Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

Ndo maana namkubali trump!
Wahuni wote anawanyoosha
 
Kapelekwa mahakama ya kiraia, tazama live hapa



Ameshafikishwa mahakamani, hawezi kusimama mwenyewe hivyo kwa ruhusa maalum ya hakimu amesomewa mashitaka akiwa amekaa.

Amesomewa mashitaka ya uhaini.

Wakili anayemtetea ameomba ahamishiwe kwenye hospitali binafsi apate matibabu, wakili wa Serikali amepinga kwa madai kwamba anaweza kutibiwa na serikali akiwa mahabusu

Hakimu ameruhusu mshtakiwa namba A33 ambaye ni Bobi Wine atibiwe na madaktri binafsi kwa kuwa hali yake ni mbaya na anahitaji matibabu ya haraka

Kesi itapelekwa mahakama kuu yenye uwezo wa kusikiliza kesi hii
 
Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amekamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini.

Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uganda M7 ni moto, Rwanda Kagame ni Moto, na kutoka kwao Jiwe anacopy na kupaste. Rwanda ukimgusa Jiwe wa kule kifo kinakuhusu. Nadhani kwa sasa Rwanda haina chama cha upinzani. Na Uganda sasa Inaelekea huko huko. Jiwe wa kule hataki kusikia kitu upinzani. Huyu wa huku kwetu anaweza kuvunja record za hao wawili. Tunapoelekea itakuwa haramu kusalimiana na mfuasi wa chama cha upinzani. Kwenye chaguzi anaelekea kufaulu maana fomu za wapinzani zitakuwa hazipokelewi hivyo majimbo mengi ccm kitakuwa kinapita bila kipingwa. Na hata zikipokelewa, tayari wakurugenzi wote wameshapewa maelekezo ya kutowatangaza wapinzani pale wanapokuwa wameshinda chaguzi.

Yajayo........... Yanasikitisha
 
Dahh!! Hakuna haja ya uchaguzi, waendelee tu kujichagua na kujitangaza
 
Back
Top Bottom