Mahakama ya Tanzania inatukera watanzania

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Mahakama ya Tanzania ni mali ya watanzania inayohudumiwa na watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote kama ilivyo kwa Serikali na Bunge. Serikali, Bunge na mahakama ni mihimili ambayo lazima ionekane ikifanyakazi ya kulinda usatawi wa watanzania na mali za watanzania wote kama taifa kabla ya kufanyakazi ya kulinda ustawi wa mtu mmojammoja au kikundi. Kama kuna kifungu kwenye Katiba au sheria ambayo hailindi maslahi ya watanzania dhidi ya maslahi ya mtu au kikundi basi kifungu hicho au sheria hiyo haina budi kufutwa.

Majaji na mahakimu ni watanzania wenzetu ambao tumezaliwa, kukua, kulelewa, kusoma na kuishi nao majumbani na mitaani kabla hawajakuwa mahakimu na Majaji wa mahakama zetu. Hivyo, wanazijua pia mila, utamaduni, desturi na taratibu zetu.

Tanzania inayo Katiba halali ya mwaka 1977 na Sheria zake hata kama baadhi ya watanzania wanaziona zina mapungufu ya hapa na pale lakini Katiba ipo na sheria zipo na zinatumika hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na watanzania wenyewe. Watanzania hatutegemei tumuone mtanzania mwenzetu au kikundi tu cha watu fulani wakiibeza Katiba yetu au sheria zetu bila kupewa adhabu bila kuchelewa pale ushahidi wa kufanya hivyo utakapokuwa wazi pasipokuwa na mashaka ili kutufundisha watanzania umuhimu wa kuheshimu na kutii bila shuruti Katiba na sheria zetu.

Majaji na mahakimu kama watanzania wengine walikuwepo nchini wakati mtu na kundi lake wakijipa kura ya veto kupoka mamlaka ya watanzania 65m kulazimisha Katiba ya watanzania wote ibadilishwe vifungu la sivyo uchaguzi Mkuu wa Kikatiba watauzuia usifanyike, na kweli walifanya hivyo kwa kusababisha usumbufu kwa watanzania waliokwenda kupiga kura na waliotaka kwenda kupiga kura na kuharibu mali za watanzania vikiwemo vituo vya kupigia kura na kuwapiga waliopiga kura. Mali zilizochomwa zipo, zinafahamika na mabaki na majivu yapo hata sasa.

Bahati nzuri au mbaya Watanzania na Majaji tulikuwepo wote wakati kundi likigomea takwa la kikanuni la uchaguzi la kutia saini kanuni za uchaguzi na kukataza wagombea wao wasishiriki zoezi la kuchagua na kuchaguliwa kwenye zoezi la kikatiba la uchaguzi Mkuu 2025. Wote tulikuwepo na tuliwasikia wakisema wataasi, na kweli waliasi wakachoma mali za watanzania bila kujali chochote hadi kusababisha watanzania wenzetu kuumia, kufa na kupoteza mali zao na kuharibiwa kwa miondombinu ya umma na wenzetu wachache. Mpaka sasa watanzania kuna huduma wanazikosa kwasababu ya kuharibiwa na watu wachache kwa kisingizio kuwa wanadai haki zao.

Maswali ni:

1. kwanini kesi ya watu waliovunja Katiba na sheria za nchi mbele ya macho na masikio ya watanzania wakiwemo majaji ichukue muda mrefu kutoa hukumu wakati kila kitu kinafahamika?

2. Kwanini rasilimali watu, fedha na muda wa watanzania ziendelee kupotea kugharamia kesi ambayo ushahidi wake uko bayana?

3. Kwanini mahakama isitumie sheria pamoja na elimu, uelewa, hekima, busara uzoefu, utanzania, uzalendo, mila, desturi na utamaduni wetu kusimama na watanzania waliowengi kulinda Katiba, sheria, mali na maslahi ya watanzania badala ya kuhangaika na technicalities za kisheria?. Yaani watanzania wanapokwa haki zao na wachache kwa kutumia technicalities tu?

Mahakama iwatendee VIZURI watanzania kuliko mtu au kundi, na Kitu kizuri ni kile chenye manufaa kwa watu wengi zaidi. Do Good; Good is Good by itself.

Mahakama inataka kutuambia sisi watanzania na vijana wa taifa hili kuwa

1. kuzuia uchaguzi wa Kikatiba usifanyike sio kosa?,
2. watu wachache wanaweza kulazimisha Katiba ibadilishwe kwa nguvu?,
3. kuchoma moto vituo vya kupigia kura, barabara, sheli, ofisi za serikali ya mitaa, mahakama, vituo vya polisi, nk sio kosa kama ulivichoma wakati ukiwa umekasirika kutokana kunyimwa au kucheleweshewa haki yako?
4. Technicalities za kisheria zinaweza kupoteza haki ya umma mzima/Taifa?. Mfano, Tanzania inaweza kuchukuliwa na Malawi kwa kutumia technicalities za kisheria?

