Pre GE2025 Mahakama yaamuru Dkt. Slaa kufikishwa Kisutu Machi 4 ili kutolewe uamuzi wa kesi inayomkabili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kutolewa kwa amri ya Mwanasiasa Mkongwe, Dkt. Wibroad Slaa (76) kufikishwa mahakamani ifikapo Machi 4, mwaka huu ili uweze kutolewa uamuzi wa kesi hiyo itakuwa inasikilizwa kwa njia gani.

Uamuzi huo ulitolewa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo.
DKT SLAA.jpg
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema alidai kuwa shauri hilo lilipelekwa kwa ajili ya kutajwa na kueleza kuwa kwa kuwa shauri hilo lipo katika taratibu nyingine za kirufaa zinaendelea katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya shauri hilo kutajwa.

Rufaa katika kesi hiyo ilikatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka juu ya uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam wa kuamuru shauri namba 993/2025 kurudishwa mahakamani hapo ili liweze kutolewa uamuzi juu ya dhamana ya Dkt. Slaa ambayo hapo awali iliwekewa pingamizi na upande wa mashitaka.

Soma, Pia: Dkt. Slaa kurejea Mahakamani Kisutu leo, Mbivu, mbichi kesi ya kusambaza uongo kujulikana

Baada ya Mrema kueleza hayo upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Melkion Sanga ulidai kuwa katika kikao kilichopita ilitolewa amri ili mshitakiwa aweze kufikishwa mahakamani siku ya leo na kujua mwenendo wa kesi yake inavyoendelea.

Sanga alidai kuwa kwa kuwa mshitakiwa hakufikishwa mahakamani aliiomba mahakama itoe ahirisho fupi ili aweze kufikishwa mahakamani kama ilivyoamuriwa katika kikao kilichopita, pia alidai kuwa amri ya mahakama ilivyotolewa ilitakiwa ifuatwe kwa mshitakiwa kufikishwa mahakamani hapo.

Akijibu hoja hiyo Mrema alidai kuwa kwa upande wa mashitaka hawakupokea amri ya mshitakiwa kufikishwa kutoka mahakamani ndiyo sababu walishindwa kumfikisha mshitakiwa mahakamani hapo.

Mrema alidai kuwa kwa mshitakiwa kufikishwa mahakamani hakuthibitishi afya yake ipo vipi kama alivyodai wakili wake, hivyo alidai kuwa mahakama inaweza kutoa uamuzi kwa kutoa amri mshitakiwa afikishwe mahakamani au kesi isikilizwe kwa mkutano wa njia ya video.

Chanzo: ITV Tanzania

======================
Dkt. Slaa hajafikishwa Mahakamani kesi yasogezwa mbele mpaka Machi 4, 2025

Dkt. Willbroad Slaa (76) anayekabiliwa na kesi Namba 993/2025 hajafikishwa mahakamani licha ya kutolewa kwa amri ya kufanya hivyo iliyowataka upande wa mashtaka kumleta mahakamani.

Kesi hiyo inayosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuja kwa ajili ya kutajwa leo February 19, 2025 lakini imeshindwa kuendelea kutokana na uwepo rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa kuhusu suala la dhamana.

Hata hivyo baada ya kuona mshtakiwa hajafikishwa Mahakamani, Mawakili wa upande wa utetezi kupitia Melikior Sanga wamehoji juu ya utekelezwaji wa maagizo ya Mahakama kuhusu kumleta mahakamani Dkt. Slaa, ambapo wamesisitiza kwamba ni haki mteja wao kuwepo Mahakamani wakati shauri lake linatajwa.

Upande wa Jamhuri umejibu hoja hiyo ukidai kuwa licha ya maelekezo ya Mahakama kuhusu kutakiwa kumleta mtuhumiwa Mahakamani, wamedai kuwa bado hawajapokea oda ya Mahakama ili waweze kutekeleza hilo.

Baada kusikiliza hoja za pande zote mbili Mahakama imeelekeza oda hiyo itolewe na kuwafikia upande wa mashtaka ili waweze kuitekeleza. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka March 4, 2025.

Itakumbukwa ni takribani siku 40 zimepita tokea Dkt. Willbroad Slaa alipotiwa kizuizini na kufunguliwa kesi ambapo wadau mbalimbali wanaotetea haki za binadamu wamekuwa wakipaza sauti na kutaka mshtakiwa apatiwe haki ya dhamana wakidai kuwa shauri linalomkabili alimkoseshi haki ya dhamana.
 
Sababu ni zilezile.

Maelekezo kutoka juu.

Uchawa unafanya vyombo vya Dola kujipendekeza Kwa kufikri wanamfurahisha mama ili Hakimu ateuliwe kua Jaji wa Mahakama KUU.

Ujinga wa kutoelewa na kutafasiri Sheria (hili liko wazi, ndio maana wanasheria wanafeli sana pale school of law ), Elimu yetu imetoka kizazi chenye Vyeti lkn kuondoa yaliyoko kwenye makaratasi kua vitendo ,imekua ngumu sana ,nadhan inachangizwa na Ukosefu wa Akili kichwan ndio maana hatujawahi kugundua chochote .

Kwenye Sheria, Mtanzania namba Moja nayemuelewa ni TUNDU LISSU.

Mtanzania akili yake huwezi ikuta Mahali popote hapa Duniani zaidi ya Tanzania tu.

Katiba MPYA, Tume huru ya Uchaguzi
 
Na hili joto la Dar, atatoka ameiva kweli, nashauri wasimruhusu anyoe ndevu, atoke amechakaa akiwa na wadudu wanamfanyia patrol.

Job Mrema, moja ya mawakili bora kabisa ambaye alipigwa fitna akahamishiwa Kagera
 
Hii mbinu imetumiwana wafungwa wengi wakisiasa duniani.

Kwa umri wake hana cha kupoteza,hakuna chakula ambacho hajawahi kula,agomee kula kwa siku tano tu

Akianza kudhoofika watamuwachia bila masharti,

Aanze aasa
 
Kwani hawa wakora wanajali basi, wao nia yao afie jela akigoma kula watafurahi anawarahisishia kazi
 
Agome afe, alipewa sukari kaamua kunywa magadi mwache ameze anachotaka.
 
Sababu ni zilezile.

Maelekezo kutoka juu.

Uchawa unafanya vyombo vya Dola kujipendekeza Kwa kufikri wanamfurahisha mama ili Hakimu ateuliwe kua Jaji wa Mahakama KUU.

Ujinga wa kutoelewa na kutafasiri Sheria (hili liko wazi, ndio maana wanasheria wanafeli sana pale school of law ), Elimu yetu imetoka kizazi chenye Vyeti lkn kuondoa yaliyoko kwenye makaratasi kua vitendo ,imekua ngumu sana ,nadhan inachangizwa na Ukosefu wa Akili kichwan ndio maana hatujawahi kugundua chochote .

Kwenye Sheria, Mtanzania namba Moja nayemuelewa ni TUNDU LISSU.

Mtanzania akili yake huwezi ikuta Mahali popote hapa Duniani zaidi ya Tanzania tu.

Katiba MPYA, Tume huru ya Uchaguzi
Utalalamikia JF hadi lini Dogo?
 
Na hili joto la Dar, atatoka ameiva kweli, nashauri wasimruhusu anyoe ndevu, atoke amechakaa akiwa na wadudu wanamfanyia patrol.

Job Mrema, moja ya mawakili bora kabisa ambaye alipigwa fitna akahamishiwa Kagera
Mahakama imesha amua , ushauri wako ni null aka hauna mashiko wala umuhimu
 
Back
Top Bottom