Mahakama ya Tanzania ni mali ya watanzania inayohudumiwa na watanzania wote kwa manufaa ya watanzania wote kama ilivyo kwa Serikali na Bunge. Serikali, Bunge na mahakama ni mihimili ambayo lazima ionekane ikifanyakazi ya kulinda usatawi wa watanzania na mali za watanzania wote kama taifa kabla ya kufanyakazi ya kulinda ustawi wa mtu mmojammoja au kikundi. Kama kuna kifungu cha katiba au sheria ambayo hailindi maslahi ya watanzania dhidi ya maslahi ya mtu au kikundi kifungu hicho au sheria hiyo haina budi kufutwa.
Majaji na mahakimu ni watanzania wenzetu ambao tumezaliwa, kukua, kulelewa, kusoma na kuishi nao majumbani na mitaani kabla hawajakuwa mahakimu na majaji wa mahakama zetu. Hivyo, wanazijua mila, utamaduni, desturi na taratibu zetu.
Tanzania inayo Katiba halali ya mwaka 1977 na Sheria zake hata kama baadhi ya watanzania wanaziona zina mapungufu ya hapa na pale lakini katiba na sheria zipo na zinatumika hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Watanzania hatutegemei tumuone mtanzania mwenzetu au kikundi tu cha watu fulani wakiibeza Katiba yetu au sheria zetu bila kupewa adhabu bila kuchelewa pale ushahidi wa kufanya hivyo utakapokuwa wazi pasipokuwa na mashaka ili kutufundisha watanzania umuhimu wa kuheshimu katiba na sheria zetu.
Majaji na mahakimu kama watanzania wengine walikuwepo nchini wakati mtu na kundi lake wakijipa kura ya veto na kupoka mamlaka ya watanzania 65m kulazimisha Katiba ya watanzania wote ibadilishwe vifungu la sivyo uchaguzi Mkuu wa Kikatiba watauzuia usifanyike, na kweli walifanya hivyo kwa kusababisha usumbufu kwa watanzania waliokwenda kupiga kura na waliotaka kwenda kupiga kura na kuharibu mali za watanzania vikiwemo vituo vya kupigia kura na kupiga waliopiga kura.
Watanzania na majaji tulikuwepo wote wakati kundi likigomea takwa la kinanuni za uchaguzi la kutia saini kanuni za uchaguzi na kukataza wagombea wao wasishiriki zoezi la kuchagua na kuchaguliwa kwenye zoezi la kikatiba la uchaguzi. Wote tulikuwepo na kuwasikia wakisema wataasi na kweli waliasi wakachoma mali za watanzania bila kujali chochote hadi kusababisha watanzania wenzetu kuumia, kufa na kupoteza mali zao na kuharibiwa kwa miondombinu ya umma na wenzetu wachache.
Maswali ni kwanini kesi ya watu waliovunja Katiba na sheria za nchi mbele ya macho na masikio ya watanzania wakiwemo majaji ichukue muda mrefu kutoa hukumu wakati kila kitu kinafahamika?
Kwanini rasilimali watu, fedha na muda wa watanzania ziendelee kupotea kugharamia kesi ambayo ushahidi wake uko bayana?
Kwanini mahakama isitumie sheria pamoja na elimu, uelewa, hekima, busara uzoefu, utanzania, uzalendo kusimama na watanzania waliowengi kulinda Katiba, sheria, mali na maslahi ya watanzania badala ya kuhangaika na technicalities za kisheria?. Yaani watanzania wanapokwa haki zao na wachache kwa kutumia technicalities tu? Mahakama iwatendee VIZURI watanzania kuliko mtu au kundi, na Kitu kizuri ni kile chenye manufaa kwa watu wengi zaidi. Do Good; Good is Good by itself.
Mahakama inataka kutuambia sisi watanzania na vijana wa taifa hili kuwa
1. kuzuia uchaguzi sio kosa?,
2. watu wachache wanaweza kulazimisha Katiba ibadilishwe kwa nguvu?,
3. kuchoma moto vituo vya kupigia kura, barabara, sheli, ofisi za serikali ya mitaa, mahakama, vituo vya polisi, nk sio kosa kama ulivichoma wakati ukiwa umekasirika kutokana kunyimwa au kucheleweshewa haki yako?
4. Technicalities za kisheria zinaweza kupoteza haki ya umma mzima/Taifa?. Mfano, Tanzania inaweza kuchukuliwa na Malawi kwa kutumia technicalities za kisheria?
Sisi watanzania laymen wa sheria tunaona kama vile Mahakama inapaswa kuwa upande walioko watanzania wote except mtu/kikundi kututetea. Lakini pia ituonee huruma kodi zetu kutumika kuendesha kesi kwa muda mrefu bila sababu wakati kila kitu kiko wazi.