Mahakama ya Rufani: Maamuzi ya Rais kuhusu Wafanyakazi wa Umma ni ya mwisho

Kwa majibu haya ya mahakama,tusishangae kujikuta tuna watumishi wasio waadilifu sababu hawajui kesho yao.
na hata wakienda mahakamani wataambiwa rudini kwa mwajiri wenu awape majibu.

Watu wataanza kutumia vibaya nafasi zao ili kujinufaisha mapema kabla hayajawakuta.
Na hapa wa kuumia ni sisi raia ambao tutake tusitake ni lazima twende kupata huduma kwenye
ofisi za umma ambazo hazina mbadala wake.
 
Hiki
Hiki kifungu kineanza lini?na je waliofukuzwa kazi kabla ya kifungu hiki wanafanyaje?
Hiki kifungu kineanza lini?na je waliofukuzwa kazi kabla ya kifungu hiki wanafanyaje?
Hiki kifungu kimeanza mwaka 2017
Lengo kuu hasa ni watumishi wasio na cheti kidato cha nne....
Mwendazake aliona wengi watakimbilia CMA... Akaamuwa kuwapiga pini wasiende huko na yeye mwenyewe awe muamuzi wa mwisho na sio mahakama...

Moja ya kifungu cha hovyo kufanyiwa marekebisho... Kabla ya hapo watumishi walikuwa wanakwenda CMA
 
Pamoja na nia yake ya kutaka kuwapiga pin watumishi, bado wanasheria wake mwendazake walidraft vibaya kifungu hicho na kukifanya kisiwe na maana yoyote na wanasheria haohao wakawa wanakitumia kuielekeza vibaya mahakama kufikia maamuzi, na wakafanikiwa kwa kutufikisha hapa tulipo sasa.

Sasa tunaitaka mahakama ya Rufaa ipitie uamuzi wake na kujitafakari na kubadili ilichokisema kwa kuwa kifungu cha 32A hakijatoa mamlaka ya CMA kusikiliza kesi bali ni mawazo tu ya mwendazake na wanasheria wake ambayo walishindwa kuyaweka kisheria ila wakawa wanayuzungumza mahakamani (just thoughts with no legal back up)...tunataka CMA irejeshewe mamlaka yake japo nako ma-arbitrator ni kama wameshakontroliwa hivi kwa sasa
 
Mkuu ni kweli... kuna kesi moja ngoja nijaribu kuweka attachments..
Yaani moja ya sheria ya hovyo...
 
Attachments

Mkuu ni kweli... kuna kesi moja ngoja nijaribu kuweka attachments..
Yaani moja ya sheria ya hovyo...
Jaji Matupa hapa alieleza vyema sema sasa CAT ndio wametoa uamuzi wa kuiondolea mamlaka CMA, hapa bila kubatilisha uamuzi huo, ndio inakuwa "sheria" sasa malalamiko kwenda Tume ya Utumishi wa umma. Kifungu cha 32A kinakuwa kimepewa nguvu na mahakama
 
Hapa Jaji anasema sio kila mtumishi wa Serikali anaangukia katika sheria ya utumishi wa umma....
Wanasheria wa Serikali wamejaribu sana kupotosha Mahakama...
 
Attachments

Jaji Matupa hapa alieleza vyema sema sasa CAT ndio wametoa uamuzi wa kuiondolea mamlaka CMA, hapa bila kubatilisha uamuzi huo, ndio inakuwa "sheria" sasa malalamiko kwenda Tume ya Utumishi wa umma. Kifungu cha 32A kinakuwa kimepewa nguvu na mahakama
Jaji Matupa hapa alieleza vyema sema sasa CAT ndio wametoa uamuzi wa kuiondolea mamlaka CMA, hapa bila kubatilisha uamuzi huo, ndio inakuwa "sheria" sasa malalamiko kwenda Tume ya Utumishi wa umma. Kifungu cha 32A kinakuwa kimepewa nguvu na mahakama
Wakuu ,

Inabidi hii 32A iangaliwe... Watu bado wanaonewa sana
 
Nashukuru kwa ufafanuzi Mkuu, maana kuna ndugu yangu ni Mhanga, amekata Rufaa kwenda kwa Rais mara baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Rufaa amekata tangu mwaka 2019, lakini bado hajajibiwa mpaka sasa.
Majibu kashapata u??
 
Wakili msomi Peter Kibatala amejitolea kumtetea Jonas Afumisye Mwangunga aliefukuzwa kazi na shirika la TRC kwa kupinga TOZO, wakili Kibatala amesema endapo Jonas atakwenda Mahakamani kutafuta haki yake yeye yupo tayari kumtetea bure.
 
Shetani alibadilisha sheria ili kuumiza watu
 
Anaweza ila ni mpaka amalize hatua zote za ndani, yaani aende tume ya utumishi watoe amri na kama hajaridhika aende kwa Rais nako akiwa hajaridhika na maamuzi ndio waende mahakamani. Hiyo ni timeframe ya kama miaka 4 hivi
 
Hapo tume tuu inaweza ikakaa hata miaka mitatu
 
Judicial review inahitajika kwa sheria hizi kandamizi za wafanyakazi.
 
Anaweza ila ni mpaka amalize hatua zote za ndani, yaani aende tume ya utumishi watoe amri na kama hajaridhika aende kwa Rais nako akiwa hajaridhika na maamuzi ndio waende mahakamani. Hiyo ni timeframe ya kama miaka 4 hivi
Mkuu sajo hivi ofisi ya raisi rufaa huchukua muda gani?
 
Mkuu sajo hivi ofisi ya raisi rufaa huchukua muda gani?
Hakuna muda wa kisheria uliowekwa kwa Rais kutoa uamuzi wa Rufani , lakini uzoefu unaonesha ni kati ya miaka 2 na kuendelea (wengine mpaka miaka 5 huko), yaani Rais anatoa uamuzi wa rufaa pake atakapojisikia kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…