Mahakama ya Rufani: Maamuzi ya Rais kuhusu Wafanyakazi wa Umma ni ya mwisho

Nini hii? Rais ndiyo muajiri mkuu na mfukuzaji mkuu, halafu uamuzi wake uwe wa mwisho?
Naona kama mahakama imejishusha hadhi!
Hebu wataalamu tusaidiane!
 
Huu uamuzi binafsi nimeomba TLS iombe mapitio/marejeo kwa CA.
.
Wakuu wamejielekeza vibaya, they’ve open Pandora Box!.
.
That means all pending cases, judgment , execution is nullity
 
Hukumu iko sahihi kabisa, tatizo ni kwenye mfumo wetu wa utumishi ambapo civil service commission iko under control ya wizara, na hivyo moja kwa moja kuwa chini ya rais.
 
Huu uamuzi binafsi nimeomba TLS iombe mapitio/marejeo kwa CA.
.
Wakuu wamejielekeza vibaya, they’ve open Pandora Box!.
.
That means all pending cases, judgment , execution is nullity
Sure, zinakufa kibudu automatically
 
Hukumu iko sahihi kabisa, tatizo ni kwenye mfumo wetu wa utumishi ambapo civil service commission iko under control ya wizara, na hivyo moja kwa moja kuwa chini ya rais.
Hukumu haipo sahihi, sheria inayotoa haki za wafanyakazi ni sheria ya ajira na mahusiano kazini na sheria hiyo ndiyo iliyotoa tafsiri ya neno "dispute" (mgogoro). Kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kimeeleza kuwa sheria hiyo inatumika kwa wafanyakazi wa sekta zote mpaka wa serikali (watumishi wa umma), na kifungu cha 14(1) cha sheria ya mahakama za kazi inaeleza kuwa migogoro ya kazi itapelekwa CMA. Sasa hukumu hii maana yake imetengua kifungu cha 2(1) cha Sheria ya Ajira na mahusiano kazini kuwa itatumika kwa wafanyakazi wasio wa serikali tu.

Kumbuka sheria ya utumishi wa umma haitoi wala kueleza haki za wafanyakazi bali inaeleza kazi za taasisi za serikali kwenye utendaji wa utumishi wa umma. Kwenye sheria ya utumishi wa umma, mkosaji ni mwajiriwa tu na sio mwajiri
 
Sure, zinakufa kibudu automatically
Haki Haihitaji Indoor Meetings.

Haki Inatakiwa Ionekane. Itachelewa Lakini Itaonekana.
.
Wamethibitisha Ufinyu wa Weledi Katika Kutekeleza Majukumu Yao.
.
HAKI YAKO NI MUHIMU KULIKO MAELEKEZO YAO.

[emoji375][emoji375]
 
HV MTU AKIENDA CMA AKASHINDWA ANAWEZA KWENDA KWA RAISI?
 
Inaelekea sheria unazijua au una elimu ya sheria. Asante kwa contribution nzuri. BTW kusema kuwa mambo yaishie kwa rais hakutafanya wafanyakazi kukosa haki hasa rais anapokuwa mtu zimezibuka kama Mwendazake? Naona ni kama kusema tajiri ndiye atakayekuwa na maamuzi ya mwisho kuhusu wafanyakazi wake na mahakama haiwezi kuingilia.
 
... sitaki kuamini Mahakama ya Rufani (Supreme Court of the land) imekuwa low kwa kiwango hiki.
 
anatakiwa akate rufaa kwenda Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maamuzi ya Rais yatakuwa ya mwisho, hii ni Kwa mujibu wa Kifungu Cha 25 Cha sheria ya utumishi wa umma Public Service Act (Cap 298 R.E. 2019)
Hii sheria kama iko hivi ni hatari sana.... Rais ndie mkuu wa utumishi, halafu mfanyakazi ana kesi na utumishi; inakuwaje tena Rais awe mwamuzi wa mwisho? Au kuna kitu kimeachwa hapa? Hakuna nafasi ya mahakama hapa? Pascal Mayalla hebu tupe mwanga kidogo
 
Kwa sababu vyombo vinaripoti kwake. Tusimwangalie kama individual. Tumwangalie kama system au taasisi.
Ana rasilimali za kumtosha kufanya uamuzi sahihi.
Hebu tukumbushe ya Tozo ya shs 100 kwenye mafuta ilikuwaje?
 
Watu wengi wanatafsiri vibaya, Sheria ya Utumishi wa Umma inataka watumishi wa Umma waexhaust all remedies kabla ya kwenda CMA au Mahakamani. Hivyo Mtumishi wa Umma (ambapo hata Mashirika ya Umma yanaangukia ndani ya Utumishi wa Umma) wanatakiwa wakiwa aggrieved na maamuzi ya mamlaka zao za ajira au nidhamu (hapa ni mambo yote disputes na nidhamu) wanatakiwa wakate rufaa Tume ya Utumishi wa Umma na wasiporidhika na uamuzi basi wakate rufaa kwa Rais, Rais akishatoa uamuzi wake ambapo ni highest kwenye Executive hapo sasa wanaweza kwenda Mahakamani.

Kilichokuwa kinafanyika ni watumishi wa umma kwenda CMA kabla hawajaexhaust all remedies kama Sheria ya Utumishi wa Umma Kifungu 32A kilivyotamka.
 
Wewe ni mmoja wa wanaotafsiri vibaya sheria ya utumishi wa umma hususani kifungu cha 32A. Hebu itafyte sheria hiyo na usome kifungu hicho halafu uone kama kinaeleza kuhusu watumishi wa umma wote (all public servants) au ni kifungu kwa kundi fulani tu la watumishi wa umma (operational service). Yaani usome na uone kama kifungu hicho kinatumika mpaka watumishi maofisa!!!

Halafu hilo neno dispute kama ulivyoliweka, umelitoa wapi mkuu, maana sheria ya utumishi wa umma haina tafsiri ya neno dispute bali sheria ya ajira na mahusiano kazini ndiyo yenye tafsiri ya neno dispute. Unavyosema dispute zinatakiwa kuamriwa ndani na wasiporidhika wakate rufaa utumishi wa umma, ni kifungu kipi cha sheria gani kinachoeleza hayo?
 
Hicho kifungu cha 32A cha Sheria ya Utumishi wa umma, alikiweka mwendazake ili aweze kuwadhibiti wale walioitwa watumishi wa umma wenye vyeti feki. Hakutaka waende CMA, akaona njia ya kuwabana ni kwa kuongeza hicho kifungu cha 32A, hapo akawa amesahau kuwa kifungu hicho hakiwahusu maofisa (watumishi wa umma wenye shahada - degree), matokeo ni kuwa mawakili wa serikali wakaiongoza vibaya mahakama kuwa kifungu cha 32A kinawazuia watumishi wote wa umma kwenda CMA, na hapo Mahakama haikusoma kwa kina sheria ikajipiga piga mitama na kuwa na maamuzi tofauti tofauti (mahakama kuu) na sasa mahakama ya Rufaa ndio imetoa uamuzi wa mwisho ambao imejipotosha kabisa kuwa kutafsiri vibaya kifungu hichohicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…