Mahakama ya rufaa yamfutia kesi ya Ugaidi Wilfred Lwakatare

Mahakama ya rufaa yamfutia kesi ya Ugaidi Wilfred Lwakatare

Kicheba One

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
399
Reaction score
194
Wana jamvi,
Ttaarifa za hivi punde ni kwamba, Wilfred Lwakatare Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili. Mahakama imetupilia mbali tuhuma zote kwakujiridhisha kuwa ni zakupika hivyo mpaka sasa Lwakatale yupo huru.

Mahakama ya rufaa Tanzania leo imetupilia mbali maombi ya marejeo yaliyopelekwa na Serikali kupinga uamuzi wa mahakama kuu ya Tanzania kumfutia Mashtaka ya ugaidi mkurugenzi wa Ulinzi na usalama Chadema Wilfred Muganyizi Lwakatare.

Hii ni baada ya kukubaliana na hoja za wakili wa Chadema kuhusu mapungufu ya kisheria katika maombi hayo.


Lwakatare achomoka kesi Ugaidi | East Africa Television
Baada ya maamuzi hayo ya Mahakama, Mbunge Lwakatare amefunguka na kusema serikali imeona haina nia ya kuendelea na mapingamizi hayo katika Mahakama ya Rufaa na kudai kwake yeye ni jambo ambalo anamshukuru Mungu.

"Kama ilivyokuwa tangu awali na kama ambavyo Mahakama Kuu imeona hakukuwepo na njama zozote hii ni mipango ambayo ilikuwa imefanywa hata sielewi kwa sababu zipi jambo ambalo wataalamu, watafiti watakuja kutueleza siku za mbele kwamba sababu zote zilikuwa ni nini, namshukuru Mungu lakini pia nawashukuru Mawakili ambao wamejitoa kuanzia mwanzo kwani wamefanya kazi kubwa sana" alisema Lwakatare

Aidhaa Lwakatare amesema alikuwa hatarajii maamuzi ambayo yamefanywa na mahakama ya rufaa dhidi yake na kusema ndiyo maana amekuwepo jijini Dar es Salaam kwa takribani wiki nzima kujiandaa kwa kesi hiyo.

"Kwa wafuatiliaji wa kesi hii kama mnakumbuka mtiti uliokuwepo ambapo nilikaa ndani katika mahabusu ya Keko kisha nikaamishiwa Segerea kwa muda zaidi ya miezi minne na nafikiri unakumbuka jinsi kesi hii ilivyokuwa na taswira kitaifa kwanza msafara uliokuwa unanisindikiza mahakamani zaidi ya polisi 50, magari zaidi ya 10 hata nikiwa naenda hospitali wakati naumwa nasikindikizwa hivyo hivyo, hospitali kama Muhimbili wanazuiliwa kufanya shughuli zozote mpaka mimi nitibiwe niondoke ndiyo waanze kuhudumia watu wengine, kimsingi kesi ilikuwa inatisha sana" alisisitiza Lwakatare

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mwezi Machi 2013 ilimfutia kesi ya makosa ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph, baaadaye Jamhuri ilikata rufaa kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu.
 
Tukae chonjo sasa kama GAIDI anarudi mtaani
 
Duuu... sasa zile mbwe mbwe zote za kamanda @kova , mara kampiga tanchi usiku wa manane....mara kanyang'anywa laptop. kumbe zote hizo zilikuwa ni mbio za sakafuni tu?
 
Ole wa nchi na bahari maana yule mshitaki wenu kaja duniani.
 
Mahakama ya rufaa Tanzania leo imetupilia mbali maombi ya marejeo yaliyopelekwa na serikali kupinga uamuzi wa mahakama kuu ya Tanzania kumfutia Mashtaka ya ugaidi mkurugenzi wa Ulinzi na usalama Chadema Wilfred Muganyizi Lwakatare.

Hii ni baada ya kukubaliana na hoja za wakili wa Chadema kuhusu mapungufu ya kisheria katika maombi hayo.
 
Ila anakesi ya kumteka msack ambayo ni jinai hata mungu anajua hayo.
 
Duuu... sasa zile mbwe mbwe zote za kamanda @kova , mara kampiga tanchi usiku wa manane....mara kanyang'anywa laptop. kumbe zote hizo zilikuwa ni mbio za sakafuni tu?
Lwakatare bado ni gaidi tu hata jamii inajua hivyo.
 
Fedha za escrow zitakuwa zimetembea. Siamini kama Rugemalila aliacha kumuokoa ndugu yake
 
Mwigulu ndo gaidi number moja. Kuokoka kwani nini, maana kwa sasa ni bora kulala na samba kuliko anayejiita ameokoka. Naye adaiwe hela na gharama zote hizo
 
Hivi Mwigulu anakumbuka kweli hii kitu na uratibu wake? Nakumbuka pia alisema anao ushahidi wa video kuthibitisha tuhuma za ugaidi dhidi ya CDM, ambao angeumwaga hadharani mitandaoni muda wowote. Mheshimiwa Mwigulu muda ndio huu.
 
Ila anakesi ya kumteka msack ambayo ni jinai hata mungu anajua hayo.

Zaidi ya kesi ya ugaidi, hii ni kesi namba ngapi? Ilifunguliwa Mahakama ipi? Sio lazima ujibu lakini, kama hujui kauka.
 
Back
Top Bottom