Sisi watanzania laymen wa sheria tunaona kama vile Mahakama inapaswa kuwa upande walioko watanzania wote kututetea dhidi ya mtu au kikundi. Lakini pia ituonee huruma kodi zetu kutumika kuendesha kesi kwa muda mrefu bila sababu wakati kila kitu kiko wazi. Hata magofu na majivu ya mali zilizoharibiwa bado zipo, watu wanaokosa hudumia kwa kuharibiwa ofisi na miundombinu bado wapo, shida ni nini?
 
Umeandika kwa maarifa makubwa sana.
Kuna watu watafurahia kumbe umewaponda na wengine watakasirika kumbe umewasemea.
 
Gentleman,
mahakama huru za Tanzania na kote ulimwenguni, hutekeleza majukumu yake kwa uhuru na kwakuzingatia kanuni na taratibu za kimahakama, lakini pia kwa kuzingatia sheria na katiba ya nchi.

Mahakimu na majaji hawatumii hisia kufikia hitimisho la kesi zunazopelekwa mbele yao, wala hawashinikizwi na mihemko, mayowe au matakwa ya watuhumiwa, mawakili wao au wafuasi wao, bali huzungatia ushahidi usio na shaka dhidi ya mashaka kufikia hitimisho la kesi.

Nadhani ni muhimu sana kuzipatia nafasi, muda na uhuru mahakakama zetu, na kuwapa fursa mahakimu na majaja muda wa kutosha kushughulikia mashauri yanayowasilishwa mbele yao, kuliko kutumia hisia kulalamika au kulaumu 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mahakama inayokwenda kinyume ma maslahi ya umma ni mahakama corrupt, iliyonunuliwa. Yaani mahakama impe haki mtu aliyetia sumu kisima kwasababu anamkasirikia mwenyekiti wa kijiji. Hebu acha utoto.
 
Mavi ya mama? Yananukia?
 
Naona una wakumbusha wamtendee haki Lissu waendeshe kesi haraka aachiliwe.
Tunajua hana kosa atashinda kesi.
Kama kwa kumwachia huru ni kwa maslahi ya umma na taifa basi wafanye hivyo haraka. Tusipoteze hela zetu nyingi kuendesha kesi, pesa ambayo ingeweza kununua nguzo za umeme 10,000,000 kusambaza umeme vitongojini inatumika kuendeshea kesi ambayo kila mtu anaifahamu. Sio haki kwa Taifa.
 
Mavi ya mama ???
 
Mahakama ya Tanzania ni mali ya watanzania inayohudumiwa na watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote kama ilivyo kwa Serikali na Bunge. Serikali, Bunge na mahakama ni mihimili ambayo lazima ionekane ikifanyakazi ya kulinda usatawi wa watanzania na mali za watanzania wote kama taifa kabla ya kufanyakazi ya kulinda ustawi wa mtu mmojammoja au kikundi. Kama kuna kifungu cha katiba au sheria ambayo hailindi maslahi ya watanzania dhidi ya maslahi ya mtu au kikundi kifungu hicho au sheria hiyo haina budi kufutwa.

Majaji na mahakimu ni watanzania wenzetu ambao tumezaliwa, kukua, kulelewa, kusoma na kuishi nao majumbani na mitaani kabla hawajakuwa mahakimu na majaji wa mahakama zetu. Hivyo, wanazijua mila, utamaduni, desturi na taratibu zetu.

Tanzania inayo Katiba halali ya mwaka 1977 na Sheria zake hata kama baadhi ya watanzania wanaziona zina mapungufu ya hapa na pale lakini katiba na sheria zipo na zinatumika hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Watanzania hatutegemei tumuone mtanzania mwenzetu au kikundi tu cha watu fulani wakiibeza Katiba yetu au sheria zetu bila kupewa adhabu bila kuchelewa pale ushahidi wa kufanya hivyo utakapokuwa wazi pasipokuwa na mashaka ili kutufundisha watanzania umuhimu wa kuheshimu katiba na sheria zetu.

Majaji na mahakimu kama watanzania wengine walikuwepo nchini wakati mtu na kundi lake wakijipa kura ya veto na kupoka mamlaka ya watanzania 65m kulazimisha Katiba ya watanzania wote ibadilishwe vifungu la sivyo uchaguzi Mkuu wa Kikatiba watauzuia usifanyike, na kweli walifanya hivyo kwa kusababisha usumbufu kwa watanzania waliokwenda kupiga kura na waliotaka kwenda kupiga kura na kuharibu mali za watanzania vikiwemo vituo vya kupigia kura na kupiga waliopiga kura.

