Uganda M7 ni moto, Rwanda Kagame ni Moto, na kutoka kwao Jiwe anacopy na kupaste. Rwanda ukimgusa Jiwe wa kule kifo kinakuhusu. Nadhani kwa sasa Rwanda haina chama cha upinzani. Na Uganda sasa Inaelekea huko huko. Jiwe wa kule hataki kusikia kitu upinzani. Huyu wa huku kwetu anaweza kuvunja record za hao wawili. Tunapoelekea itakuwa haramu kusalimiana na mfuasi wa chama cha upinzani. Kwenye chaguzi anaelekea kufaulu maana fomu za wapinzani zitakuwa hazipokelewi hivyo majimbo mengi ccm kitakuwa kinapita bila kipingwa. Na hata zikipokelewa, tayari wakurugenzi wote wameshapewa maelekezo ya kutowatangaza wapinzani pale wanapokuwa wameshinda chaguzi.
Yajayo........... Yanasikitisha