Mahakama ya Kimataifa ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Rais Vladmir Putin wa Urusi

Tunasubir mwanaume wa kuingia Russia na kumkamata. Kutoa tamko sio shida.
wanafahamu kuwa hawawezi kwenda kumkamatia nyumbani ila watamvizia ugenini[emoji1],
Ila sio rahisi, nadhani sasa wamemchokoza........tusubirie aitishe kikao atoe tamko Kali zaidi
 
Kajambe
 
Ongezea...
Ariel Sharon hakukamatwa
Benjamin Netanyahu hajakamatwa....
Maelekezo ya πŸ‡ΊπŸ‡²
Hawa waliwahi kufunguliwa mashtaka huko ICC ?...au wamewahi kufunguliwa mashtaka na hati ya kuwakamata ikatolewa ?

Au kwanini nchi zilizotendewa uhalifu na hawa jamaa hazijawafungulia kesi huko ICC ?

kwa nini hatuanzi na numerous war crimes commiited by US over the years - waburuzwe mahakamani akina Bill Clinton, Bush Sr kama angekuwa alive, Bush Jr, Johnson, akina Nulad na Seneta McCaine kama angekuwa alive.
 
Warusi wanachokaje vita mzee, vita ndo zimewafanya wawe hapo walipo.. wababe duniani na wanajiweza. Vita, vita
Wachovu tena sana vinginevyo urusi isingesambaratika na kuwa nchi kibao

Ubabe wao mbona walishindwa kuifanya Russia kuwa nchi moja? Ujue hata Ukraine ilikuwa sehemu ya Russia wakawadindia Russia ,Russia akaufyata wakaanzisha taifa lao wakaweka na Raisi wao Zelewisky

Nchi kibao walitwangana nao na wakajitenga na Russia

Putin kuondoka lazima na The Hague kuna.husu kama atabahatika kunudurika bichwa lake kulimbwa risasi
 
Endelea kuota ndoto za kitandani ukifanya masihara utakojoa ukijinyea kwa stress
 
You never know, Putin sasa ataishi kwa khofu zaidi, nje ya Russia hatajaribu kukanyaga atafia kremlin au ICC watamtia mikononi haijali muda gani itachukua
Endelea kuota. Walishindwa kumkamata Albashir na akawa anaenda Nigeria, Chadi na SA pamoja na uwepo wa warrant hiyo ije iwe Mwamba Putin.

Sana Sana kuonyesha wako serious hao westerns wanaweza kuzuia asifanye ziara katika mataifa yao kama sehemu ya Vikwazo lakini siyo kumkamata. Hakuna mwenye uthubutu huo.

Believe me Putin ataongoza hadi kustaafu na baadae kufa, pasipo kuguswa na yeyote ndani na nje ya Russia.
 
Rais gani wewe usikanyaga mataifa zaidi 60 ulimwenguni? warusi wamechoshwa na Putin watampeleka tuu waishi kwenye nchi yao kwa amani waondokani na udikteta
 
wanafahamu kuwa hawawezi kwenda kumkamatia nyumbani ila watamvizia ugenini[emoji1],
Ila sio rahisi, nadhani sasa wamemchokoza........tusubirie aitishe kikao atoe tamko Kali zaidi
Huyu jamaa alishatoa matamko makali mengi e.g. Ole wake nchi/Taifa atakayeingilia vita hii atajibiwa kwa ukali, hii siyo vita ni OP tu ya saa 72.... na hakuna hata limoja alilotimiza. Kwa hivyo watu walishamjua na kuzoea vitisho vyake.
 
Putin kwa umaarufu wake huo ni kivutio zaidi na kwa hiyo wengi watajitahidi kumkamata au kumuua ili nao wajijengee umaarufu zaidi.
 
Endelea kuota ndoto za kitandani ukifanya masihara utakojoa ukijinyea kwa stress
Lakini huyo Yehodaya ametoa uchambuzi wake kuhusu hali ilivyo na pia akitabiri ni nini kinachoweza kufuatia.
Mbona sasa ww unatoa kashfa na kejeli badala ya ama kupinga kwa hoja au kuunga mkono kwa hoja.
 
Naunga mkono hoja.
Ni kweli Putin alishatepeta mno na hata ukiangalia sababu zilizomfanya aivamie Ukraine ni kwamba Ukraine aklitaka kujiunga na NATO na ndipo Urusi anastuka kwamba kitendo cha Ukraine kikikubaliwa manake adui yake amemfikia mlangoni na hatakuwa na pa kukimbilia tena na atakuwa ameishiwa pumzi jumla. Lakini kwa upande wake Putin hii ni Too late kwani mahesabu yalishapigwa na matokeo kudhihirika.
 

Nisiwafanye mkiwa na nani, nimekuambia kesi ilijifia kwa kukosa ushahidi, aidha mashahidi wengi walihongwa au kuuawa mitaani....
Kimsingi na narudia tena, ICC imesaidia kuleta amani Kenya na mataifa mengi Afrika, madikteta wengi wamekua makini sana baada ya kujua wanaweza wakaburuzwa.
Na hata huyo 'mungu' mtu wenu iko siku yake tu, kama hatafia kwa risasi Klemrin, basi ICC itamhusu maana Urusi itaendelea kubinywa mpaka imuachie.
 
kwahiyo ICC haina mamlaka hayo kwa nchi zenye nguvu ila nchi za duniani ya 3 ina mamlaka juu yao
 
Rais wa South Africa Ramaphosa:- South Africa inaitambua hati halali ya kukamatwa kwa Putin.

Waziri wa ujeruman:- ujeruman Itamkamata Putin endapo atakanyaga Ujeruman.
😁😁
 
Wangeanza na George W Bush kwa mauaji aliyofanya nchini Iraq, na Barrack Obama kwa alichokifanya nchini Libya hadi alikiri alikosea katika awamu yake ya mwisho ya Urais. Wakishindwa kuwakamata hao, wao ni mbwa asiye na meno anabweka tu.
 
Lini George W. Bush atakamatwa ?
Lini Baraka Obama atakamatwa?
Lini Tommy Blair atakamatwa?
Waache unafiki.

Wameishiwa waanze na hawa kwanza ndio tutawaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…