benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Mahakama ya Rufani Morogoro, imetupilia mbali rufani ya Justine Chamashine aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua dereva wa bodaboda, Joseph Frorence 'Msimbe'.
Uamuzi huo ulitolewa wiki iliyopita na Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma. Majaji wengine ni Augustine Mwarija na Othman Makungu.
Chamashine alikata rufani kupinga hatia na adhabu aliyopewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Majaji hao walisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili wamebaini hoja za rufani hazina mashiko na Mahakama Kuu ilimhukumu mrufani kwa usahihi. Walibainisha miongoni mwa hoja za mrufani kupinga adhabu hiyo ilikuwa ni kwamba Mahakama Kuu ilikosea kumhukumu kwa kutumia ushahidi wa kukutwa na vitu vya marehemu huku kukiwa hakuna ushahidi iwapo wakati Msimbe anauawa alikuwa akitumia pikipiki aliyokutwa nayo yeye.
Pia, alidai hakuna ushahidi wa malalamiko unaomuunganisha mrufani na pikipiki iliyoibwa kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kumuita Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuthibitisha umiliki wake.
Wakizichambua hoja hizo, Majaji walisema Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa sahihi kusema mrufani ndiye aliyemuua Msimbe. Aidha, walisema ushahidi unaonyesha mrufani alikamatwa na polisi akiwa anamiliki pikipiki hiyo ilithibitishwa na mmiliki wake halali ambaye alimkabidhi Msimbe kufanya biashara ya kubeba abiria Januari 6, mwaka 2017.
Ilielezwa Januari 9, mwaka 2017, Msimbe aliuawa na siku iliyofuata saa 7:30 mchana askari walimkamata mrufani akiwa anaendesha pikipiki hiyo, ndipo walipomfungulia shtaka la mauaji kwasababu alikutwa na pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Msimbe.

Majaji hao walisema kwa ushahidi huo, hawaoni hitimisho lingine isipokuwa kama Jaji wa mahakama ya chini alivyoeleza kwamba mrufani alihusika na mauaji ya Msimbe na kuiba pikipiki.
Majaji hao walisema kutokana na hali hiyo wameona hoja za mrufani hazina mashiko, hivyo wanaitupa rufani kama ilivyokatwa. Chamashine alitenda kosa hilo, Januari 9, mwaka 2017, eneo la Kikwaraza, Kata ya Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro.