Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

The guy is ahead of the time ana timu nzuri pia anajua destination yake ni ipi akurupuki

Naona yule jamaa atatawala hiki kiwanda cha music na maisha kwa muda mrefu Sana .

Smart
Humble
Financial intelligence
Good team work

Also the guy never get complacent -Ana njaa na MAISHA haridhiki
Mtandale hata mziki wake ukiisha ataendelea kupata hela kutoka kwenye investment alizofanya
 
Juzi nimeona hascana anasema kiboko wa wachawi aachwe afanye kazi zake kwasababu yeye kama muumini wake anakosa huduma za kiroho

Hanscana na Mwarabu Fughter wamenyang'anywa tonge mdomoni.....Hanscana alikuwa ndiyo anarecord matukio yote ya kanisani na alikuwa analipwa mpunga mzuri tu,so lazima apige makelele maana ugali umeingia mchanga.
 
Upuuzi kabisa mtu unakuta anatamba eti kazi ya ualimu ni kazi ya Laana,Sasa tangu nizaliwe sijawahi sikia mwalimu kafikishwa mahakamani Kwa kushindwa kulipa mkopo wa benki au kauziwa assets zake Kwa kushindwa kurejesha mikopo ya benki.


Sasa Harmonize kashindwa kulipa M 100,Huu upuuzi,Sitaicha kazi ya ualimu kamwe,hapa navuta Muda nije niende nikavute mpunga M 32 nione mtu ananilaumu Kwa kutegemea mikopo , nijivinjari zaidi.Asante Mungu kwa kazi ya ualimu,Kiufupi huwezi toboa maisha bila kukopa ,kama unakopesheka kopa
2047 kesho kutwa hapo. Kopa hiyo enjoy maisha
 
Sasa mwanamke kama Kajala unalala na kuamka naye hata maisha yako yakiharibika unakuwa umepoteza nini?

Kajala ni mzuri jamani sio filter wala AI. Halafu ana aibu flani makes her even more beautiful.

Ningekuwa mwanaume mimi…au basi
Wengine sisi tunaona kawaida tu
Ila kweli udongo wake mzuri

Ova
 

View attachment 3072826
View attachment 3072827

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.

Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.

Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kibiashara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.

Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.

CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.

Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755/=
Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.

Chanzo changu na mimi,

Nifah.
Kajala one and two tena zote ni range. Mwenzetu umetuma ka laki tu na bado. Unauliza chenji.
 
Back
Top Bottom