Hii Mahakama jina lake rasmi ni Mahakama Kuu, Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, yaani Corruption and Organized Crime Division. Ni moja ya division za Mahakama Kuu. Division nyingine za Mahakama Kuu ni High Court Land Division, Labour, na Commercial.
Mwenye mamlaka ya kuamua ni kesi ipi inafaa kwenda division ipi ni DPP. Na anaamua kwa kuzingatia sheria na vigezo vya kikanuni.
Usiniulize kwani Kisutu ni Mahakama Kuu.
Ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, huwa ina exercise extended jurisdiction yaani, Hakimu Mkazi anapewa mamlaka ya kuwa Jaji na Mahakama ya Hakimu Mkazi inakuwa na hadhi ya Mahakama Kuu, na hivyo kuamua kesi za Mahakama Kuu. Na hata mtu akikata rufaa kutokana na hukumu hiyo, rufaa inaenda Mahakama ya Rufaa.
Mwanasheria ndiye atanielewa zaidi