Mahakama ya Kimataifa ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Rais Vladmir Putin wa Urusi

Hahaha urusi kashaanza mchakato wa kujitoa kwenye hiyo mahakama uchwara.
Sio keshaanza, ila hajawahi kujiunganisha nayo,, hiyo ni mahakama kwa ajili ya maombaomba,, Russia sio matonya,,! Ninachokiona hapo ni habari-,: - TEMA MATE TUMCHAPE,,! Zele anafalijiwa
 

ICC ilisaidia Kenya pakubwa, ile tu kuwaburuza mahakamani wakaishia kujitetea na kutia huruma ilisaidia maana baada ya hapo hatujawa na mibabe wa fujo, kabla ya hapo wanasiasa walikua wanahubiri fujo na machafuko, ila chaguzi zote baada ya mtanange wa ICC, wanasiasa wamekua makini sana.
Huyo "mungu" mtu wenu aendelee kumwaga damu ya wananchi wa Ukraine, ila siku zake zinakaribia, wanajeshi wake wanaendelea kuisha kama senene, ataliwa tu.
 
1. Hii ina maana gani?: Ina maana kwamba Putin anahitajika ashtakiwe kwa uhalifu wa kivita. 2. Atakamatwa na nani: Anaweza kukamatwa ndani ya nchi yake na kupelekwa huko Uholanzi ili wamtie adabu, au akamwatwe nje ya nchi yake pale atakapotembelea mojawapo ya nchi 123 wanachama wa ICC. Hili litamfanya Putin akose uhuru hapa duniani na kuishi kama digidigi anayewindwa. Maana kila akitaka kusafiri nje ya nchi lazima akumbuke na kujihoji je huyu si mwanachama wa ICC?.
 
Hakuna dunia hii anayeweza Kumkamata Putin usipokuwa Mungu Tu.
Umenikumbusha kauli ya MTEMI CHENGE,, "wakimkamata yupo ila wa kuifunga simuoni",,

Kwa PUTIN, Wa kutoa amri yupo, ila wa kumkamata PUTIN hatumuoni,,!

Wamemshindwa Boss wa Wagner, kwa PUTIN wanaanzia wapi,,!?
Wapigane vita waache vichekesho,,
 

Hujajibu swali!!! Kuna ushahidi wa kutosha kwamba ni kweli walitenda war crimes - sasa mbona hawakufungwa, badala yake unatuletea adithi za kubuni tu - kujustfy war crimes za Wakenya wenzako huku ikijitia kumkalia kooni Putin kwa madai ya kipuuzi tu.

Hivi hawa ICC wanawezaje kumsakama Putin eti kwa kuwahamisha watoto na watu wazima ambao ni ethinic Russian kutoka kusini mashariki mwa Ukraine kwenda Urusi kwenye usalama - kwani nani ambaye hajui jinsi jeshi la Zelensky lilivyo kuwa linapiga mizinga kusini mashariki mwa Ukraine na kuwauua zaidi ya ethinic Russian zaidi ya 14,000 tangu 2015 - mabeberu especially USA pamoja na media zao mliwahi kuzisikia zinalalamikia ukatiri huo wa kuwaua watoto wadogo kwa mizinga na rockets mashuleni na mahospitali - hakuna. Cha ajabu wanafiki hawa hivi sasa ndio wanajitia kutaka kumshtaki Putin kwa kuokoa Warusi wenzake wanao ishi kusini mashariki mwa Ukraine kwa kuwahamishia Urusi kwenye usalama zaidi, akili za viongozi wa magharibi zikoje lakini, ukiangalia kijuu juu unaweza kufikiri wana uchungu wa kweli kuhusu kuhamishwa kwa watoto lakini deep down lengo lao ni kutaka kumfanya Putin hasisafiri nje ya Taifa lake - hata wafanye mbinugani za kutaka kumu contain Pitin ukweli ni kwamba hawamuezi unless wakitaka kuanzisha WW3 - Urusi haiwezi kukubali ujinga huu hata siku moja.
 
Huu uandishi wa Mathanzua kabisa, bila shaka hii ni ID yake nyingine.
 
Waliotenda Bush, Blair, Obama etc huko Afghanistan, Libya etc pia ni uhalifu wa kivita. Kwanini nao wasikamatwe? Unafiki wa NATO
 
Sawa kabisa. Kongole mkuu
 
Famous β€œBlack Hawk Down” incidence in Mogadishu (Somalia), more than 6 thousand civilians including women and children were killed in a single day attack by US soldiers. No investigation for justice has been conducted
 
Raisi yupi alikuwa madarakani akapelekwa
 
Tusubiri tuone mwisho wa hii sinema.

"Sisemi mrusi anaweza mpiga Marekani, au Marekani anaweza mpiga Mrusi, nachokataa mimi, ni kusema kuwa Marekani anaweza cheza na Mrusi kama anavyocheza na Libya".

Nimemnukuu MALCOM LUMUMBA naamini niko sawa kimantiki alichokisema.
 
Akili kisoda
 

hawakufungwa maana ushahidi haukupatikana wa kutosha kuwafunga, nilifuatilia sana kesi zao with passion, ila nimekuambia ICC ilitusaidia sana maana chaguzi zote zilizofuata zimekua za amani, mjiandae kwa msiba wa huyo "mungu" mtu wenu, aidha aliwe risasi au aishie ICC.
 
Urusi siyo Libya au Iraq, na hawa majaji sijui wamelipwa sh ngapi na West.Ngoja tusubiri kuona Putin akikamatwa
You never know, Putin sasa ataishi kwa khofu zaidi, nje ya Russia hatajaribu kukanyaga atafia kremlin au ICC watamtia mikononi haijali muda gani itachukua
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Yaani we jamaa. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Husitufanye tuseme maneno mengi, kama kweli ulikuwa unifiatilia kesi hii with passion, sasa kwa kwa nini key witness karibu wote walikufa vifyo vyenye mazingara ya kutatanisha na wengine kutishiwa maisha wakikubali kwenda kutoa ushahidi the Hague dhidi ya Ruto na Kenyatta!!
 
Famous β€œBlack Hawk Down” incidence in Mogadishu (Somalia), more than 6 thousand civilians including women and children were killed in a single day attack by US soldiers. No investigation for justice has been conducted
There you are - what a million dollar question? Sina shaka MK254 atatupatia jibu sahihi ie jibu lenye mshiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…