Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).

Ni dhahiri huyu muhanga hawezi kulipa hizo faini. Je hukumu kwa kawaida ikitoa adhabu ya faini pia husema iwapo mshitakiwa atashindwa kulipa huwa kuna option ya kutumikia kifungo! Je hukumu hizo zote mbili dhidi ya Musiba hazizungumzii hiyo option ya kutumikia kifungo kwa huyu kiumbe?
 
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Anaamika ndiyo maana anaweza kuwa na madeni ya namna hii!!! Lazima tujaribu kutafuta vimelea vya uchanya kwenye kila jambo badala ya uhasi ili kupunguza uwezekano wa kusononeka! Tupo pamoja?
 
Mahakama Kuu ya Tanzania, imemuamuru Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kumlipa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kiasi cha Sh.Bilioni 6 kama fidia ya kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.

Hukumu hiyo ni ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018 na imetolewa na Jaji Joacquine De Mello ambapo amesema mbali na mambo mengine Musiba amlipe Sh.Bilioni 6 Membe, pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.

Mahakama imesema Sh.Bilioni 5 ni fidia ya hasara halisi na Sh. Bilioni 1 hasara ya jumla, katika kesi hiyo Membe alimshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo aliwadai Sh. Bilioni 10 kwa kumchafua.

Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.
#MillardAyoMAHAKAMANI
 
M
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Mama tibaijuka nae ana tuzo dhidi ya musiba
 
Kwa waliokuwa wanamtuma kupaza sauti za matusi...😁😁
Wanamkimbia...CCM wahuni sana, wanakutumia na kukupamba, ukitokea msala wote wanakukimbia wanakuacha peke yako, wao wanaenda kuimba mapambio kwa mwenye mpini wakati huo!

Tha same thing kinamtokea Sabaya, alikuwa na marafiki kila kona huko CCM, kwa sasa wote kimyaa, hakuna hata mmoja anainua mdomo kumzungumzia!

Ndicho kinachomtokea/kitamtokea Bashite, kuna watu wanasema eti anasiri za viongozi wengi hagusiki, CCM dont give a shit, wakiamua kukuchinjia baharini wanakuchinja mchana kweupe hata bila ya chembe la aibu
 
Mahakama kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya kesi ya kuchafuliwa jina iliyokuwa ikimkabili mkurugenzi mkuu wa gazeti la Tanzanite na mwanaharakati huru, ndugu Musiba dhidi ya aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo, ndugu Bernard Membe. Mahakama hiyo imemtaka Musiba kulipa kiasi hicho cha pesa.
Jiwe amewaponza wengi!
 
Back
Top Bottom