Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

Mahakama ya Kijeshi yamuondolea Bobi Wine mashitaka! Akamatwa tena sasa kushitakiwa Mahakama ya kiraia

Nilifikiri hayo yapo Tz tu,kumbe Afrika yote Uhuru wa kidemokrasia,we mungu tuokoe.
 
Hapa ndipo najiuliza umoja wa afrika mashariki nini au umoja wa waafrika ina msaada gani kwa unyanyasaji wa mwafrika mwenzao!!, au umoja wa afrika ni kwenye biashara tu?, kwanini Marekani ndio iongelee mabaya yanayofanyika Uganda na wakati umoja wa kikanda na Africa hawawezi kukemea???, huwa nawashangaa wanaosema eti matatizo ya waafrika yatatatuliwa na waafrika wenyewe kwa styl hii tutatokwa mapovu
 
Uganda M7 ni moto, Rwanda Kagame ni Moto, na kutoka kwao Jiwe anacopy na kupaste. Rwanda ukimgusa Jiwe wa kule kifo kinakuhusu. Nadhani kwa sasa Rwanda haina chama cha upinzani. Na Uganda sasa Inaelekea huko huko. Jiwe wa kule hataki kusikia kitu upinzani. Huyu wa huku kwetu anaweza kuvunja record za hao wawili. Tunapoelekea itakuwa haramu kusalimiana na mfuasi wa chama cha upinzani. Kwenye chaguzi anaelekea kufaulu maana fomu za wapinzani zitakuwa hazipokelewi hivyo majimbo mengi ccm kitakuwa kinapita bila kipingwa. Na hata zikipokelewa, tayari wakurugenzi wote wameshapewa maelekezo ya kutowatangaza wapinzani pale wanapokuwa wameshinda chaguzi.

Yajayo........... Yanasikitisha
inawezekana kweli watanznia ni waoga,ila hata walio wababe leo walikuwa waoga kama au pengine kuliko sisi,majanga yanapozidi mioyo huota kutu.Ipo siku watu watastaajabu.
 
Miafrika tumeumbwa mijitu ya ajabu ajabu sana.

Hapo M7 amemuachia kwakua anaogopa kukosa misaada.
Unatesa watu kisa madaraka, alafu M7 ndiye role model wa jamaa yetu.

Mungu atunusuru Watanzania yasijirudie ya Lissu

Sent using Jamii Forums mobile app
HAHAHHAAAHAA nacheka sio kwasababu ni mazuri ila ni maajabu ya dunia
 
Bobi Wine ameachiwa huru leo na inadaiwa ni kutokana na shinikizo toka Ubalozi wa Marekani nchini Uganda,

Hana kesi ya kujibu.

Chanzo: City Radio Uganda

=======

Taarifa za hivi punde kutoka Uganda ni kwamba mahakama ya jeshi imemuondolea mashtaka mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi.

Inaarifiwa kwamba mahakama hiyo ya jeshi inataka badala yake inataka kumkabidhi mbunge huyo kwa mahakama ya kiraia ajibu mashtaka ya uhaini pamojana wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bobi Wine leo alitarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kimataifa la kutaka Bobi Wine aachiwe huru.
=========

UPDATE
Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Chanzo: BBC
Bob Wine Kaachiwa kwa Dhamana....
 

Attachments

  • Screenshot_2018-08-27-13-49-01.png
    Screenshot_2018-08-27-13-49-01.png
    107.9 KB · Views: 44
Unajua uoga wetu ndio umaskini wetu,lakini Bobiwine kaonesha haki inavyotafutwa,kufa kila mtu atakufa hakuna atakaye ishi milele yuko wapi MOBUTU.
 
Back
Top Bottom