Mahakama ya Mafisadi imekufa kifo cha kawaida?

Mahakama ya Mafisadi imekufa kifo cha kawaida?

Hakuna ufisadi bila ushiriki wa watumishi wa uma kwa namna moja ama nyingine. Kusuasua kwa kesi zinazohusu ufisadi hutokana na kuwa washitaki wanahusika kwenye hizo tuhuma pia.
Siyo rahisi kuwashitaki na kuwatia hatiani Singh na Rugemalila bila kuwaunganisha na watumishi we serikali waliohusika.
Kiujumla siioni mahama special kwaajili ya mafisadi hapa nchini

Kwa sasa ilitakiwa ioneshe makucha yake, wahujumu uchumi wapo wengi tu sio lazima watumishi wa serikali wahusike
akina Manji hawa wote ni wahujumu, tupia akina Jamali malinz nk wote hawa ilitakiwa mahakama ya mafisadi iwashuhulikie na sio kuwajaza kisutu ambako mrundikano wa kesi ni mkubwa zaidi

D.A"mwanaume mashine"
 
Sheria inamapungufu kadhaa Mahakama ilianzishwa kisiasa sana hivyo inahitajika maboresho kidogo ya hiyo sheria ndy Mahakama ianze kazi.

Hivyo soon sheria itakapofanyiwa maboresho itaanza kazi hata hawa kina Rugemalila watapelekwa tu huko.
Acha kuongelea jambo jama huna ABC zake! Ni kutaarifu tuu kuwa mahakama ya mafisadi ina case nyingi tuu...Zikiweo hizo zakina Rugemalira lakini case ikiwa katika hatua ya awali inaendelea kutajwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi hadi hapo utaratibu na upelelezi utakapo kamilika...Baada ya hapo inaanza kusikilizwa kwenye mahakama ya mafisadi.

Na ndio maana maombi yote ya dhamana kwa watu wenye makosa ya uhujumu uchumi na ufisadi huyapeleka mahakama ya mafisadi maana huko ndio wanaweza kukupa au kuto kukupa dhamana.

Kwa kifupi case haiendi moja kwa moja kwenye mahakama ya mafisadi.
 
Kiujumla siioni mahama special kwaajili ya mafisadi hapa nchini

Kwa sasa ilitakiwa ioneshe makucha yake, wahujumu uchumi wapo wengi tu sio lazima watumishi wa serikali wahusike
akina Manji hawa wote ni wahujumu, tupia akina Jamali malinz nk wote hawa ilitakiwa mahakama ya mafisadi iwashuhulikie na sio kuwajaza kisutu ambako mrundikano wa kesi ni mkubwa zaidi

D.A"mwanaume mashine"
Watuhumiwa hao hawawezi kufanya vitendo vyao bila msaada wa watumishi wa serikali. Wao huwa na mipango (nia ovu au mens rea) ambayo kwayo bila kitendo kufanyika hakuna kosa.
Kosa hutimilika pale ambapo watumishi wa serikali hushirikishwa na kubariki utekelezaji (actus reus).
Unategemea serikali iwashitaki washirika wake katika kosa, watiwe hatiani halafu wahukumiwe?
Labda watumishi wote waandamizi waliokuwepo wakati kosa linatendeka wawe wameondoka.
Uthibitisho ni utetezi wa wazi wa dola kwenye sakata la escrow.
 
IPO Law school
Kuna siku
Mtuhumiwa alikua Kwenye
Land cruiser halafu polisi wakapanda karandinga
 
Mnakumbuka Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano.

Dkt Magufuli aliwaeleza wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa ya kuiongoza Tanzania,atahakikisha anaanzisha mahakama maalumu ya Mafisadi na Wala rushwa.

Baada ya kuingia ikulu ikaanzishwa mahakama ya mafisadi sambamba ya sheria yake.

Rais mwenyewe amekuwa akilia kwamba awamu ya nne ilijaa mafisadi chungu mzima. Wakati wa kampeni tukaambiwa mafisadi wamekimbilia UKAWA. Tukaambiwa CCM mpya.

Sasa ni miaka hakuna kinachoendelea zaidi ya kesi za tudagaa. Huku wanaotajwa kuwa mafundi wa ufisadi wakiendelea kula mema ya nchi.

Hivi kuna hata FUNDI mmoja wa ufasadi ametolewa kama mfano? Huu ndio wakati sasa wa kufanya remix ya song la mafisadi na sio kuwapiga madodoki mafisadi
 
Mbona hatutangaziwi kama inavyofanyika kwa kesi zilizopo Kisutu na Mahakama Kuu?Au mtu kutuhumiwa kwa ufisadi linakuwa jambo la siri?Majaji kuonekana mahakamani sio hoja.Mantiki ni je wanasikiliza hizo kesi?Ni za akina nani waliofisadi taifa letu?
Mahakama ya Mafisadi ipo, na jengo lake lipo nyuma ya ofisi za TCRA, na ndani ya geti la Law School. Kila siku watuhumiwa wanaletwa hapa na majaji wanakuja. Acheni kusambaza uongo eti hii mahakama haifanyi kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ya Mafisadi ipo, na jengo lake lipo nyuma ya ofisi za TCRA, na ndani ya geti la Law School. Kila siku watuhumiwa wanaletwa hapa na majaji wanakuja. Acheni kusambaza uongo eti hii mahakama haifanyi kazi
Hahahaha rejea sababu zilizofamya ikajengwa. Hakuna kesi ya maana hata moja ukiacha ya Yule Mkurugenzi sijui wa Halmashauri gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa zinasema kitilya na mkwe wa lowasa kesi yao imetolewa mahakama ya mafisadi kurudi mahakama za kawaida, bila shaka hii ni moja ya ahadi alizopewa endapo atarudi nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app


Mahakama zipo huru ndio sababu hata Jaji Sam Rumanyika akatoa hukumu ya Hovyo katika Historia ya Mahakama lakin haijaguswa wala kuonywa
 
Kimsingi mahakama za mafisadi hamna zile zilikuwa ni gia ya kutafutia tu kura. Mahakama zilizopo ni za kukandamiza demokrasia kwa kuwaadhibu wale wanaokataa kujiunga na ccm ili kuunga mkono juhudi.
 
Back
Top Bottom