Tetesi: Mahakama ya mafisadi kuwazoa mawaziri

Tetesi: Mahakama ya mafisadi kuwazoa mawaziri

Hii mahakama ya mafisadi nayo imekuwa hewa au imepatwa na nini?

Waziri Mkuu alituhakikishia kuwa mwezi Julay, 2016 Tanzania ingekuwa na mahakama ya Mafisadi.

Ni nini kimekwamisha huu mkakati wakati Rais alimtaka jaji mkuu asisubiri bunge kupitisha hii mahakama? Na pia tulisikia kuwa kuna pesa zilikuwa zimesha tengwa kwa ujenzi wa hii mahakama?

Serikali itufahamishe huu mchakato umefika wapi mpaka sasa? Serikali isipende kutudanganya watanzania kiasi hiki. Inabidi itambue kuwa "Mungu anawaona". Wengu tunatamani kumuona yule fisadi mliyekuwa mnatuambia kipindi cha kampain akifungua hii mahakama kama mshtakiwa wa kwanza.

WanaJF hebu

1474477744547.png


View attachment 404480
 
upembuzi yakinifu umeshafanyika...ila bado tunajadili iwe Dar au Dodoma,kama ni dodoma basi itabidi isubiri mpaka 2020.(in PM voice)
 
IT WAS JUST
Hii mahakama ya mafisadi nayo imekuwa hewa au imepatwa na nini?


Wazir mkuu alituhakikishia kuwa mwezi Julay, 2016 Tanzania ingekuwa na mahakama ya Mafisadi.

Ni nini kimekwamisha huu mkakati wakati Raisi alimtaka jaji mkuu asisubiri bunge kupitisha hii mahakama?
Na pia tulisikia kuwa kuna pesa zilikuwa zimesha tengwa kwa ujenzi wa hii mahakama?

Serikali itufahamishe huu mchakato umefika wapi mpaka sasa? Serkali isipende kutudanganya Watanzania kiasi hiki. Inabidi itambue kuwa "Mungu anawaona". Wengu tunatamani kumuona yule fisadi mliyekuwa mnatuambia kipindi cha kampain akifungua hii mahakama kama mshtakiwa wa kwanza.

WanaJF hebu
View attachment 404470

View attachment 404480
IT WAS JUST KIKI AND PROMO
 
Kama mumeshindwa kuwapeleka kwenye mahakama za kawaida basi uko kwa mahakama ya mafisadi ni maigizo tu pia ety kesi zitakuwa haraka ivi miezi 9 n haraka
 
Haya maigizo hunishangaza sana. Kila anayeingia madarakani anakuja na igizo la kupumbaza wananchi. Alipoingia madarakani JK aliingia na gia ya TAKUKURU na kuwajengea jengo jipya ili wachape kazi. Hebu uwekeni comments zetu hapa tujikumbushe kuhusu TAKUKURU.
 
Iwapo ccm isingejaa mafisadi nchi hii ingekuwa imeendelea sana. Mafisadi ndiyo imekuwa nguzo kubwa katika kufanikisha ccm kushinda.
Makamba, aliyekuwa katibu mkuu wa ccm, aliwahi kusema "ukitaka biashara yako iende au istawi vizuri jiunge ccm." Hakuna kiongozi wa ccm wala wa serikali aliyewahi kupinga kauli hii ya Makamba.
 
Yaani bado tu hamjagundua kwamba mahakama ya mafisadi ni delaying technique?! Kama kusingekuwa na na hii technique, kelele zingekuwa nyingi sasa "mbona mafisadi hawapelekwi mahakamani... mbona mafisadi hawapelekwi mahakamani!" Kinyume chake, raia mmetulia tulii kama maji mtungini mkisubiri mahakama ya mafisadi! Mkapa used the same technique kwa kuunda Kamati ya Jaji Warioba kuchunguza mianya ya ufisadi! Watu wakadhani baada ya ripoti ile ambacho kingefuata ni mafisadi kufikishwa mahakamani! Kinyume chake ambacho kilifuata ni ufisadi wa kutisha zaidi pengine kuliko ule ambao waliuundia tume!

Sitashangaa wakija mazombi watakaosema JPM sio Mkapa!!
 
Ndo wanamplizia kisasi eeh Bhakhera ahamishie nchi nyingine maana ukute kodi alikua analipa tu ila kutokuchangia chama tawala au Ku support wengine kuna mu cost
Gazeti wamesema kashfa ya kodi. Usipende kuongeza visivyokuwepo!
 
Ndio mwisho wa CCM, maana kuna wale Makada wa CCM waliotengeneza ARV feki, Kuna yule anayejifanya Usalama wa Taifa, Kuna wale wenye Majina Feki, kuna wale wenye miradi ndani ya Serikali, wanacheza dili, kuna wale waliojimilikisha mali za Taifa....
 
Wameshindwa vyeti bandia, kufichua wazungu wa unga, genge la majangiri wa tembo, wataweza katika hili?
 
Hyo mahakama ni maigizo tu kuwahadaa watu ufisadi ndo ngao ya ccm ka ilivo samaki na maji.
Upinzani hauna tofauti kwa sasa, ufisadi upo kwa chama tawala a upinzani. Hoja ya ufisadi imewekwa pembeni.
 
Back
Top Bottom