Hili la kukaa nje ya mahakama na kukubaliana ndilo la msingi.
Huko nyuma nilikuwa nawaambia Watu hili jambo si rahisi wanavyofikiria. Wengi walikuwa wanachangia kwa mihemko, kwamba Jack hakuchuma mali kwa hiyo akae kando Watoto wake watatunzwa na Watoto wakubwa wa Mengi.
1. Wanachosahau ni kuwa Jack ni mke halali wa Mengi (ndiyo maana katika mashauri yote hakuna mahali limepingwa)
2. Jack amezaa na Mengi watoto wawili. Watoto ambao ni haki yao kurithi mali za Baba yao ambaye ni Mzee Mengi
3. Na kwa kuwa Watoto wa Jack ni Watoto halali wa Mzee Mengi na hawajafikisha umri wa miaka 18 mnaweza kujua nani anastahili kusimamia haki zao.
Wosia uliodaiwa kuandikwa na Mengi ulitupiliwa mbali na mahakama. Kwa hiyo hapa mambo yanaanza upya ndiyo maana wakili wa Jack kaanza na kuhakikisha mali zote ambazo zilikuwa hazijagawanywa zinarudishwa pamoja halafu kesi ya mgao ianze upya. Hapa hata kama humpendi lakini huyo dada katumia mawakili wazuri.
Naona hapo la msingi wakae pamoja kwa kushirikiana na Wazee wenye busara na mgao ufanyike tu. Hata kama Jaclk hatapata kama ilivyosemwa kwenye ule wosia uliokataliwa, lakini obvious ataondoka na mgao mkubwa si haba.
Halafu sisi maskini humu JF acheni habari ya kuzungumzia kuhusu kuuliwa Jack.
Mzee Mengi hakuwa na historia ya aina hiyo. Wakati anamtongoza na kumuoa Jack, alifanya hayo yote akiwa na akili timamu na Mtu mzima. Tusitie kinyongo kwa mali zisizotuhusu.