mtz one
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 4,284
- 1,221
Utawala huu umejaa matendo ya rushwa kuliko tawala zote
Mahakama ya Ufisadi ilianza rasmi ikiwa ni jitihada za serikali ya awamu ya 5 kupambana na ufisadi nchini. Uazishwaji wa mahakama husika, uliambatana na uwepo wa kesi nyingi za uhujumu uchumi ikiwa ni uwepo wa wateja wa mahakama hiyo.
Wingi wa kesi hizo zikiwa bado katika hatua za mwanzo mahakamani Kisutu, jana limekuja wazo la kushauri uwezekano wa kusamehe watuhumiwa iwapo wataungama makosa na kuwepo uwezekano wa kulipa fedha kulingana na kiwango cha ufisadi.
Magwiji wa sheria naombeni mtujuze juu ya uwepo wa mahakama ya ufisadi iwapo kila mtuhumiwa ataamua kuungama na kuahidi kulipa kiasi cha fedha aliyofisadi.