Mahakama ya rufaa yamfutia kesi ya Ugaidi Wilfred Lwakatare

Mwigulu sasa hivi ni kiongozi mambo ya siasa hayuko kivile tena ndio maana hata hii ishu ya escrow alisema wahusika wote wafilisiwe na kufungwa gerezani.anapanda kweli yule wa tra alimsimamisha mara moja na pesa kaambiwa arudishe
 
Ila anakesi ya kumteka msack ambayo ni jinai hata mungu anajua hayo.
Wewe nawe unasema hili suala la ugaidi hata Mungu analijua, kauli yako inafanana fanana na ya Bosi wako Mwigulu, ambaye alisema anao ushahidi wa kutosha kuhusu Lwakatare kujihusisha na ugaidi, ambapo yuko tayari kuutoa hapa Diniani na hata Mbinguni.

Sasa tukuulize Simiyu yetu, mbona bosi wako Mwigulu kashindwa kuuwakilisha huo ushahidi wake alotamba kuwa nao, kwenye hiyo mahakama ya Rufaa?!

Sasa kama hata hapa duniani tu, huyo Mwigulu, 'amegwaya' kutoa huo ushahidi wake wa 'mangumashi' wa ugaidi.

Sasa huko mbinguni, anakotamba kuwa nako atauwasilisha ushahidi wake, si ndiyo ataingia nao mitini pale kwenye lile eneo la kulia na kusaga na meno?
 
Duu jamaa ashukuru sana amepona,maana yule wa Arusha alishabebesha hukumu isiyo yake,lakini tushaizoea serikali yetu.
AMANI IENDELEE KUTAWALA TANZANIA.
 
Duu jamaa ashukuru sana amepona,maana yule wa Arusha alishabebesha hukumu isiyo yake,lakini tushaizoea serikali yetu.
AMANI IENDELEE KUTAWALA TANZANIA.
 
Yule aliyesema atatoa ushahidi duniani na mbinguni yupo wapi na ushahidi wake? Bwana madelu nchemba lete ushahidi wa mbinguni sasa.
 
Ya Escrow yametoka wapi hapa?

Tunajadili kuhusu Gaidi Rwakatare kuachiwa.

Wewe sikuhizi upo juu ya Sheria? Kama mahakama imesema siyo wewe ndio umekua msemaji mkuu? Wacha mambo yakilumumba
 
Wale waliokula Hela ya Escrow na Bunge kuwabaini wamefikishwa wapi? Shirikisha ubongo
Hawajafikishwa kokote, na badala yake ndiyo kwanza wabunge wetu wameichukua kesi ya ngedele na kumpelekea......

Hivi kwa kibuli walichokionyesha akina Muhongo, kwa kukataa kabisa kujiuzulu, hivi hiyo si ishara ya wazi kabisa kuwa kwenye hilo dili, hao akina Werema ni kama tu walikuwa 'matarishi' wa kupeleka vimemo vya kufanikisha hilo dili wakitekeleza maagizo ya mkulu?!

Na hilo group la kina Maswi, lishampiga mkwara mzito, mkuu wa kaya, kuwa akithubutu tu kumwaga ugali kwa 'kuwamwaga' wao, basi nao hawatasita kumwaga mboga, kwa kueleza mhusika mkuu wa hiyo dili!

Kwa hiyo kazi imesalia kwake, mkuu wa kaya, aamue kusuka au kunyoa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…