DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mahakama ya Mazingira na Ardhi nchini Kenya imezuia kampuni ya Taifa Gas kuendelea na ujenzi wa kiwanda cha gesi ya LPG chenye thamani ya Shilingi bilioni 16 katika eneo la Dongo Kundu, Mombasa.
Uamuzi huo umetokana na hofu ya uharibifu wa mazingira ya pwani, kufuatia ombi la wakazi wawili wa Likoni waliodai kuwa mradi huo unahatarisha viumbe wa baharini, miti asilia, na maeneo ya uvuvi.
Taifa Gas, inayomilikiwa na bilionea wa Tanzania Rostam Aziz, ilikuwa imewasilisha mradi huo kama suluhisho la kupunguza gharama za gesi na kuimarisha sekta ya nishati nchini Kenya.
Mahakama imeamuru kusitishwa kwa shughuli zote za ujenzi hadi uchunguzi zaidi ufanyike, jambo linaloibua mjadala mpana kuhusu uwiano kati ya maendeleo ya viwanda na uhifadhi wa mazingira.