Mahakama yamtia hatiani Zitto Kabwe katika kesi yake ya Uchochezi. Atakiwa kutotoa matamshi ya Uchochezi kwa mwaka 1. Asema kukata Rufaa

Leo ni msiba mkubwa kwa vijana wa lumumba maana walikuwa wanaombea Zitto apigwe mvua za kutosha

Hizo ni ndoto za mchana kweupe. Jambo usilolijua bora kubaki kimya.
 
Kutoka kwenye hukumu kuna maneno yanasema "Zitto hasijiusishe na uchochezi mwaka mmoja" Sasa unakaa unajiuliza inakuwaje mtu umzuie kufanya uchochezi kwa mwaka kwahyo baada ya mwaka ni sawa kufanya uchochezi? hii ni moja ya hukumu ya kipumbavu sana.

Mkuu umesomea sheria?
 
Bloomberg - ''Tanzania Convicts Opposition Chief of Sedition Ahead of Election''

Wameanza kulialia kama kasuku! ''Ukitaka kuua nyoka gonga kichwani.''
 
Utabiri mwingine buana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mtoa post mbona bado una ufala? Zito katiwa hatiani Na kuhukumiwa mwaka 1 kifungo cha nje kwa sharti la kutotoa neno lolote la uchochezi
 
Mkuu conviction ya mhe. Huruma shaidi kwa zito ni ya ajabu sana, unaposema nimekuachia huru ila usiseme maneno ya uchochezi ndani ya mda fulani ana maana kwamba amemtia hatiani zito?

Mkuu, hili ni kosa kubwa sana kwa hakimu. Kuna kupatikana na hatia au kutopatikana na hatia. Kama Zitto hakuwa na hatia ilikuwa inatosha kumwachia. Kosa lingine atalofanya Zitto halipaswi kuhusishwa kwa namna yoyote na shitaka hili ambalo hakukutwa na hatia.

Tuna au majaji wanasiasa au wanaotoa hukumu za hisia.
 
Kwa hiyo kisheria baada ya mwaka mmoja mahakama inampa ruhusa Zitto kutoa maneno ya uchochezi?
 
Tanzania opposition leader banned from comment ahead of vote

A Tanzanian court has banned an opposition leader from making “seditious” statements for one year, just months ahead of the election in which President John Magufuli seeks a second term

Credit: TOM ODULA Associated Press

''A Tanzanian court has found an opposition leader guilty of sedition and banned him from making public statements for one year, just months ahead of the presidential election.

The magistrates court released Zitto Kabwe, leader of the ACT-Wazalendo party, on the condition that he does not make “seditious” statements for a year.

It is not clear who decides what statements are seditious in the East African country, and human rights groups have called for the related colonial-era laws to be repealed. Kabwe's party said it will appeal the decision.

“The judgment and related conditional discharge is tantamount to censorship, effectively barring Zitto from saying anything critical of the government and the president during an election year,” vice chair Dorothy Semu said in a statement. Kabwe has been among the most vocal critics of President John Magufuli's five-year rule. Magufuli seeks reelection in October.

Rights groups accuse Magufuli's administration of stifling criticism, targeting independent journalism and severely restricting the activities of non-governmental organizations. Opposition parties have been banned from political activities including public rallies. Kabwe, a lawmaker, was accused of making seditious statements in 2018 during a press conference in which he asserted that 100 people had been killed in clashes between cattle keepers and police in Uvinza district.

His sentence comes weeks after the national chairman of the opposition Chadema party, Freeman Mbowe, and eight others were sentenced to serve a five-month jail term or pay or fines for charges including conspiracy to commit offences, unlawful assembly, sedition and incitement.''

Tanzania opposition leader banned from comment ahead of vote

Tabia hua haibadiliki mzushi kakutana na 40 zake. Alizusha JPM amefariki na kwenda kutibiwa Germany hakuridhika. Akazusha Tanzania isipate mikopo nk sasa kidomo domo chote kwishnei afunge tu account zake za twitter na kuacha kuropoka kwa mwaka moja.
 
*TAARIFA KWA UMMA*

Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mshtuko taarifa ya kutiwa hatiani kwa Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe ambaye alishitakiwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu na kukabiliwa na mashtaka matatu chini ya Sheria ya Vyombo vya Habari.

Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa leo na Hakimu Huruma Shaidi, Ndugu Zitto ametiwa hatiani kwenye makosa yote matatu na kuachiwa huru kwa sharti la kutotoa matamshi ya kichochezi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Ndugu Wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo, kwa sasa itoshe tu kusema kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinapokea na kuyaheshimu maamuzi ya Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu yaliyotolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi na kwamba kwa sasa Chama kinasubiri kupokea ushauri wa mawakili wa Ndugu Zitto Kabwe kuhusu tafsiri ya hukumu hiyo na hatua sahihi za kuchukua.

Muda mfupi uliopita, nimeongea na Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!

Wakati tukiendelea kusubiri tafsiri na ushauri wa wanasheria, nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama kuwataka wanachama wote mtulie katika kipindi hiki huku mkisubiri taarifa mbali mbali zitakazotolewa na Chama kupitia viongozi wenu.

Tunachukua fursa hii pia kuwapongeza mawakili wote ambao wamefanya kazi kubwa sana tangu mwanzo hadi mwisho wa kesi hii. Mawakili hao ni Stephen Mwakibolwa, Bonifasia Mapunda, Peter Kibatala, Jebra Kambole na Jeremia Mtobesya.

Asanteni na nashukuru sana!

*Dorothy J. Semu,*
*Makamu Mwenyekiti Bara,*
*ACT Wazalendo.*
*29 Mei 2020.*
 
Mapambano na yaendelee. Hakuna To me Huru, Hakuna Uchaguzi.

Tuwajue wachumia tumbo.

Maghufuli Tano Tena
 
Watajijua wenyewe sisi tupo na Magufuli kwenda uchumi wa kati
 
"Kiongozi wetu na amenihakikishia kuwa yupo imara na kamwe hukumu hii haitamrudisha nyuma. Mapambano ya kuondoa mfumo kandamizi na uchumi goigoi lazima yaendelee. Aluta Continua!!"

kwa hiyo ndio sababu inayomfanya atoe matamshi ya kichochezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…