Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

Mnaodhani kuwa mkiwa madarakani basi mnaweza kufanya kila mnalolitaka mmekosea sana kwani sasa ni rasmi kwamba Mitandao ya Kijamii ndiyo kimbilio pekee la upatikanaji wa Haki hapa duniani ambapo nguvu ya Kimaoni ya Wachangiaji wake inaweza hata kumfanya Mtawala aliyepo madarakani akimbie kama siyo kuwa mpole.

Katika kile ambacho hakikutegemewa na wengi muda mfupi tu uliopita Mahakama ya Kijeshi ya nchini Uganda imefuilia mbali mashtaka yote ambayo yalikuwa yakimkabili Mbunge maarufu na Msanii Robert Kyagulanyi ( Boby Wine ) baada ya kuona kuwa Mashtaka hayo hayakuwa na msingi wowote ( baseless ) hasa Kisheria.

Hivi sasa taratibu mbalimbali zinaendelea ili sasa kumrudisha Msanii huyo jijini Kamplala ili aweze Kuungana na Familia yake. Chezeni na Vitu vyote ila kaeni mbali na Mitandao ya Kijamii na nguvu zake kwani kwa dunia ya sasa Mitandao ya Kijamii inaweza kuleta mabadiliko yoyote na wakati wowote hasa kwa wale Viongozi Wababe, Wabishi na Madikteta waliopo duniani.

Hata hivyo japo tutashangilia kuwa Boby Wine amefutiwa Mashtaka yake ila hapa kuna mchezo umechezwa ili Kuwazuga Watu ambapo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kwamba tayari wameshammaliza Kijasusi Boby Wine kwa kumuwekea Sumu na Kumjeruhi vibaya hivyo wana uhakika kwamba muda wowote anaweza akafa na kuwa ni ushindi mkubwa Kwao hasa ikionekana kwamba huyu Msanii kwa sasa ana mvuto mkubwa kwa Wapiga Kura wengi ambao ni Vijana nchini Uganda na ambaye pia anaonekana atakuja kuwa tishio kwa Rais Museveni kuliko hata yule aliyekuwa Mpinzani wake Mkuu Kiongozi wa FDC Dkt. Kiiza Besyige.

Kwa mateso mabaya na makubwa aliyofanyiwa Boby Wine nina wasiwasi kama ataishi muda mrefu. Kitendo kilichofanywa na Mahakama hiyo ya Kijeshi nchini Uganda ni kutaka tu Kupoza msukumo mkubwa uliopo na Vilio vya Wanaharakati wengi duniani dhidi ya kilichomkuta Msanii huyo ila kwakuwa Kukamatwa Kwake kulihusisha kwa ukaribu sana Idara ya Ujasusi ya Kijeshi ya Uganda ( CMI ) wakishirikiana na wale wa Kikosi Maalum cha SFC kuna uwezekano mkubwa kuwa watakuwa wameshammaliza japo anaweza asidhurike leo au kesho ila hana muda mrefu.
 
Kuna tetesi kwamba jamaa hatoweza kusimamaisha tena, kapewa kubwa kuliko. Huo msamaha ni sehemu ya tu ya mpango wao
 
Hawezi ishi huyo walahi!

Nakubaliana nawe kwa 100% kwamba tayari watakuwa wameshammaliza. Hapa ujuzi wa Kijasusi wa Kirusi utakuwa umetumika mno dhidi ya Msanii Boby Wine. Haiwezekani ghafla tu hivi wajifanye wameona hana makosa wakati ni hao hao ndiyo walimkamata, kumtesea, kumjeruhi na kumuumiza vibaya huku wakisema ana makosa ya kujibu na leo wamegeuka na kudai hana makosa.
 
Akifa kwa sababu yoyote mwili wake utafanyiwa post mortem na ikigundulika kafa kwa sababu zisizo za kawaida Uganda ijiandae kwa vikwazo na hilo bomba la mafuta watalisahau
 
So true!
 
Akifa kwa sababu yoyote mwili wake utafanyiwa post mortem na ikigundulika kafa kwa sababu zisizo za kawaida Uganda ijiandae kwa vikwazo na hilo bomba la mafuta watalisahau
Akafanyie uchunguzi wa afya yake nje na aje aweke ripoti yake wazi kwa wananchi.

Akifa ijulikane kabisa kuwa Kaguta anahusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom