Mahakama yamuamuru Shilole kumlipa Mary Musa TZS 14M kama fidia ya kutokuhudhuria kwenye show

Mahakama yamuamuru Shilole kumlipa Mary Musa TZS 14M kama fidia ya kutokuhudhuria kwenye show

Pumbavu zake yeye na kale katoto ka uchebe walipe tu kama hawana pesa wafungwe tu
 
Imefika kipindi sasa, Mziki au sanaa kwa ujumla iwe kazi rasmi yaani msanii apate anachostahili na aichukulie sanaa kama kazi rasmi
 
haya sasa wale waliomchangia kwenye harusi wamchangie tena kwenye matatizo.....hapa ndio pa kuwajua binadamu vizuri.
kwenye raha wako na wewe kwenye shida uko peke yako
 
Hii ni fundisho kwa wasanii wetu alikuwa analia sana , alitumiwa summoms mpaka kwenye gazeti lakini akajiona star..Sasa kale kamgahawa sijui katafika milion 14 na gharama za court brokers.

 
Shilole aangua kilio baada ya mahakama kutoa hukumu kumtaka alipe million 14 za kitanzania kwa Mary Musa.

Mwaka 2017 katika mkesha wa Pasaka Shilole alilipwa mil.3 akatumbuize huko Mbagala lakini alishindwa kutokea kwa wakati hivyo mashabiki kupandwa na hasira na kuharibu Mali ukumbini Hapo.

Mary alifungua kesi kuomba alipwe fidia lakini Shilole akawa anapuuza wito wa mahakama.

Shilole ametakiwa kutoa pesa hizo ndani ya wiki moja la sivyo Mali zake zitashikiliwa.

Crediti: GPL
------------
Safi sana Mahakama, ni wakati sasa wa wanasanaa wetu kujua umuhimu wa kuheshimu sheria na kuheshimu mikataba.
Atalipiwa na kiongozi wa wanyonge😀
 
Leo March 1, 2018 Msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amehukumiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 14 na mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya kutapeli na kusababisha hasara kwa kushindwa kufika kwenye shoo.

shilole-1-660x394.jpg


Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu imethibitika kuwa Shilole alilipwa kiasi cha Shilingi Milioni tatu na Mary Musa kwa ajili ya kutumbuiza siku ya mkesha wa Pasaka mwaka jana 2017 katika Ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala-Kijichi jijini Dar es Salaam lakini alishindwa kutokea kwenye shoo hiyo kama walivyokubaliana.

Kutokana na kitendo hicho, mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo walipandwa na hasira na kufanya fujo huku wakiharibu mali ukumbini hapo na kumsababishia mwandaaji ambae ni Mary, hasara ya Shilingi Milioni 14 ambazo mahakama imeamua Shilole azilipe kama fidia kwa mlalamikaji.

Chanzo: Millard Ayo
 
Akimpata wakili mzuri anaweza kupunguziwa adhabu na kuamriwa arudishe mil 3 aliyolipwa. Suala la uharibifu yeye alimhusu kwani aliyeandaa show alipaswa kuweka ulinzi imara

what if kwenye mkataba pameandikwa m14 kama hatohudhuria? wabongo huwa hatusomi kabisa contract tunapitia juu juu tu au lugha ilimchanganya maana mikataba ya kiingereza mmh
 
Akimpata wakili mzuri anaweza kupunguziwa adhabu na kuamriwa arudishe mil 3 aliyolipwa. Suala la uharibifu yeye alimhusu kwani aliyeandaa show alipaswa kuweka ulinzi imara
Acha kumdanganya uharibufu usingetokea endapo angetokea kwenye show. Kwa hiyo yeye ndio chanzo cha uharibifu
 
Back
Top Bottom