Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 17,080
- 33,076
Unajua ule moto Prof Muhongo alitakiwa awe pale alikimbia mimi naendelea kumuonea Iman alipelekwa kwenye kisu asichokijua wadogo wana maswali ya balaa mno mno ni kama Mwanasheria mmoja bwana mdogo wa Kenya ana balaa sana sio wa kuingia anga zake...Nimeicheki asee. Dah jamaa alikuwa anatetemeka balaa mikono inasheki. Yani hat msukuma na kibajaji wanaconfident kumshinda.
Mkuu nna uhakika aliekua upande wa kampuni against Prof ni mwanasheria anazo ABC za geology lakn ni mbobezi wa Sheria za madini, jiulize Tanzania kama taifa tuna wanasheria waliobobea kwenye madini? Kwanini waliosaini mkataba (wanasheria) wamefyata mikia?Unajua ule moto Prof Muhongo alitakiwa awe pale alikimbia mimi naendelea kumuonea Iman alipelekwa kwenye kisu asichokijua wadogo wana maswali ya balaa mno mno ni kama Mwanasheria mmoja bwana mdogo wa Kenya ana balaa sana sio wa kuingia anga zake...
Hivi hamuoni kama taifa Lina shida kubwa sana wakuu?Huyo ndio think tank wa serikali,yupo hapo hajui chochote yuko kama lusinde
huyu kijana anaujua upumbavu wote wa ccm, ndiyo sababu amespcialised kuiadhibu TZYani jamaa mdoga anavomuendesha mzee kilaza mruma alafu anaulizwa ndio unavowafundisha hapo UDSM.
Inaleta picha gani kwamba maprofa vilaza na phd za mchongo walizonazo hapa tz.
Aisee ccm mnawakati mgumu sana sema mnatumia nguvu kubaki madarakani.
Hakuna kesi tulizoshinda.View attachment 2698364
View attachment 2698365
Mkuu, geologist anaenda kuhojiwa na mwanasheria unategemea nini hapo?Hiyo nafasi ilikuwa ya Professor Kabudi au hata mwanasheria mwingine Nguli.
sasa Sijui ilikuwaje akaenda Geologist?
Kimsingi mtaalam sio kazi yake kujibu masuala ya Kisera. Ningekuwa ni mimi wala singekubali kuhojiwa.....
Tuwekee hiyo clip, plsNdugu Watanzania!
Video hii ni sehemu ya Kesi ya Madini kati ya Tanzania na Kampuni ya Winshear Gold Corp. Mkataba wa Madini uliosainiwa mwaka 2014 na Waziri wa Nishati na Madini enzi hizo ndio unaobishaniwa hapa. Katika safu ya utetezi, Tanzania ilimpeleka Prof. Abdulkarim Mruma kuwa sehemu ya utetezi. Pamoja na umahiri na usomi wake, Prof. Mruma, hajafua dafu kwani vifungu vya mkataba vinaiumbua Serikali ya Tanzania.
... Prof. Mruma alienda kama shahidi na sio wakili. Ikumbukwe akiwa CEO wa GST, documents za mkataba zilipitia kwenye desk lake kama hatua ya kukamilisha process.Hiyo nafasi ilikuwa ya Professor Kabudi au hata mwanasheria mwingine Nguli.
sasa Sijui ilikuwaje akaenda Geologist?
Kimsingi mtaalam sio kazi yake kujibu masuala ya Kisera. Ningekuwa ni mimi wala singekubali kuhojiwa.....
Akili zingine bhana wewe utakuwa mdogo wake Mruma, sasa geologist kwenye hizi office ni wanini?Hivi hamuoni kama taifa Lina shida kubwa sana wakuu?
Tukae hapohapo kwenye mkataba huo
Point yangu ya msingi ni kuwa mikataba wanasaini watu wa madili mjini mambo yakibuma wanaanza kutafutwa wataalamu wa kada husika, it's a shame guys.
- Je, prof. Mruma alikuwepo kwenye kudraft hiyo contract?
- Je, ni nan alieshiriki kwenye hiyo process?
- Kama hakuwepo, team iliyodraft mkataba imeenda wapi mpka Prof. Aingie kwenye game mda huo?
Mfano: Office za umma zifuatazo zilitakiwa angalau ziwe na geologists kama list zao za wafanyakazi;
-CAG office
-Attorney general office
-Mkemia mkuu office
-TBS
-NEMC
-TBA
-Ikulu
-Mahakama
-TANESCO
- Bunge
Kwenye hizo office ukitoa TANESCO ni office moja tu imeajiri geologists mwaka huu, CAG office.
So guys, haya ni matokeo ya taifa kuongozwa na siasa plus watu wa dili kuliko weledi.
Umeandika kweli tupu.Hii nchi inefeli kwasababu watu wengi walioshika nyadhifa za juu akili zao ni kama hizi, CCM imejaa maboga matupu yasiyofaa kupeleka popote, mtu kama Professor Mkumbo utasema kuna akili mule?
Wale waliokua hawaoni tatizo la kuongozwa na mtu asiyekuwa na elimu "halisi" ya kutosha, nadhani watakuwa wamejifunza hapa. Kama huyu ndiye alieonekana kuwa mtaalamu mbele ya SHH na jopo lake, yeye SHH yupoje? Hako kalikompiga KO Prof Mruma ni chini ya miaka 30.
Magufuli aligundua kuwa CCM imejaa maboga yasiyoweza kumsaidia lolote ndiomaana alianza kuiba vijana wenye elimu nje ya CCM na kuwaingiza kwenye mfumo.
Nchi ya kipumbavu kabisa hii.
