Kama mnavyofahamu, kumekuwa na mvutano mkubwa wa kisheria kati ya Bw. Eliakim Chacha Maswi na Mbunge Mwita Waitara, ukihusisha fidia ya mabilioni ya shilingi.
Leo nimepitia hukumu mpya ya Mahakama ya Rufaa kupitia hukumu iliyotolewa leo tarehe 29 Julai 2026, na nimeona ni vyema niwaletee uchambuzi mfupi wa nini hasa kimeamuliwa na kwa nini Maswi amekosa ile bilioni 6 aliyokuwa ameshinda awali.
👇🏽
Hapa chini ni muhtasari wa kilichojiri na kilichoamuliwa na Mahakama ya Rufaa chini ya Majaji Levira, Fikirini, na Issa.
Maswi alidai kuwa tarehe 9 Agosti 2023, Waitara alitoa maneno ya kumkashifu kwenye mkutano wa hadhara (kwamba anajihusisha na rushwa, anatumia vibaya ofisi, n.k.), na baadaye maneno hayo yakarushwa mtandaoni kupitia YouTube channel ya Mara TV.
Mahakama Kuu ilimpa ushindi Maswi na kuamuru alipwe fidia ya jumla ya Tsh. Bilioni 6 (Bilioni 1 kama fidia ya adhabu, na Bilioni 5 kama fidia ya jumla). Akina Waitara hawakuridhika, wakakata rufaa.
Leo nimepitia hukumu mpya ya Mahakama ya Rufaa kupitia hukumu iliyotolewa leo tarehe 29 Julai 2026, na nimeona ni vyema niwaletee uchambuzi mfupi wa nini hasa kimeamuliwa na kwa nini Maswi amekosa ile bilioni 6 aliyokuwa ameshinda awali.
👇🏽
Hapa chini ni muhtasari wa kilichojiri na kilichoamuliwa na Mahakama ya Rufaa chini ya Majaji Levira, Fikirini, na Issa.
Asili ya Mgogoro
Bw. Eliakim Maswi (Mjumbe wa zamani wa PPRA) aliwafungulia mashitaka ya kuchafuliwa jina (Defamation) Mwita Waitara (Mkata Rufaa wa 1), Karoli Jakob Karoli (Mkata Rufaa wa 2), na Mara TV (Mkata Rufaa wa 3) katika Mahakama Kuu kule Musoma.Maswi alidai kuwa tarehe 9 Agosti 2023, Waitara alitoa maneno ya kumkashifu kwenye mkutano wa hadhara (kwamba anajihusisha na rushwa, anatumia vibaya ofisi, n.k.), na baadaye maneno hayo yakarushwa mtandaoni kupitia YouTube channel ya Mara TV.
Mahakama Kuu ilimpa ushindi Maswi na kuamuru alipwe fidia ya jumla ya Tsh. Bilioni 6 (Bilioni 1 kama fidia ya adhabu, na Bilioni 5 kama fidia ya jumla). Akina Waitara hawakuridhika, wakakata rufaa.
Sababu za Mahakama ya Rufaa Kutengua Hukumu ya Bilioni 6
Baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, Mahakama ya Rufaa imekubaliana na akina Waitara na kufuta hukumu ya Mahakama Kuu kutokana na sababu kuu mbili:- Kushindwa Kuthibitisha Usambazaji (Failure to Prove Publication): Kesi hii ilifunguliwa chini ya Sheria ya Huduma za Habari (Media Services Act). Sheria hii inataka kuthibitisha kuwa taarifa ilisambazwa kwa "watu wengine" kupitia vyombo vya habari/mtandao. Ingawa Maswi alileta "flash disk" (Kielelezo P3) kuonesha video ya YouTube, mahakama ilipoicheza ilionesha watazamaji (viewers) sifuri. Maswi hakumleta shahidi yeyote (hata mkewe, mwanawe, au mtu aliyempigia simu kumtaarifu) kuthibitisha kuwa waliona hiyo video mtandaoni na ikashusha hadhi yake mbele yao. Watu waliokuwa kwenye mkutano wa hadhara hawakuhesabika chini ya sheria hii ya kimtandao.
- Kukosekana kwa Ushahidi wa Madhara (No Proof of Injury): Sheria ya kuchafuliwa jina inataka kuthibitisha kuwa "hadhi yako ilishuka mbele ya jamii" (kupoteza kazi, heshima, au wateja). Mahakama ya Rufaa imebaini kuwa, badala ya kushushwa hadhi, baada ya tukio hilo Maswi alipandishwa cheo kutoka kuwa Mkurugenzi wa PPRA na kuteuliwa na Rais kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria. Hii inathibitisha kuwa mwajiri wake na jamii hawakupoteza imani naye, hivyo hakukuwa na madhara yaliyohalalisha yeye kulipwa fidia ya Bilioni 6.