Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Upuuzi kabisa mtu unakuta anatamba eti kazi ya ualimu ni kazi ya Laana,Sasa tangu nizaliwe sijawahi sikia mwalimu kafikishwa mahakamani Kwa kushindwa kulipa mkopo wa benki au kauziwa assets zake Kwa kushindwa kurejesha mikopo ya benki.


Sasa Harmonize kashindwa kulipa M 100,Huu upuuzi,Sitaicha kazi ya ualimu kamwe,hapa navuta Muda nije niende nikavute mpunga M 32 nione mtu ananilaumu Kwa kutegemea mikopo , nijivinjari zaidi.Asante Mungu kwa kazi ya ualimu,Kiufupi huwezi toboa maisha bila kukopa ,kama unakopesheka kopa
Retirement date 20/07/2047.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Huyu namjuwa tokea anasoma kumbukumbu pale wakati huo naishi nyumbani blok 41,kundi lao walikuwa na Joan pia na mwenzake mmoja anaitwa Rose
Hawa hawazeeki bana
Pale osterbay alikuwa anakaa kwa baba yake polisi mzee masanja na mama yake pia alikuwa polisi
Washaastafu sahv wanakaa mbezi makoka huko
Huyu kajala kaanza kusasambua kitambo sana wakati huo kwenye beach party unawakuta,pale langata club asset washafanya sana vurugu...anyway sahv wageni wanamuona kama toto la jana 😄
Kajala ana udongo mzuri bana
Harusi yao na faraji walifanyia pale police mesi ilikuwa balaa yaani,pombe tulibeba bana na kuondoka nazo
Sema ndy hivyo kwa upande mwingine naona faraji kama aliharibu future yake kuangukia kwa Huyu mdogo wangu na ktk watu waliomuonya huyu faraji mm mmoja wapo sema mtu akikolea bwana kumzuia ngumu sana

Ova
Daaaah maisha ni fumbo.
 
hawana lolote hao CRDB

wangekuwa wanajua banking and lending wangeshikilia dhamana

Konde Boy, wapige kisawa sawa hao wasomi uchwara wa CRDB

Walikutaka ufungue akaunti ya. biashara ili waone miamala yote ya maokoto na ma bills ya kampuni.

Biashara went burst, and they see all the accounting records, what they what you to do, rob the bank to pay the bank ?

Wamezoea predatory lending kwa wanyonge wasio na sauti. Konde, kaza hapo hapo. We don't commiserate with these predatory banks. Eff them!

Sio kweli, CRDB walimkopesha on Trust, maana amekuwa anatumikia kwenye matangazo yao, ili kuwa na uhakika wa kulipwa Deni lao wakamuimba afungue akaunti kwenye benki yao ili iwe rahisi kukata Deni la mkopo na interest ya mkopo.
 
Kumbe kesi yenyewe imesikilizwa upande mmoja/ exparte

Hapa Armo anarudi kwenye kesi akitoa sababu za msingi wanatudi interparties kesi isikilizwe pande zote mbili

Anarudije kusikiliza kesi wakati trial imeisha? Alikuwa na wakati wa kujitetea mahakamani ila akachagua kula Kona, nadhani aliona gharama kutafuta wakili.
 

View attachment 3072826
View attachment 3072827

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.

Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.

Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kibiashara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.

Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.

CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.

Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755/=
Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.

Chanzo changu na mimi,

Nifah.
🎼🎵🎶. . . Kajala 1 & 2 tena zote ni range. . .
 
Mazuri ya kujifunza kwa Harmonize!

1. Msela ana uthubutu na ujasiri.

2. Anajitambua na amejipata.

3. Funguo za mafanikio anazo na anaifahamu milango yenye fedha.

4. Rafiki mkubwa wa benki na ndio maana CRDB wamempa mkopo na wakamuongeza tena ila inawezekana amefanya urafiki na benki nyingine tofauti ndio maana CRDB wakastuka na kuchukua hatua! Ndio maana walitaka pesa za biashara zipitie kwa akaunti ya CRDB.

5. Uwezo na nia ya kulipa deni upo na anao isipokuwa amepuuza kufanya mawasiliano hicho ndio kimemgharimu.

Mengineyo, tujiulize mimi, wewe na yule wanayeshadadia kumkandia msela, je, tunaweza kupata mkopo kama wa msela CRDB? Je, wewe au mimi ni rafiki wa benki?

Tukubali au tukatae jamaa ni mwamba amewazidi uwezo wa kukopa madaktari, walimu, manesi na wataalamu wengine. Badala ya kumnanga msela tumpeni maua yake.

By the way issue yake ni ndogo sana kama mbegu ya haradali, kesho jamaa akiweka mzigo kwenye akaunti ya CRDB anakaribishwa kahawa na kashata au juice kwenye ofisi ya meneja wakigonga cheers kama premium customer. Kwa hiyo jamaa hapangi foleni akifika benki kama watumishi wengine au mapolisi na wanajeshi wanavyopanga foleni.

Tuweke akiba ya maneno sababu mimi na wewe hatujui msela amepitia changamoto gani hadi ikatokea hivyo.

Punguza maneno mengi, mwambie alipe mkopo wa watu.
 
Huyu namjuwa tokea anasoma kumbukumbu pale wakati huo naishi nyumbani blok 41,kundi lao walikuwa na Joan pia na mwenzake mmoja anaitwa Rose
Hawa hawazeeki bana
Pale osterbay alikuwa anakaa kwa baba yake polisi mzee masanja na mama yake pia alikuwa polisi
Washaastafu sahv wanakaa mbezi makoka huko
Huyu kajala kaanza kusasambua kitambo sana wakati huo kwenye beach party unawakuta,pale langata club asset washafanya sana vurugu...anyway sahv wageni wanamuona kama toto la jana 😄
Kajala ana udongo mzuri bana
Harusi yao na faraji walifanyia pale police mesi ilikuwa balaa yaani,pombe tulibeba bana na kuondoka nazo
Sema ndy hivyo kwa upande mwingine naona faraji kama aliharibu future yake kuangukia kwa Huyu mdogo wangu na ktk watu waliomuonya huyu faraji mm mmoja wapo sema mtu akikolea bwana kumzuia ngumu sana

Ova
Sasa mwanamke kama Kajala unalala na kuamka naye hata maisha yako yakiharibika unakuwa umepoteza nini?

Kajala ni mzuri jamani sio filter wala AI. Halafu ana aibu flani makes her even more beautiful.

Ningekuwa mwanaume mimi…au basi
 
Back
Top Bottom