wa Muswada ili ujadiliwe
Bungeni.
2.0 UCHAMBUZI WA MUSWADA
2.1 Utangulizi
Mheshimiwa Spika, kamati ilichambua Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na.4 wa Mwaka 2023 [The
Page 176
Mheshimiwa Spika, Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mhe.
Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.
Pauline Philipo Gekul (Mb) Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Mhe. Eliezer Mbuki Feleshi Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Mwandishi Mkuu wa Sheria wa Serikali Ndg. Onorius Njole, pamoja
na watendaji wote wa Serikali kwa ushirikiano wao wa dhati katika
kuyafanyia kazi maoni na mapendekezo ya Kamati.
Mheshimiwa Spika, nawashukuru Watumishi wote wa Ofisi ya
Bunge chini ya uongozi thabiti wa Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa
J. Mwihambi, ndc na kwa upekee Sekretarieti ya Kamati kwa
uratibu wa shughuli za Kamati hadi kukamilika kwa taarifa hii.
4.2 Msimamo wa Kamati Kuhusu Hoja
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, Kamati inalishauri
Bunge lako tukufu kuujadili, kuukubali na kuupitisha Muswada huu
pamoja na Jedwali la Marekebisho kama lilivyowasilishwa na mtoa
hoja.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja.
Mhe. Florent Laurent Kyombo (Mb)
M/MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA
BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA
31 Oktoba, 2023
SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge, ahsante sana
Makamu Mwenyekiti. Nimuite sasa Mheshimiwa Waziri wa Katiba
na Sheria, Mheshimiwa Balozi, Dkt. Pindi Chana, aje awasilishe hoja
yake. (Makofi)
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa
ni mara yangu ya kwanza kusimama hapa kama Waziri wa
masuala ya katiba na sheria, nitakuwa mchoyo wa fadhila ikiwa
sitatumia fursa hii leo kwa mara ya kwanza nikiwa kama Waziri wa
Katiba na Sheria, nisipomshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kwa
Page 184
kuendelea kuniamini na kuniteua tena kuwa Waziri wa Katiba na
Sheria. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais,
kwa kuridhia kutoa fedha za kuwezesha Mkutano wa 77 wa Tume
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, unaoendelea jijini Arusha.
Matokeo ya mkutano huu yamezidi kuing’arisha Tanzania kuwa
kinara wa ulinzi na haki za binadamu duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kipekee nichukue fursa hii kukupongeza
wewe kwa kupata ushindi wa kishindo, uliyokufanya kuwa Rais wa
31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU). Nampongeza pia
Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Muswada huu unakusudia kufanya
marekebisho katika sheria mbalimbali za sekta ya sheria ili kuondoa
mapungufu yaliyobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo.
Muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali za sekta ya sheria
wa mwaka 2023 kama ulivyowasilisha, unapendekeza
marekebisho katika sheria zifuatazo. Zimeelezwa hapo kuanzia
ukurasa wa pili hadi ukurasa wa nne, naomba ziingie kwenye
hansard kama zinavyojieleza namba moja hadi 23.
Mheshimiwa Spika, Muswada huu umegawanyika katika
sehemu 24, ambapo sehemu ya kwanza inahusu masharti ya
utangulizi, yanayojumuisha jina la Muswada na namna ambavyo
sheria mbalimbali zinapendekezwa kurekebishwa na Muswada
huu. Sehemu ya pili ya Muswada, inapendekeza kufanya
marekebisho katika Sheria ya Mawakili sura ya 341, ambapo
kifungu cha 4(a) kinapendekeza kurekebisha ili kuondoa cheo cha
Wakili wa Serikali Mfawidhi, State Attorney in charge, na badala
yake kuweka cheo cha Wakili wa Serikali wa Mkoa (regional State
Attorney).
Mheshimiwa Spika, madhumuni ya marekebisho haya ni
kumfanya Wakili wa Serikali wa Mkoa, kuwa muwakilishi wa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika kamati ya mawakili ya Mkoa.
Pia kuendana na muundo wa sasa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
Page 185
wa Serikali. Aidha Muswada unapendekeza kufanya marekebisho
katika kifungu cha 8(1)(e) ili kuongeza wigo wa vyuo na kuweka
sharti la lazima kupita katika shule ya sheria kwa vitendo. Lengo ni
kuimarisha mfumo wa udhibiti wa ubora wa Mawakili kwa kuwa na
mafunzo yanayofanana kwa wote.
