Mahakama ya Rufani Tanzania imemuachia huru Deo Kisandu (Civilian Coin) mwanasiasa aliyeacha Siasa

Mahakama ya Rufani Tanzania imemuachia huru Deo Kisandu (Civilian Coin) mwanasiasa aliyeacha Siasa

Hivi kwani siku hizi hizo mahakama hazijui kutofautisha mtu timamu na mwenye matatizo kiakili?
 
Jamaa yangu sana huyu! Hana baya na mtu! Hata waliomfunga watakuwa walimuonea tu. Binafsi ninamsubiri kwa hamu sana humu jukwaani.
Ndio katika jela nazani hata Hali ya kiuchumi bado haijakaa sawa.
Nitafurahi sana ,ukimuona huko mwambie mwanaye nyoka bado nipo napambana na maisha
Kwa urahisi mtafute Facebook naona huko Yuko active sana
 
Ikumbukwe Bwana Civilian Coin au Kisandu alifungwa na Mahakama ya wilaya ya Kahama miaka 7 jela kwa kosa la "Kumtaja mtu mchawi" tangu tarehe 11 April 2022, Aiza Civilian Coin alikata rufaa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa huku akitumikia kifungo gerezani, lakini Mahakama ilitupilia mbali malalamiko yake mnamo tarehe 27 April 2023. Civilian Coin mtoto wa Kisandu hakurizika, alikata Tena rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania na tarehe 9 March 2026 Mahakama ya Rufani ilimuachia huru baada ya kuridhishwa na utetezi wake na hivyo tarehe 11 march2026 magereza nayo ilimtoa rasmi gerezani na kuwa huru.

Civilian Coin-mtoto wa Kisandu aliwahi kuwa kutangaza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 2012 akiwa Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) mkoa wa tanga na pia aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa NCCR MAGEUZI Taifa kitengo Cha Vijana na mjumbe wa Halmashauri kuu wa Chama hicho. Civilian Coin-mtoto wa Kisandu alishaga achana na Siasa miaka mingi kidogo baada ya kupoteza sifa za kugombea Urais baada ya kufungwa Mara ya kwanza mwaka Desemba 2018 na Mahakama ya Hakimu mkazi_Mwanza na kunyimwa nakala ya hukumu mpaka akamaliza kifungo huko gereza Kitengule-Kyaka Karagwe akitoke gereza Butimbs tarehe 26 Juni 2020. Kwa kesi ya "Kutoa taarifa za uongo kwenye mfumo wa kompyuta" unaoitwa Facebook.

Kifungo Cha pili amezungushwa magereza mengi akitokea gereza Kahama baadae gereza Shinyanga, na gereza Malya_Maswa na gereza Msalato_Dodoma mpaka anaachiwa huru juzi alirudishwa gereza Shinyanga akitokea gereza Msalato_Dodoma mwezi February

Pia soma Deo Kisandu afungwa jela miaka 7 kwa kumuita mama yake mzazi mchawi

2026

View attachment 3558521

Naweka picha zake na wimbo wake mmoja baada ya kujiondoa kwenye Siasa na kukomalia Sanaa na Uandishi wa habari.


View: https://youtu.be/PCVVeUzbe8Y?si=0aSz6oGY1FFZooH2

View attachment 3558519

Jifunze kuandika kiswahili,hii nchi itakua na shida sana mbeleni,ukute ni mhitimu wa shahada ya chuo kikuu
 
Huyu mwehu tu hana madhara ni bangi tu inamsumbua.
Hata jela kwenyewe kumuweka ni kupoteza rasilimali tu.
Mirembe pangemfaa sana tu
 
Hivi inakuwaje mfungwa anahamishwa jela, je Kama Ana rufaa inakaaje hapo.
Sababu zipo nyingi sana, Kama vile askari anavyoamishwa hata Mfungwa nae uhamishwa pia Sababu za usalama/ulinzi/msongamano/kiafya/mahitaji maalum

Jamaa sema nae anahistoria sana kutoka kusomea Upadre kuwa mwalimu, Mwanasiasa na mwandishi hadi kuwa mjela jela OG
 
Back
Top Bottom