Mahakama ya Rufani Tanzania imemuachia huru Deo Kisandu (Civilian Coin) mwanasiasa aliyeacha Siasa

Ikumbukwe Bwana Civilian Coin au Kisandu alifungwa na Mahakama ya wilaya ya Kahama miaka 7 jela kwa kosa la "Kumtaja mtu mchawi" tangu tarehe 11 April 2022, Aiza Civilian Coin alikata rufaa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga akiwa huku akitumikia kifungo gerezani, lakini Mahakama ilitupilia mbali malalamiko yake mnamo tarehe 27 April 2023. Civilian Coin mtoto wa Kisandu hakurizika, alikata Tena rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania na tarehe 9 March 2026 Mahakama ya Rufani ilimuachia huru baada ya kuridhishwa na utetezi wake na hivyo tarehe 11 march2026 magereza nayo ilimtoa rasmi gerezani na kuwa huru.

Civilian Coin-mtoto wa Kisandu aliwahi kuwa kutangaza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 2012 akiwa Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) mkoa wa tanga na pia aliwahi kuwa Katibu Mwenezi wa NCCR MAGEUZI Taifa kitengo Cha Vijana na mjumbe wa Halmashauri kuu wa Chama hicho. Civilian Coin-mtoto wa Kisandu alishaga achana na Siasa miaka mingi kidogo baada ya kupoteza sifa za kugombea Urais baada ya kufungwa Mara ya kwanza mwaka Desemba 2018 na Mahakama ya Hakimu mkazi_Mwanza na kunyimwa nakala ya hukumu mpaka akamaliza kifungo huko gereza Kitengule-Kyaka Karagwe akitoke gereza Butimbs tarehe 26 Juni 2020. Kwa kesi ya "Kutoa taarifa za uongo kwenye mfumo wa kompyuta" unaoitwa Facebook.

Kifungo Cha pili amezungushwa magereza mengi akitokea gereza Kahama baadae gereza Shinyanga, na gereza Malya_Maswa na gereza Msalato_Dodoma mpaka anaachiwa huru juzi alirudishwa gereza Shinyanga akitokea gereza Msalato_Dodoma mwezi February

Pia soma Deo Kisandu afungwa jela miaka 7 kwa kumuita mama yake mzazi mchawi

2026

View attachment 3558521

Naweka picha zake na wimbo wake mmoja baada ya kujiondoa kwenye Siasa na kukomalia Sanaa na Uandishi wa habari.

View: https://youtu.be/PCVVeUzbe8Y?si=0aSz6oGY1FFZooH2

View attachment 3558519

Mwamba karudi tena uraini. Tusibiri nyuzi za kufa mtu sasa
 
Kwa mujibu wa Malisa Godlisten ndugu yetu kabisa Deo Kisandu ameshinda Rufaa ya kesi yake ya mchongo, tunamkaribisha uraiani na JF kwa ujumla. Legends wa JF wanakumbuka vituko vyake.

Mnamkumbuka huyu jamaa? Anaitwa Deogratius Kisandu. Aliwahi kuwa Katibu wa BAVICHA mkoa wa Tanga, mgombea ubunge jimbo la Lushoto kupitia Chadema. Baadae akahamia NCCR Mageuzi na kuwa Msaidizi binafsi (PA) wa Mwenyekiti Mbatia, kisha akawa Katibu Mwenezi wa chama hicho taifa.

Mwaka 2018 alikamatwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo mtandaoni. Akashtakiwa na kupatikana na hatia. Akafungwa miaka miwili. Akatumikia kifungo chake gereza la Butimba Mwanza kwa mwaka mmoja na kwenda kumalizia adhabu gereza la Kitengule Kagera.

Alipotoka tu, akarudi mtandaoni na kuandika kuwa kuna viongozi wachawi serikalini. Akataja majina viongozi wakuu wastaafu na wengine waliokuwa madarakani. Akakamatwa tena. Akashtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu viongozi kuwa wachawi. Akapatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 6 gerezani.

Akiwa gerezani akakata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kahama. Lakini mwaka 2024 Mahakama Kuu ikatupilia mbali rufaa yake. Hakuridhika, akakata rufaa Mahakama ya Rufaa. Tar.09 March 2026 Mahakama ya Rufaa imekubali rufaa yake na imemwachia huru kwa kuwa Jamhuri haikuweza kudhibitisha kuwa viongozi hao si wachawi na pia serikali haiamini katika ushirikina.

Kisandu akiwa amebakiza miezi michache amalize kifungo chake cha miaka 6, anashinda rufaa na kuachiwa huru. Baraka Mpenja anasema “dakika za jioooooooooni”.

Swali kwa Mawakili wasomi: Hii imekaaje? Yaani unafungwa kimakosa na unatumikia kifungo, halafu wakati unakaribia kumaliza ndipo mahakama inasema ulifungwa kimakosa. Je, hawezi kudai fidia akalipwa kwa kupotezewa muda? Kwa nchi zilizoendelea kama Marekani hilo linawezekana kabisa na atalipwa mabilioni ya pesa. Je kwa nchi zetu za dunia ya 3 hali ikoje? Inawezekana kudai fidia au ndo huwezi kushindana na serikali? 🤷‍♂️

ANDIKO HILI NIMELITOA KWENYE UKURASA WA FACEBOOK WA GODLISTEN G
 
Lakini kwa jinsi nifikiriavyo mimi, huyu bwana Civilian Coin kidogo dishi limeyumba.

