Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,411
- 3,712
Majaji wa mahakama ya kimataifa (ICC),imetoa hati ya kukamatwa popote atakapopatikana rais wa urusi Vladimir Putin.
=====
Katika uamuzi wake, ICC imemtuhumu Rais wa Russia kuhusika na uhalifu wa kivita kutokana na kufanya uvamizi na kutwaa ardhi Nchini Ukraine ingawa Moscow imesema hatua hiyo haina maana yoyote.
Pia, Hati ya Mahakama ya ICC imeeleza kuwa Rais Vladimir Putin aliagiza mashambulizi yaliyosababisha Watoto kuhamishwa kinyume cha Sheria pamoja na uhamisho usio halali wa Raia kutoka eneo la Ukraine na kuingia Nchini Urusi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova amesema "Maamuzi ya ICC hayana maana kwasababu Urusi haiko kwenye Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, hivyo haiwajibiki chini yake."