Uhitaji wa wananchi? wananchi wapi hao? wa CCM au wa Tanzania? Brother anaeogopa wagombea huru ni CCM sio wananchi wa Tanzania.
Kati ya maamuzi tata ya mahakama ya rufani ya Tanzania na yatabaki kwenye historia ni pale ilipokwepa wajibu wake wa kuhukumu kesi na kuirudisha iamuliwe na wanasiasa, huu uamuzi hadi leo sijawahi kuuelewa kabisa.
Na mara papu aliyekuwa jaji mkuu wetu wa mahakama ya rufani na mwenyekiti wa jopo la majaji walio amua kesi hii ya kupokwa kwa haki zetu za kiraia na kundi dogo tu la wana siasa, haaa!! kumbe nae ni mwanasiasa! tukashuhudia na yeye kachakua fomu kugombea urais,mama yangu toka siku hiyo sina ninaye mwamini iwe hapa,pale ,huko yaani popote pale katika mihimili yote ya utawala katika nchi hii.