Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh. bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe

Duuh... Kaazi kweli kweli. Watu wa Magufuli tunazidi kuumizwa.
 
Nauliza kwa sauti. Je mahakama yetu inatenda haki? Au ndio kwa mujibu wa chama?
 
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
Bado Tibaijuka naye alipewa tuzo alipwe 80m. Huyu wadai waombe afungwe miaka kadhaa na wamlipie gharama za jela (civil prisoner)
 
Unapo kazi a hukumu kuna option Tatu. Ya kwanza mdaiwa alipe mwenyewe ya pili kukamata Mali zake na kunadi na ya Tatu kumuweka ndani kama mfungwa wa madai mpaka atakapo Lipa. Thus hio option ya kumuweka ndani ipo kwenye kesi zote 2

Je unapomuweka ndani jela mdaiwa kwenye hiyo option , mdai ndio anamgharamia mfungwa?
 
Sisi kama CDM tunasema tunakwenda na membe,mwenyekiti asubiri kwanza[emoji38][emoji38][emoji38]

Mnapigwa kimbwa mbwa sana.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa hiyo huyu mwamba kwa sasa ana madeni yapatayo 13bilion! Manake kule kuna shangazi Fatuma alipata tuzo ya 7b na huku Membe 6b. Nadhani sasa Musiba ni raia anayedaiwa madeni makubwa kuliko raia yeyote hapa nchini na anastahili sifa ya Highly Indebted Poor Person (HIPC).
 
Musiba ni kichwa hao wanafurahisha genge tu...hawapati hata sh kumi yake na jela hakai... jifunzeni sheria bavicha msipende sna kuwkea nguvu kwenye povu
Ala, kwa hiyo mahakama imekosea au? Mh.mwanasheria msomi hebu tuambia kitatokea nn iwapo hatoweza kuwalipa?
 
Mfilisi huyo mjinga mpenda sifa asiyejitambua
Wala wasimfunge.Wafilisi mali zote na deni halitoisha wanasubiri kila akipata mali nyingi e wanachukua tena.Ili huyu Musiba maskini wa fikra abaki maskini wa kipato maisha.Na msiba wake hakika hautoisha.Au ajishushe awaombe msamaha wahusika na uma wa Wa Tanzania tulochikizwa na wazimu wake.
 
Ni dhahiri hataweza kulipa hiyo faini, kwa hiyo itakuwaje? wanasheria hebu saidieni

1. Atapewa muda wa kulipa cash.

2. Kama pesa hana, mali zake za kampuni (gazeti la Tanzanite) zitakuwa attached kisheria na kuuzwa kwa mnada halali publicly kwa order ya Mahakama, ili kulipa pesa yote husika.

3. Kama hana mali yoyote ya kukamata, ama mali zake husika hazitoshi kulipa dai lote, basi hapo mdai anakuwa na utashi (discretion) wa aina mbili: Kupokea pesa iliyopatikana (pungufu) na kumaliza kesi, ama kuridhia mdaiwa apelekwe jela kwa gharama za mdai mwenyewe. Civil prisoner. Yaani mfano mdaiwa akafungwa jela (civil prisoner) kwa miaka mitatu. Yule mdai atalipia gharama zote za mfungwa kwa miaka hiyo mitatu. Yaani mdai utalipia ili mdaiwa wako apelekwe gerezani kwasababu hana mali yoyote ya kulipa. Afisa magereza anaitaarifu Mahakama kuwa mfungwa mmoja anatumia gharama shilingi ngapi kwa siku kuwa gherezani. Kisha wanapiga calculation, mdai unalipia na risiti ya serikali unapewa, kisha mdaiwa wako anapelekwa 'ngome'.

-Kaveli-
 
Musiba hana hela ya kulipa huyu mbwa. Membe awe anamkaza nyoro kwa wiki Mara 2 mpaka mwisho wa maisha yake
 
Mahakama kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya kesi ya kuchafuliwa jina iliyokuwa ikimkabili mkurugenzi mkuu wa gazeti la Tanzanite na mwanaharakati huru, ndugu Musiba dhidi ya aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, ndugu Bernard Membe. Mahakama hiyo imemtaka Musiba kulipa kiasi hicho cha pesa.

==========

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya Sh6 bilioni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 28,2021 na Jaji Joacquine De Mello aliyeisikiliza kesi hiyo.

Katika hukumu hiyo Musiba ametakiwa kumlipa Membe kiasi hicho cha fedha pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka miwili.

Pia imeweka zuio la kudumu kwa Musiba la kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.

Mwananchi

Pia, soma=> Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu
Yani hukumu kama huzi huwa za kisiasa sana

Wewe unamwambia mtu alipe 6B na hali unajua hawezi kabisa sasa unahukumu ili iweje??
 
Huyu mwendawazimu ndio aliwahi kusema atamfunga Mbowe miaka 200. qumamaye.
 
Atakwambia haitambui hiyo mahakama....
Thubutuuu haitambui mahakama yeye kama nani?! La msingi hapa ni yeye kuwa mpole na pengine kuomba msamaha. Sijui katika hali hii akiomba msamaha kuna tija yoyote. Nifahamisheni wakuu
 
shilingi imegeuka upande wa pili., nadhan hapa wale wanaotumwa kufanya kila kitu watakuwa wamejifunza jambo
 
Back
Top Bottom