Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mbo
Mkopo huo ulikuwa wa Dhamana ya Ardhi (Nyumba) (Mortgage) au ni wa Nini hasa??? Dhamana au rehani aliweka assets gani ili kudhamini huo mkopo? Milioni 300 aliwezaje kukopeshwa na benki ya CRDB kiurahisi hivyo bila ya kuweka rehani mali yake yoyote ile? Ina maana kwamba alikopeshwa pesa nyingi kiasi hicho bila ya Mkopeshaji (Crdb) kujiridhisha Kwanza kuhusu uwezo wa mtu huyo wa kulipa marejesho ya deni lake???

Anyway, mkopo siyo sadaka, Mkopaji alipaswa kukopa kwa malengo.
Dawa ya deni ni kulipa.
Mbona hela ndogo tu hiyo,ukiwa na business plan na una kipaji unapewa mkopo ,kwani maofisini stadg wakichukua mkopo dhamana huwa ni nini,hiyo ni hela ndogo kwa msanii wa kaliba yake
 
Hamonize amuulize 50 cent hasara ya wanawake wenye makalio, utaishia kufilisika tu.

Diamond alishtuka mapema sana wanawake wenye makalio ni muflisi akaachana nao. Kaamua kujitaftia low profile wake ajilie taratibu.
 
View attachment 3072517

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.

Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.

Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kiabishara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.

Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.

CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.

Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755. Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.

Chanzo changu na mimi,

Nifah.
Mwenzake alikopa akafungua studio na baadae akaenda kuwekeza kwenye media.
Kweli penye miti hakuna wajenzi.
 
"Ni Ujinga nikadondokea umachinga,hapo ndipo akili ikaanza kukomaa na nikajuta kwanini sikusoma kwa jinsi jua la la utosi linavyochoma."

"Kama utani nikaanza kuimba ,Mungu si athumani nikakutana na simba akanipa kampani ila kuna wengine waliopinga eti sina kipaji wakashindwa kuelewa mola ndiyo mpaaji."

JESHI hiyo mistari inanipa morali ya kupambana sana...ebu lipa madeni buana uza hata LC300 moja ,kugombana na mabank inakuharibia future yako.
 
Mkopo huo ulikuwa wa Dhamana ya Ardhi (Nyumba) (Mortgage) au ni wa Nini hasa??? Dhamana au rehani aliweka assets gani ili kudhamini huo mkopo? Milioni 300 aliwezaje kukopeshwa na benki ya CRDB kiurahisi hivyo bila ya kuweka rehani mali yake yoyote ile? Ina maana kwamba alikopeshwa pesa nyingi kiasi hicho bila ya Mkopeshaji (Crdb) kujiridhisha Kwanza kuhusu uwezo wa mtu huyo wa kulipa marejesho ya deni lake???

Anyway, mkopo siyo sadaka, Mkopaji alipaswa kukopa kwa malengo.
Dawa ya deni ni kulipa.

Mkuu umesahau kwamba MAGU alikuwa anamkubali KONDE kinoma? Possible KONDE alitoa proposal kwa JIWE then JIWE simu moja kwa KIMEI ,kimei akatoa KIBUNDA.
 
View attachment 3072517

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rajabu Abdukahali Ibrahim almaarufu Harmonize ametiwa hatiani na mahakama kuu divisheni ya biashara tarehe 2 mwezi huu wa 8 kwa kushindwa kulipa kikamilifu mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 300 alizokopa katika benki ya CRDB mwaka 2019.

Mkopo huo uliokuwa na riba ya 18% ulielezwa na msanii huyo kama uwekezaji kwenye shughuli zake za kimuziki ikiwemo studio ya kisasa ya uzalishaji wa muziki na video, ulikuwa ulipwe ndani ya miezi 36 (miaka mitatu).
Na ulikuwa mkopo wa awamu mbili, ya kwanza ikiwa milioni 100 kisha awamu ya pili milioni 200 ambazo awamu zote alipewa na benki hiyo mwaka huohuo wa 2019.

Moja ya makubaliano ilikuwa (Harmonize) kufungua akaunti ya kibiashara katika benki hiyo kisha kuiweka milioni 100 na kuifanya akaunti hiyo kuwa akaunti yake kuu katika shughuli zake za kiabishara, takwa hilo pamoja na mengine ikiwemo marejesho ya mkopo kwa kila mwezi yalishindwa kufikiwa na Harmonize.

Baada ya usumbufu uliopitiliza wa ulipaji wa mkopo huo kutoka kwa Harmonize, CRDB walifikia uamuzi wa kwenda mahakamani. Uamuzi huo ambao mahakama ilitoa wito mara kadhaa kwa Harmonize, lakini Harmonize hakufika mahakamani. Na hata mahakama ilipomuomba kutoa maelezo (Written statement of defence WSD) hakufanya hivyo.

CRDB waliendelea kumkumbusha Harmonize kulipa mkopo kila mara na kila njia hadi zikiwemo jumbe za WhatsApp, mwanzoni mwa mwaka 2022 Harmonize aliandika barua kwenda tawi la benki hiyo lililopo Mlimani City akiomba kulipa marejesho kwa kiasi cha 3.3 milioni badala ya utaratibu uliowekwa wa 10.8 milioni kila mwezi wakati huo deni la mkopo likiwa 109,731,733.46/= CRDB walikubali ombi lake hilo ila akitakiwa kulipa 3.9 milioni badala ya 3.3 milioni aliyokuwa ameomba.

Harmonize alifanikiwa kupunguza deni hilo hadi kufikia kiasi cha 103,185,755. Baada ya hapo hakulipa tena hadi kufikia hukumu iliyotolewa 2/08/2024 ambapo msanii huyo ametakiwa kulipa kiasi chote kilichobaki katika mkopo, gharama za kesi na fidia ya milioni 10 na nyinginezo kama mahakama ilivyoona.

Chanzo changu na mimi,

Nifah.
Mbwembwe zote hizo kumbe harmonize hamna kitu. Show off za kishamba. Wanaanza kuumbuka. Tunawasubiria kina chiefgolove na dj ally b.

King Kong III mrangi
 
Nakala ya hukumu ninayo, ila sitoiweka hapa.
Screenshot_20240817-161234~2.png
Screenshot_20240817-161240~2.png
Screenshot_20240817-161244~2.png
Screenshot_20240817-161250~2.png
Screenshot_20240817-161255~2.png
Screenshot_20240817-161259~2.png
Screenshot_20240817-161304~2.png
Screenshot_20240817-161309~2.png
Screenshot_20240817-161313~2.png
Screenshot_20240817-161316~2.png
Screenshot_20240817-161320~2.png
Screenshot_20240817-161324~2.png
 
duwh juz kati nilikutananae classic mall yuko na range moja matata kaingia crdb moja kwa kwenye getto la branch manager tukasema dah mwamba kishapita level za kukaa kwente mnyororo yeye fungu anaenda kuchukulia kwa wakubwa kabisa.
kumbe muhuni ana majanga makubwa kuliko sisi
 
Back
Top Bottom