Mahakama yakubali mshtakiwa mauaji ya mkewe apimwe Afya ya Akili

Daah roho mbaya tu hiyo na Umasikini upo kwenye damu kwani ungemtengenezea mazingira mazuri ya yeye kuendelea kuishi ungepungukiwa nini unahadithia kuchukua gari aisee...
Ungejua aliyokuwa ananifanyia na ulicho-comment hapo UNGEFUTA mara moja,na kama ningeendelea kuishi nae hakika ningekuwa natumikia Kifungo Jela, yule si Mama yangu wala damu ya ukoo wetu, hakukuwa na nafasi ya kumtengezea hayo mazingira mazuri unayoyamaanisha
 
Kesi imeisha hiyo,hapo dokta anapewa mlungura, anasema upo crazy unapelekwa sober house!! Miaka, mitatu wa bongo wameisha sahau,unarudi zako hm kula bata.

Si rahisi kama tunavyodhani.
Si suala la daktari mmoja, ni jopo la madaktari na mikutano/vikao na mijadala mirefu ya kukuhusisha na bila kukuhusisha. Pia si zoezi la siku moja.

Nenda pale Dodoma Isanga utakuta kuna watu wapo pale miaka chini ya utafiti. Kukaa mle tu ni zaidi ya jela, mazingira nk.

Ndani ya maisha mle ndani kuna taarifa zinakusanywa pia kwa room na maisha kwa ujumla. Pia, uweze ku-prove kuwa wakati unafanya hivyo ulikuwa hauko sawa na si kwamba tatizo limeanza baada ya tukio.

Mazingira ya tatizo, kabla na baada ya tukio pia yatakuhukumu sana.

Labda iwe halisia au utegemee nguvu tofauti na kuigiza. Kwani unaigiza kitu ambacho wenzako wanakitafuta na hukijui.
 
Hapo sawa
 
Mungu atuepushe na haya maamuzi magumu,watoto wanaambiwa baba yenu alimuua mama yenu dah,Hao wenye mtoto wao je?
 
Alikuwa anakuchit nn?
 
Mawakili wetu bwana,yaani mtu achukue gunia,achome mtu afukie majivu afu awe hana utimamu wa akili.
Huyo mtuhumiwa atakuwa anajifanyisha tu. Na kama ni kuchanganyikiwa, basi ni baada ya hayo mauaji. Ila kabla ya hapo, viashiria vyote vinamuonesha alikuwa na akili timamu.
 
Nakupongeza kwa hilo,oeni wanawake wacha Mungu waziombee ndoa zenu jamani,shetani akiona ndoa imetulia lazima ajipenyeze.
Mwanamke ukiishi kwa akili na mwanaume anayekupenda utakula mema ya nchi

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hii kesi jamaa atachomoka inaonekana anatembeza mpunga wa kutosha, kesi gani isiyoisha na kitu kipo wazi kabisa. Hapo majibu yanakuja ana matatizo ya akili mwisho wa siku anaachiwa huru au anahukumiwa miaka miwili au mitatu
Akikutwa na matatizo ya afya ya akili atafungwa Isanga
 
Sina hakika sana ila wataalamu mtanisaidia nilisikia mahali kuwa hapa Tanzania hamna hiko kipimo cha afya ya akili (sijajua kama kipo huko duniani kwingine)

hivyo ili kufahamu mtu afya yake ya akili , huulizwa maswali kadhaa maalum ambayo anapaswa kuyajibu then mhusika (nimuite mpimaji either Dokta au mwasaikolojia etc.)

kutokana na majibu yake kwa kutumia utaalamu lake atachakata na kuhitimisha kuwa huyu afya yake ya akili ipo timamu au ina walakini
 
Kama uliweza kuyafanya hayo yote kwa mafanikio, basi wewe ni genious upewe sifa.

Waweza kufanikisha kumtoroka mtu, lakini akakupeleleza ulikohamia na timbwili likaendelea.

Basi tuseme una uwezo wa kutunza siri zako pamoja na siri za mazingira.

Ni vigumu sana kumtoroka mtu miaka 12 ashindwe kukupata katika jiografia ya eneo moja!

Au naye alikamia muachane na utoro wako akautumia kama ni fursa?
 
Hii kesi jamaa atachomoka inaonekana anatembeza mpunga wa kutosha, kesi gani isiyoisha na kitu kipo wazi kabisa. Hapo majibu yanakuja ana matatizo ya akili mwisho wa siku anaachiwa huru au anahukumiwa miaka miwili au mitatu
Na akitoka ndugu wa mke sijui watakuwa kwenye hali gani maana

Ova
 


Mlango wa kutokea huyo, watu washapiga hela, ila ni sawa sawa tu.
 
Safi sana,ajakusumbuaga tena mkuu?hawa viumbe nuksi sana
 
Kimsingi alinipeleleza na kunifuatilia sana nia ni kutaka tugawane mali,mpaka naachane nae sikuwa hata na kiwanja maana nilikuwa naishi nyumba ya Serikali,nilivyoanza kuishi mwenyewe milango ikafunguka,nikaanza kununua viwanja na kujenga,mwaka juzi baada ya kupata taarifa ya maendeleo yangu na kupeleleza mpaka kujua baadhi ya nyumba zangu Dar akakimbilia Mahakamani kudai mgao[emoji1787][emoji1787]uzuri hizo Nyumba sikuandika majina yangu(HATI),hivyo Mahakamani amegonga mwamba,hakika yule alikuwa MWANGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…