Watanzania na majaji tulikuwepo wote wakati kundi likigomea takwa la kinanuni za uchaguzi la kutia saini kanuni za uchaguzi na kukataza wagombea wao wasishiriki zoezi la kuchagua na kuchaguliwa kwenye zoezi la kikatiba la uchaguzi. Wote tulikuwepo na kuwasikia wakisema wataasi na kweli waliasi wakachoma mali za watanzania bila kujali chochote hadi kusababisha watanzania wenzetu kuumia, kufa na kupoteza mali zao na kuharibiwa kwa miondombinu ya umma na wenzetu wachache.

Maswali ni kwanini kesi ya watu waliovunja Katiba na sheria za nchi mbele ya macho na masikio ya watanzania wakiwemo majaji ichukue muda mrefu kutoa hukumu wakati kila kitu kinafahamika?

Kwanini rasilimali watu, fedha na muda wa watanzania ziendelee kupotea kugharamia kesi ambayo ushahidi wake uko bayana?

Kwanini mahakama isitumie sheria pamoja na elimu, uelewa, hekima, busara uzoefu, utanzania, uzalendo kusimama na watanzania waliowengi kulinda Katiba, sheria, mali na maslahi ya watanzania badala ya kuhangaika na technicalities za kisheria?. Yaani watanzania wanapokwa haki zao na wachache kwa kutumia technicalities tu? Mahakama iwatendee VIZURI watanzania kuliko mtu au kundi, na Kitu kizuri ni kile chenye manufaa kwa watu wengi zaidi. Do Good; Good is Good by itself.

Mahakama inataka kutuambia sisi watanzania na vijana wa taifa hili kuwa

1. kuzuia uchaguzi sio kosa?,
2. watu wachache wanaweza kulazimisha Katiba ibadilishwe kwa nguvu?,
3. kuchoma moto vituo vya kupigia kura, barabara, sheli, ofisi za serikali ya mitaa, mahakama, vituo vya polisi, nk sio kosa kama ulivichoma wakati ukiwa umekasirika kutokana kunyimwa au kucheleweshewa haki yako?
4. Technicalities za kisheria zinaweza kupoteza haki ya umma mzima/Taifa?. Mfano, Tanzania inaweza kuchukuliwa na Malawi kwa kutumia technicalities za kisheria?

Sisi watanzania laymen wa sheria tunaona kama vile Mahakama inapaswa kuwa upande walioko watanzania wote except mtu/kikundi kututetea. Lakini pia ituonee huruma kodi zetu kutumika kuendesha kesi kwa muda mrefu bila sababu wakati kila kitu kiko wazi.
Ng’ombe wa mama bakini zizini ili msije mkaishia kuvamia na kuharibu mazao kwenye shamba la mfugaji wenu.

Tanzania ingekuwa na mahakama, mfugaji wenu angekuwa anafanya biashara ya mamantilie Kizimkazi au angekuwa nyuma ya nondo siku nyingi.
 
You utter nonsense! Ni kifungu kipi cha katiba na sheria kinachosema kuwa kupingq uchaguzi ni kosa?
Acha kujipa umuhimu usiokuwa nao na kujifanya mjuvi wa sheria usizozijua. Au wewe ni Katuga?
Taja vifungu kama kweli unavijua!
 
Mahakama lazima ihudumie taifa sio kakikundi ka wahuni kanakobeba makapu ya makaratasi kukwepa kutiwa hatiani huku mali za umma zikiwa zimechomwa moto. Mahaka ya Tanzania lazima itoe onyo kali kwa wengine waliokuwa wanawaza kwenda kuichoma hata Mahakama Kuu yenyewe. Kama itawaachia huru itakuwa imeseti presidency mbaya sana kwa taifa na dunia.
 
You utter nonsense! Ni kifungu kipi cha katiba na sheria kinachosema kuwa kupingq uchaguzi ni kosa?
Acha kujipa umuhimu usiokuwa nao na kujifanya mjuvi wa sheria usizozijua. Au wewe ni Katuga?
Taja vifungu kama kweli unavijua!
Ndio hizo technicalities za kipuuzi ambazo mahakama lazima izidisregard. Uchaguzi wa kila baada ya miaka 5 ni wakikatiba, kuuzuia ni kuivunja Katiba na kuzuia nchi isiwe na Kiongozi na viongozi. Maana yake kama uchaguzi usingefanyika Rais aliyeko angekosea kuendelea kuwepo madarakani kikatiba. Unadhani sisi ni maboya wa kiasi hicho?

Mahakama ikicheza nao next step watachoma mahakama ya rufaa.
 
Back
Top Bottom