Nina mashaka ikiwa mahakama haikung'amua hilo kwamba mshitakiwa alitakiwa afanyiwe vipimo vya akili kwanza kabla ya kuendelea na kesi...
Au walitii maagizo kutoka juu wakaamua kumtwanga nyundo miaka 6?
 
Mnamkumbuka huyu jamaa? Anaitwa Deogratius Kisandu. Aliwahi kuwa Katibu wa BAVICHA mkoa wa Tanga, mgombea ubunge jimbo la Lushoto kupitia Chadema. Baadae akahamia NCCR Mageuzi na kuwa Msaidizi binafsi (PA) wa Mwenyekiti Mbatia, kisha akawa Katibu Mwenezi wa chama hicho taifa.

Mwaka 2018 alikamatwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo mtandaoni. Akashtakiwa na kupatikana na hatia. Akafungwa miaka miwili. Akatumikia kifungo chake gereza la Butimba Mwanza kwa mwaka mmoja na kwenda kumalizia adhabu gereza la Kitengule Kagera.

Alipotoka tu, akarudi mtandaoni na kuandika kuwa kuna viongozi wachawi serikalini. Akataja majina viongozi wakuu wastaafu na wengine waliokuwa madarakani. Akakamatwa tena. Akashtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu viongozi kuwa wachawi. Akapatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 6 gerezani.

Akiwa gerezani akakata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kahama. Lakini mwaka 2024 Mahakama Kuu ikatupilia mbali rufaa yake. Hakuridhika, akakata rufaa Mahakama ya Rufaa. Tar.09 March 2026 Mahakama ya Rufaa imekubali rufaa yake na imemwachia huru kwa kuwa Jamhuri haikuweza kudhibitisha kuwa viongozi hao si wachawi na pia serikali haiamini katika ushirikina.

Kisandu akiwa amebakiza miezi michache amalize kifungo chake cha miaka 6, anashinda rufaa na kuachiwa huru. Pascal Kabombe anasema “dakika za jioooooooooni”.

Swali kwa Mawakili wasomi: Hii imekaaje? Yaani unafungwa kimakosa na unatumikia kifungo, halafu wakati unakaribia kumaliza ndipo mahakama inasema ulifungwa kimakosa. Je, hawezi kudai fidia akalipwa kwa kupotezewa muda? Kwa nchi zilizoendelea kama Marekani hilo linawezekana kabisa na atalipwa mabilioni ya pesa. Je kwa nchi zetu za dunia ya 3 hali ikoje? Inawezekana kudai fidia au ndo huwezi kushindana na serikali?

Source: Facebook page ya GJ Malisa
 
Attachments

  • FB_IMG_1773754719691.jpg
    FB_IMG_1773754719691.jpg
    59 KB · Views: 16
Anaandika G. MALISA

Mnamkumbuka huyu jamaa? Anaitwa Deogratius Kisandu. Aliwahi kuwa Katibu wa BAVICHA mkoa wa Tanga, mgombea ubunge jimbo la Lushoto kupitia Chadema. Baadae akahamia NCCR Mageuzi na kuwa Msaidizi binafsi (PA) wa Mwenyekiti Mbatia, kisha akawa Katibu Mwenezi wa chama hicho taifa.

Mwaka 2018 alikamatwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo mtandaoni. Akashtakiwa na kupatikana na hatia. Akafungwa miaka miwili. Akatumikia kifungo chake gereza la Butimba Mwanza kwa mwaka mmoja na kwenda kumalizia adhabu gereza la Kitengule Kagera.

Alipotoka tu, akarudi mtandaoni na kuandika kuwa kuna viongozi wachawi serikalini. Akataja majina viongozi wakuu wastaafu na wengine waliokuwa madarakani. Akakamatwa tena. Akashtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu viongozi kuwa wachawi. Akapatikana na hatia na kuhukumiwa miaka 6 gerezani.

Akiwa gerezani akakata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kahama. Lakini mwaka 2024 Mahakama Kuu ikatupilia mbali rufaa yake. Hakuridhika, akakata rufaa Mahakama ya Rufaa. Tar.09 March 2026 Mahakama ya Rufaa imekubali rufaa yake na imemwachia huru kwa kuwa Jamhuri haikuweza kudhibitisha kuwa viongozi hao si wachawi na pia serikali haiamini katika ushirikina.

Kisandu akiwa amebakiza miezi michache amalize kifungo chake cha miaka 6, anashinda rufaa na kuachiwa huru. Pascal Kabombe anasema “dakika za jioooooooooni”.

Swali kwa Mawakili wasomi: Hii imekaaje? Yaani unafungwa kimakosa na unatumikia kifungo, halafu wakati unakaribia kumaliza ndipo mahakama inasema ulifungwa kimakosa. Je, hawezi kudai fidia akalipwa kwa kupotezewa muda? Kwa nchi zilizoendelea kama Marekani hilo linawezekana kabisa na atalipwa mabilioni ya pesa. Je kwa nchi zetu za dunia ya 3 hali ikoje? Inawezekana kudai fidia au ndo huwezi kushindana na serikali? 🤷‍♂️
 
Rufaa imekubali rufaa yake na imemwachia huru kwa kuwa Jamhuri haikuweza kudhibitisha kuwa viongozi hao si wachawi na pia serikali haiamini katika ushirikina.

Mimi nipo hapa. Hii kitu naiona kama ushahidi kwamba mahakama zetu ni hopeless, zinahukumu kimihemko na mapenzi yao kwa wanasiasa badala ya facts. Sasa imagine mahakama kuu iliona hili ni kosa
 
Back
Top Bottom