BORA HATA HUYU ITAKUWA KITUKO CHA MIAKA ENDAPO CHADEMA WATAKUJA KUSHIKA MADARAKA HALAFU WATUME WATAALAMU WAO KINA HECHE HUKOI HATA KUONGEA HAWATAWEZA KELELE ZAO ZIKO HAPAHAPA NCHINI TU NISIFURI KABISA AU UNAMTUMA YULE DOGO WA VIJANA MWENEYEKITI YAANI NI UOZO MTUPUProfesa Mruma amepata pigo kubwa sana kwa umri wake; waliomtuma huko Duniani wamedhamiria adhalilishwe na lengo limetimia . Anaulizwa kwa fedheha " haya ndiyo unawafundisha wanafunzi wako wa UDSM?
Muuliza swali ni mtoto wake wa kumzaa. Kwanini tumeruhusu wasiojiweza watusimamie?
---
Winshear Gold Corp. Vs. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25).
Kesi hii ipo chini ya Rais Gabrielle Kaufmann Hohrer kutoka Uswizi.
Mashahidi wetu huko ni Prof. Mruma na Mwanasheria wa Serikali bwana Igenge.
---
Video 1: Profesa Mruma akihojiwa
View attachment 2698386
Video 2: Mkurugenzi wa Huduma za Sheria(Wizara ya Madini) Edwin Igenge akihojiwa na Robert Denison
View attachment 2698385
---
WASIFU WA PROFESA MRUMA
Dkt. Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia. Profesa Mruma kwa sasa anahudumu kama Kamishna wa Tume ya Madini nchini Tanzania.
Mwaka 2017 Hayati Rais Magufuli alimteua Prof. Abdulkarim Mruma kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuhifadhi Mafuta (TIPER)
Profesa Mruma alijizolea umaarufu 24 Mei, 2017 baada ya kuongoza Kamati maalum iliyondwa na Rais Magufuli kuchunguza mchanga ulio katika makontena yenye mchanga wa madini (makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania
-
Dkt. Abdulkarim Hamisi Mruma Ph.D. M.Sc. B.Sc. ni Mkurugenzi wa Kujitegemea wa Tanzania Royalty Exploration Corporationration. Dkt Mruma ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako kwa sasa ni Profesa wa Jiolojia.
Masomo yake ya Uzamili yalijumuisha tafiti katika vyuo vikuu na taasisi za Serikali nchini Ujerumani, Ubelgiji, Zimbabwe na Ufini.
Ameandika ripoti za kiufundi kuhusu mada mbalimbali za kijiolojia na kuchangia katika majarida kadhaa ya kiufundi na yasiyo ya kiufundi juu ya anuwai ya masomo ya Jiolojia.
Orodha ya machapisho hayo ni pamoja na Jarida la UNESCO la Sayansi ya Ardhi ya Afrika na Jarida la Tanzania la Sayansi ya Dunia.
Mbali na majukumu yake ya kitaaluma, Dk. Mruma ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania nafasi ambayo ameitumikia tangu Oktoba 2004.
Pia anahudumu kama Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Sayansi za Ardhi cha Williamson Diamonds Limited cha Chuo Kikuu cha Dodoma na Shirika la Madini la Taifa la Tanzania mshirika wa ubia wa Kampuni ya Uboreshaji wa Mradi wa Buckreef Gold Mine.
Pro. Mruma hakushindwa kunibu ila siku hiyo aliamka vibaya au tuseme alikuwa anaumwa.MKATABA MBOVU WAITIA KITANZI TANZANIA
Ndugu Watanzania!
Video hii ni sehemu ya Kesi ya Madini kati ya Tanzania na Kampuni ya Winshear Gold Corp. Mkataba wa Madini uliosainiwa mwaka 2014 na Waziri wa Nishati na Madini enzi hizo ndio unaobishaniwa hapa. Katika safu ya utetezi, Tanzania ilimpeleka Prof. Abdulkarim Mruma kuwa sehemu ya utetezi. Pamoja na umahiri na usomi wake, Prof. Mruma, hajafua dafu kwani vifungu vya mkataba vinaiumbua Serikali ya Tanzania.
Wakili msomi upande wa Winshear Gold Corp anamhoji Prof. Mruma kuwa inawezekanaje huo mchakato uliopita mikono ya wengi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Sheria, Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania na wasomi wabobezi wa madini kama Prof. Mruma hawakuyabaini hayo mapungufu ndani ya mkataba? Swali hilo alishindwa kujibu Prof. Mruma, hivyo akaishia 'kulenga shabaha mwituni'!
Tunachotaka kusema ni kuwa, kama serikali ikisaini mkataba mbovu, huko mbele ya safari hata ikipeleka wasomi 100 wenye uwezo kama wa Prof. PL Lumumba, Mhe. Tundu Lissu, Peter Kibatara, Dkt. Masumbuko Lamwai (RIP), Prof. Jwani Mwaikusa (RIP), Dkt. Sengondo Mvungi (RIP), nk itapigwa tu.
Tunapohoji na kuupinga Mkataba wa Bandari muwe mnatuelewa. Waambieni Dkt. Tulia, Prof. Mbarawa, Maulidi Kitenge, Cd. Chongolo, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waipitie vizuri video hii. Lakini tutamuomba Gerson Msigwa amuonyeshe Mhe. Rais Samia clip hii. Lakini majibu ya Prof. Mruma yanaonyesha wahusika walipitia mchakato wote. Swali linalojitokeza kwetu sote ni kwa nini serikali iliusaini? Kama ni hivyo, ni kwa nini Serikali iliuvunja baadaye?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 24 Julai 2023; 15:40 pm.
Ishu ni usomi au ishu ni lugha.Kwani inakatazwa kuhojiwa kwa lugha yako ya kiswahili?