Mheshimiwa Spika, vifungu vya 41 na 42 vinapendekezwa
kurekebishwa ili kuongeza adhabu kwa watu ambao siyo Mawakili
wanaofanya kazi za Mawakili. Lengo la marekebisho haya
yanayopendekezwa ni kuzuia utendaji wa makosa ambayo
huathiri utaratibu wa upatikanaji wa haki hapa nchini.
Mheshimiwa Spika, sehemu ya tatu ya Muswada
inapendekeza kurekebisha sheria ya mamlaka ya rufaa sura ya 141
ambapo kifungu cha 4(e) kinapendekezwa kuongezwa ili kuweka
zuio kwa mahakama ya rufani kusikiliza maombi ya mapitio au
uwamuzi wa muda isipokuwa kama maombi hayo yanaradhimu
shauri la msingi.
Mheshimiwa Spika, vilevile kifungu cha 5 kinapendekezwa
kurekebishwa ili kuboresha masharti ya kukata rufaa katika
mashauri ya madai. Msingi wa marekebisho haya ni kuweka
utaratibu utakaosaidia umalizaji wa mashauri ya madai kwa
wakati.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya nne ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya usuruhishi,
sura ya 15 ambapo kifungu cha 82(3)(b) kinapendekezwa
kurekebishwa ili kuondoa mamlaka ya kusajili wasuruhishi kutoka
kituo cha usuruhishi, kwa kuwa wasuruhishi husajiliwa na Msajili chini
ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai, sura ya 33. Lengo
la marekebisho haya ni kuowanisha masharti ya usajili wa
wasuruhishi katika sheria hizo mbili.
Mheshimiwa Spika, sehemu ya tano ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora, sura ya 391, ambapo kifungu cha 6
kinapendekezwa kurekebishwa ili kufuta maneno Administrative
Justice na badala yake kuweka maneno good Governance.
Page 186
Lengo la marekebisho haya ni kutumia maneno yanayoakisi
majukumu ya Tume kama yalivyoainishwa katika Katiba ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, aya ya
kwanza, inayopendekezwa kufutwa na kuandikwa upya. Lengo ni
kuiacha tume na majukumu yake ya msingi ya uchaguzi na
masuala ya kuendesha mashauri ya kisheria yabaki katika taasisi
husika.
Mheshimiwa Spika, aidha, kifungu cha 11 kinapendekezwa
kufanyiwa marekebisho ili kuanzisha eneo na cheo cha Naibu
Makatibu wa Tume. Lengo la marekebisho haya ni kuboresha
utekelezaji wa majukumu ya tume. Vilevile kifungu cha 12
kinapendekezwa kurekebishwa ili kuweka sharti kwa Naibu
Makatibu wa Tume kuapa mbele ya Mheshimiwa Rais, kabla ya
kuanza kutekeleza majukumu yao.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya sita ya Muswada
inapendekeza kufanya marekebisho katika sheria…
SPIKA: Mheshimiwa Waziri, subiri kidogo. Ni kitu gani hicho
kinasikika huko? Waheshimiwa Wabunge, tafadhalini sana.
Mheshimiwa Waziri.
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, sehemu ya
sita ya Muswada inapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria
ya mwenendo wa mashauri ya jinai, sura ya 20 kwa kuongeza
kifungu cha 4(e) ili kuowanisha madhumuni ya msingi (overriding
objectives) katika sheria. Lengo la marekebisho haya ni kuzitaka
mahakama kutenda haki kwa wakati na kuangalia haki msingi
katika kusikiliza mashauri ya jinai bila kufungwa na kiasi kikubwa cha
masharti ya kiufundi.
Mheshimiwa Spika, aidha vifungu vya 202, 204, 205(a) na
205(b) vinapendekeza kurekebishwa kwa kuahinisha namna
ambavyo wataalam kama vile wataalam wa mripuko na
wataalam wa uchunguzi wa makosa ya mtandao wanaweza
kuteuliwa na Mkurugenzi wa mashitaka. Madhumuni ya
marekebisho haya ni kubadilisha nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa
Page 187