Sasa Harmonize wakati ana-hit hivi akienda CRDB akawa business plan yake haaminiki kweli? Natolea mfano tu kwamba, nitafungua studio, nitasainisha wasanii, tutapiga show, kila mwezi tutakuwa tunaingiza milioni 30, nyie nawaletea milioni 10 zengu, basi CRDB kwakuwa hawaujui mziki wakaingia kingi!Mkopo huo ulikuwa wa Dhamana ya Ardhi (Nyumba) (Mortgage) au ni wa Nini hasa??? Dhamana au rehani aliweka assets gani ili kudhamini huo mkopo? Milioni 300 aliwezaje kukopeshwa na benki ya CRDB kiurahisi hivyo bila ya kuweka rehani mali yake yoyote ile? Ina maana kwamba alikopeshwa pesa nyingi kiasi hicho bila ya Mkopeshaji (Crdb) kujiridhisha Kwanza kuhusu uwezo wa mtu huyo wa kulipa marejesho ya deni lake???
Anyway, mkopo siyo sadaka, Mkopaji alipaswa kukopa kwa malengo.
Dawa ya deni ni kulipa.