Kama hujui sheria uliza wanaozijua wakusaidie kwa ukweli.
kisheria, hasa sheria za Mirathi kwa Tanzania, Kinachoangaliwa ni Mali alizoacha Marehemu na warithi wa Marehemu basi.
Nitatoa mfano. Mkikaa kikao cha Mirathi, cha kwanza mtajadili Mali alizoacha Marehemu na warithi wake. Sasa sifa ya warithi haitegemei umri na mchango wake kwenye mali za marehemu.
Warithi halali ,unaanza na Mke wa Marehemu, Watoto wa Marehemu na wazazi wa Marehemu. Sasa haijalishi huyo Mke umemwoa lini na ukiwa na mali kiasi gani. Kinachoangaliwa ni hadhi yake kama ni Mke wa marehemu basi.
Anaweza kuwa Mke umemuoa ndani ya mwaka mmoja na amekuta karibu mali zote umechuma mwenyewe, Ukifa anapata mgawo wake safi kama mrithi wa Marehemu....... Msichanganye mambo ya Mirathi na sheria za ndoa katika mgawanyo wa mali pale ndoa zinapovunjika.