Mahakama ya Rufani Tanzania ina Majaji 31 wakati Supreme court ya Marekani ina majaji 9 tu. Tutaendelea kukopa madeni kwa sana!

Status
Not open for further replies.
He mfumo wa Sheria wa Marekani unafanana na wa kwetu? Kesi zikilundikana mnalalamika, ikiongezwa nguvu kazi mnalalamika!
 
Kwa hili nadhani alipotea njia. Mshahara wa Jaji ni M 7+ kwa mwezi, anashindwa vipi kwenda Africa Kusini kwa mapumziko wakati nauli ya kufika huko ni around 1M tena kwa ndege?. Zaidi wengine hata kabla ya ujaji walikuwa na fedha zao nyingi tu na wamekuwa wakienda holidays hata nje ya nchi?.
 
Mh Rais hawezi kuongea kitu ambacho hana uhakika, kauli ya marehemu ilimanisha kitu fulani ambacho hakukisema wazi wazi
 
Kazi ipo......basi tuongeze wawe 100
Bajeti mkuu.

Kila mara wanalia hakuna hela.

Lakini watu wanateseka mno haki zao zinacheleweshwa.

Sasa kwa mfano kutokana na wingi wa kesi.

Ukipeleka mwaka huu 2024 utakuja kuitwa 2026.

Serikali ijitahidi tu kuwaongeza ongeza.
 
31 wote na bado rufaa haziamuliwi kwa wakati. Hivi wana nini cha kujifunza toka kwa wenzao 9 huko usa au mpaka waende study tour?
 
Hata hawa waliopo hawatoshi... Tanzania sio ajabu kesi kukaa miaka 10 mahakamani kisa ukosefu wa majaji... siku ukipata kesi inayohitaji mahakama kuu au rufaa ndio utaelewa
 
Denmark Ina wabunge 179 tu wakati Tanzania mpokeaji mkubwa wa misaada toka DANIDA Ina wabunge 395.
 
Denmark Ina wabunge 179 tu wakati Tanzania mpokeaji mkubwa wa misaada toka DANIDA Ina wabunge 395.
View attachment 3012557
Hapo napingana na wewe mkuu,

Denmark ina watu milioni 6 na ukubwa wa kilometa za mraba 42,000.

Tanzania tupo milioni 60 na nchi ina ukubwa wa kilometa za mraba laki tisa.

Hivyo kwenye swala la wabunge bado hatujaharibu sana ni haki kabisa.

Kwani kwa Denmark kila mbunge anawakilisha wastani wa watu elfu 35 ,

Wakati kwa Tanzania kila mbunge anawakilisha watu almost laki mbili.
 
Kiwango cha bajeti ya serikali ya Tanzakiza,kinakwenda kwenye matumizi ya kifahari naya kijinga.

Serikali hutumii 500b kila mwaka kununua magari ya kifahari.
 
Hapo napingana na wewe mkuu,

Denmark ina watu milioni 6 na ukubwa wa kilometa za mraba 42,000.

Tanzania tupo milioni 60 na nchi ina ukubwa wa kilometa za mraba laki tisa.

Hivyo kwenye swala la wabunge bado hatujaharibu sana ni haki kabisa.
Mkuu hizi huwa ni porojo za hawa watoa misaada ili waendelee kutuzamisha zaidi. Na ni porojo za wala mema ya nchi ili waendelee kupeana vyeo.

Zanzibar kuna majimbo yana ukubwa sawa na Kijiji na wapiga kura wasiozidi 2000, humo humo kuna mwakilishi. Kwahiyo Jimbo lenye wapiga kura 2000 lina wabunge 2. Bado kuna masheha (madiwani), rais wa JMT na rais wa baraza la mapinduz wote wanaangalia hapo Mbona Zanzibar haijapiga hatua na kuwa kama Dabai?


Kwa maoni yangu tulipaswa kupunguza ukubwa wa matumizi ya serikali kwa kuwa na wabunge 60 tu. Kwasabb hawa wabunge siyo kweli kwamba wanaonana na mwananchi mmoja mmoja
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…