Mahakama ya kijeshi yatoa hati kiongozi wa AFC/M23 Corneille Nangaa akamatwe

Mahakama ya kijeshi yatoa hati kiongozi wa AFC/M23 Corneille Nangaa akamatwe

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama ya Kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa umoja wa makundi ya waasi nchini humo ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23), Corneille Nangaa.

Shirika la Habari la AP limeripoti leo Februari 7, 2025, kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo imetoa hati Nangaa akamatwe akituhumiwa kuhusika katika kile ilichotaja kuwa ni uasi na uhalifu wa kivita dhidi ya raia nchini humo.

1738924408697.png
Televisheni ya Taifa ya DRC nayo iliripoti kuwa hati ya kukamatwa kwa Nangaa imetolewa Jumanne Februari 4, 2025, baada ya kuhusika katika mauaji ya maelfu ya raia katika mapigano yaliyoibuliwa na wapiganaji wake katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo.

Mahakama hiyo katika hati yake imesema kutekeleza mauaji ya raia katika mapigano hayo ni kinyume cha sheria za nchi na sheria za kimataifa.

Imeamuru Nangaa akamatwe akiwa mahali popote atakapokutwa duniani na kufikishwa katika Mahakama ya kijeshi nchini DRC.

Soma, Pia: Maelfu ya wakazi wa Goma wakusanyika uwanjani kusikiliza Hotuba ya Corneille Nangaa kiongozi wa AFC/M23

==

A military court in the Democratic Republic of Congo has issued an international arrest warrant for the leader of the Congo River Alliance, which includes the M23, for war crimes and treason.

State media reported on Thursday that the warrant was issued on Tuesday against Corneille Nangaa for massacres it claimed he committed in eastern DRC’s North Kivu and, more recently, in South Kivu regions – constituting a crime under Congolese legislation, as well as international law.

The court has ordered Nangaa to be arrested wherever he may be found and brought to Congolese territory.

Violence erupted in Goma, a city of two million people in eastern DRC, two weeks ago when the M23 fighters launched a major offensive against government forces.

On Wednesday, the UN Office for the Coordination of Humanitarian Affairs estimated that at least 2,800 people died in Goma due to the violence.

Thousands of people have also been displaced, with many fleeing to neighbouring Rwanda, including staff from international organisations such as the UN and the World Bank.

Source: aljazeera.com
 
Trump kawapiga kibano "sanction" ICC

Dunia inaenda haraka Sana!
 
Sasa kama wameshamhukumu kifo hiyo hati ya makosa nyingine ya kazi Gani. Mahakama ya kijeshi mwaka Jana ilimhukumu kifo Cornell Nanga bila yeye kuwepo mahakamani. Wamsake tu wamle kichwa if possible
 
Back
Top Bottom